Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe leo ameendelea na ziara yake kwa kuingia kwa kishindo wilayani Itilima mkoa wa Simiyu akitokea mkoa wa Tabora alikohutubia halaiki ya watu Nzega hapo jana.
Mara baada ya kuingia wilayani Itilima Kiongozi huyo wa Kambi Rasmi ya upinzani bungeni amelakiwa na msururu wa magari,pikipiki na baiskeli huku wananchi wakijipanga kandokando ya barabara na kupeperusha majani ya miti.
Kwa sasa Mwenyekiti huyo wa Ukawa anahutubia umati mkubwa wa watu katika kijiji cha Legangabilili wilayani humo
Tunaungana na Kamanda Standalone aliyeko kwenye msafara wa Mwenyekiti kutuletea Live updates..
Karibuni...
Mara baada ya kuingia wilayani Itilima Kiongozi huyo wa Kambi Rasmi ya upinzani bungeni amelakiwa na msururu wa magari,pikipiki na baiskeli huku wananchi wakijipanga kandokando ya barabara na kupeperusha majani ya miti.
Kwa sasa Mwenyekiti huyo wa Ukawa anahutubia umati mkubwa wa watu katika kijiji cha Legangabilili wilayani humo
Tunaungana na Kamanda Standalone aliyeko kwenye msafara wa Mwenyekiti kutuletea Live updates..
Karibuni...
Leo Mwenyekiti wa Chadema Taifa yupo Mkoa wa Simiyu katika siku ya pili ya ziara yake.
Yupo katika,
Wilaya: Itilima
Kata: Lagangabilili
Kijiji: Lagangabilili.
Kabla ya kula Kiapo Mwenyekiti Mbowe alipewa baraka na wazee wa kisukuma nabkukabidhiwa mkuki na ngao kwa ajili ya utetezi wa taifa
Mwenyekiti anazindua mpango wa FTP 200 wa Ulinzi na Usalama wa Chama na viongozi na mali za Chama.
Mwenyekiti Mbowe aliwasili katika Kijiji cha Lagangabilili majira ya saa saba mchana akutokea Mkoani Tabora ambapo alizindua mpango wa FTP 200 Katika Wilaya ya Nzega, Kata ya Ndala.
Baada ya kuwasili Lagangabilili- Wilaya ya Itilima Mwenyekiti alikwenda katika Ofisi ya Chadema Wilaya ya Itilima na kusaini Kitabu cha wageni na hatimaye akawasili katika eneo ambalo kuna Kambi ya Vijana ambao wakuwa Kambini wakipata mafunzo katika eneo la wazi ya Ujasiriamali endelevu, Ulinzi Shirikishi, Uzalendo, Kupambana na rushwa pamoja na sheria na taratibu za uchaguzi.
Mwenyekiti alielezwa na Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema Wilfred Lwakatare kuwa vijana hao pia wana mafunzo ya uwakala pamoja na hamasa za kwenda kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la Wapiga kura.
Akihutubia vijana hao baada ya kula kiapo Mwenyekiti alisema kuwa idadi ya polisi ukilinganisha na idsdi ya watu ni ndogo sana ukilinganisha na vigezo vya Umoja wa Mataifa. Hivyo ni lazima wajilinde.
Aliwataka Msajili wa vyama na IGP kuachana na propaganda za kisiasa kwa sababu kujilinda ni haki ya kikatiba na kisheria.
Mwenyekiti atapata chakula pamoja na wananchi na wahitimu wa mafunzo kwenye uwanja huu ambao ni Kambi.
Picha zina kuja soon usiondoke...
![]()
![]()
![]()
Kaa tayari kwa picha zaidi wakati wa mkutano,,,,,Umati mkubwa tayari ushaanza kuwasili eneo la mkutano....
![]()
Mwenyekiti akipata chakula cha mchana na vijana wa Red brigade waliokuwa wamehitimu mafunzo
Akipata pia chakula na wenyeji wa kata ya Lagangabilili mara baada ya kuzungumza ni vijana hao waliokuwa mafunzoni
Mkutano wa hadhara umeanza na alianza kuhutubia Mwenyekiti wa Kijiji cha Lagangabilili kwa tiketi ya Chadema ambaye alisema yafuatayo;
1. Wilaya ya Itilima ni mpya lakini maeneo mengi hayajapimwa na watu hawaruhusiwi kuendeleza maeneo yao
2. Maeneo ya wananchi yaliyotwaliwa kwa ajili ya ujenzi wa makazi ya serikali wananchi hawajalipwa fidia.
3. Mkuu wa Wilaya ya Itilima anawagawa watu kikabila katika Wilaya ya Itilima.
4. Serikali wanatutaka kupunguza ng'ombe lakini malori yanaua watu kila mara lakini hawajawahi kuambiwa wapunguze.
5. Serikali yake imefuta michango na kulipia gharama zisizo na msingi za kiutawala i.e mihuri.
=====More Updates======
Mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti- Mhe. Kasulumbai alisema yafuatayo;
1. Wasukuma sisi ni wengi lakini wametumia umaskini wetu kutuibia rasilimali
2. Mwaka huu ni wa uchaguzi tuchague wabunge na madiwani wengi wa Chadema.
3. Akina mama, wazee, vijana tujitokeze kujiandikisha.
4. Zao la Pamba bado halijawanuaisha wananchi.
===Mhe. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Musoma Mhe. Alex Malima Kisurura ====
1. Alimtaka Mwenyekiti wa Kijiji wa Lagangabilili kuwa asilalamike matatizoyao ni kwa sababu walifanya makosa kuchagua madiwani wengi wa CCM. Wawaondoemwaka huu kwenye uchaguzi mkuu Oktoba
2. Alisema amepata taarifa kuwa madiwani wa Itilima walivunja kikao kwasababu ya kukosa posho. Ni aibu kubwa badala ya kuzungumza masuala ya maendeowanashindwa kwa sababu ya posho.
