No, ni jeuri ya pesa. Si ulimsikia juzi akimtukana Waziri Silinde kule Mbozi eti alimnunulia suti na chupi akiwa Chuo Kikuu? Ni jeuri ya pesa, pesa za urithi changanya na biasharabiashara kama Bilicanas. Aliwahonga wote wakiwa Chuo Kikuu, watoto wa familia maskini, ndiyo maana hachoki kuwasema. Ku a huyo Silinde, Zitto, Asha, Heche, Halima, Mrema, Waitara, wote hawo. Na utakumbuka mwaka ule alipokuja Lowassa kutaka Urais, jamaa alichukua donge nono. Ni jeuri ya pesa. Pia kila anayetaka vitimaalum kuna mchango wake, wanajua. Baada ya muda hugundua kumbe jamaa ni Darasa la Saba, ndipo humkimbia kama kina Zitto na huyo Waziri. To be fair, marehemu Baba yake alikuwa Muasisi wa TANU, kipenzi cha Julius Nyerere. Pamoja na utajiri wake yeye na John Rupia hawakuwahi kumsaliti.