3. Aliendelea kusema kuwa katika Halmashauri anayoongoza alikuta akina mamawanalala watatu kwenye kitanda kimoja. Kwa sasa Halmashauri chini ya Chadematatizo hilo limekwisha na huduma za afya zimeboreshwa.
4. Halmashauri yake walifuta kitu kinachoitwa michango ya maabara. Na hilolimefanikiwa kwa kuongeza mapato na kujenga Halmashauri na sio kuwasumbuawananchi.
===Mwenyekiti Taifa amepanda jukwaani na ameanza kusema yafuatayo=========![]()
![]()
1. Sukuma land imebarikiwa rasilimali nyingi lakini badp watu wake nimaskini.
2. Alitolea mfano wa almasi ya Mwadui ambayo imechimbwa miaka mingi lakinibado haiwanufaishi wananchi.
3. Kwa sasa Itilima na Bariadi zina takribani watu laki 7 na nusu lakiniukiuliza kuna shuke ngapi za Sekondari utapata aibu tupu.
Kwa matatizo haya yote bado mliichagua CCM mwaka 2010. Tunahitaji kufanyamabadiliko makubwa mwaka huu 2015.
Mwenyekiti aligusia matatizo ya zao la Pamba na kuwakumbusha wananchi kuwaKambi Rasmi ya Upinzani anayoiongoza walisemea kuhusu mbegu feki iliyosambazwakatika msimu uliopita ambayo ilisababisha hasara kubwa kwa wananchi. Serikaliilikubali kuwalipa wananchi fidia lakini mpaka leo hilo halijatekelezwa.
Aliongeza kuwa amepata taarifa kuwa wananchi wanauza pamba kwa mkopo na kwabei rahisi, hilo halitakubalika. Ni lazima kama Chama watachukua hatua kuzuiahilo.
Mwenyekiti aligusia suala la elimu na kuwaambiakuwa Serikali ya CCM imeharibu mfumo wa elimu. Unazaliwa Bariadi, unakuliaBariadi, unaoa Bariadi na unafia Bariadi. Hii ni tofauti na mfumo wa zamani waMwl Nyerere.
====More===
Alitolea mfano Jimbo lake ambapo ana Vijiji 64, na vijiji vyote 64 vina maji safi na salama. Akasema katika vijiji 64 anazo shule za sekondari 72. Akawataka wananchi kufanya mabadiliko makubwa ya kiutawala kwenye uchaguzi mkuu ili kuleta mabadiliko
Mfumo wetu elimu ni umeharibiwa ndio maana tunazidiwa na Kenya. Hata Rwanda ambayo waliuana wenyewe kwa wenyewe leo wana mfumo bora wa elimu kuliko sisi.
==More===
Mwenyekiti alisema kuwa zamani walikuwa wanaomba watu kujitokeza kugombea kupitia Chadema lakini mpaka sasa Chama kina watia noa 17 katika Jimbo la Itilima. Mwenyekiti aliwaasa watia nia kutowagawa wananchi pale ambapo wengine watakosa nafasi ya kuteuliwa.
Mwenyekiti amewapa nafasi watia nia wote waliopo mkutanoni kujitambulisha na kuwasalimia wananchi ila wawafahamu.
Mwenyekiti alisema Chadema wanatarajia kuwa na wabunge, si wabunge wengi tu bali wabunge bora.
Mwenyekiti aliwasimamisha pia watia nia wa Udiwani katika Kata zote 22. Ambao Jumla ya watia nia ni zaidi 90. Kutokana na muda alishindwa kuwapa nafasi ya kusalimia na kujitambulisha. Aliwataka wakichaguliwa mwaka huu kulinda rasilimali za nchi vizuri ikiwemo matumizi mazuro ya fedha.
Mkutano Umemalizika hapa na watu wameondoka wakiwa na shauku na hamasa isiyo ya kawaida.
Mkutano uko mwishoni na dalili sa Mvua zimeanza .Kesho MWenyekiti atakuwa Ukerewe kaeni mkao wa kula kwa updates, Lazima tuonyeshe tofauti
Nawashukuru sana wote mliokuwa hapa Japo Jukwaani,Japo kuna tatizo la network huku ila tumejitahidi sana kusammmarize.
Mungu Awabariki wote Peopleeeees .Natumaini Umejibu Poweeeeeeeeeer.
Nikiriport Moja kwa Moja kutoka Simiyi Ni Mimi Kamanda wenu Standalone
Last edited by a moderator: