Freeman Mbowe aheshimiwe

Mtukudzi

Senior Member
Nov 14, 2013
103
408
Nimekaa na kutafakari sana. Nimemtafakari bwana Freeman Mbowe. Binadamu huyu anatakiwa apewe heshima kubwa sana.

Yeye siyo adui wa nchi hii, la hasha! Mbowe ametoka kwenye jamii iliyostaaribika sana. Alichofanya tangu enzi zile mpaka Leo ni kuwafanya watanzania wawaze nje ya box. Kwamba lazima pawepo na siasa za ushindani ili kuleta maendeleo.

Ushindani ni ukuaji. Amefanya makubwa kuliko wale tunaowaheshimu kwa kuwa wako madarakani.

Mnyonge mnyongeni lakini mpeni haki yake.

Freeman Mbowe aheshimiwe
 
Wananchi wanamuheshimu sana Mh. Mbowe wanajua umuhimu wa upinzani na mchango wake katika siasa za nchi yetu...tumefika hapa tulipo mainly kwa sababu ya kujitoa kwake.

Tatizo ni hawa vijana wachache wa Mzee Polepole ndiyo waporomosha mitusi na maneno ya kuudhi sababu bila kufanya hivyo hawapati buku saba ya kula kwa siku....hunger ni mbaya sana kama ukiiendekeza kupita kiasi...ina uwezo wa kutawala hadi brain yako!! Yaani thinking yako ikawa ya ki njaa njaa!!
 
Kimsingi binafsi namheshimu na kumkubali sana huyu mdau kwa mengi, upole, busara, hekima na uwezo wa uongozi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Binafsi Mbowe namheshimu....ila ana watu ndani ya Chadema wenye siasa Kali na za ubabe na hata za kigaid.Hao ndio wanamuangusha Mbowe...yeye Kama yeye sioni Kama ana tatizo..
Ila anazidiwa na 'wahuni' ambao nadhani wana sauti kubwa kwa maamuzi ya kiuanaharakati
 
Mungu mbariki Freeman Mbowe , nguzo ya amani Tanzania
FB_IMG_1570488518462.jpg
 
Kweli ni lazima aheshimiwe kwanza ni mwenyekiti wa maisha hilo si jambo dogo, hata serikali ya awamu ya 5 ilifanya makosa kumtupia vitu vyake nje yeye hastahili kulipa kodi yeye ni mkwepa kodi wa maisha. Hata hayo matumizi mabaya ya fedha za chama ni kosahata kumtaja kwani yeye ni mtumiaji wa pesa za chama wa maisha.
Ni kweli lazima tumueshimu sana Mbowe kwani alibadilisha Gia box angani kama futi 300 kutoka usawa wa bahari bila kuangalia usalama wa watu na chombo chenyewe wakati giabox inabadiliswa ndege ikiwa chini.

Anaitaji kuheshimiwa sana kwani ameleta kitu ambacho hakijawa kuonekana tangia 9 Desemba 1961 hadi alipofika yeye tabia ya kuwafundisha wabunge wake kususa na hata kususia chaguzi na inasemekana uchaguzi wa 2020 amesha andaa utaratibu huo wa kususia uchaguzi hili kuingia barabarani tujiandae.
Ata uteuzi wa viti maarumu pia amekuwa anaitaji heshima kwani ametimiza amli ya Mungu kwenda kuijaza dunia.
 
Nimekaa na kutafakari sana. Nimemtafakari bwana Freeman Mbowe. Binadamu huyu anatakiwa apewe heshima kubwa sana.

Yeye siyo adui wa nchi hii, la hasha! Mbowe ametoka kwenye jamii iliyostaaribika sana. Alichofanya tangu enzi zile mpaka Leo ni kuwafanya watanzania wawaze nje ya box. Kwamba lazima pawepo na siasa za ushindani ili kuleta maendeleo.

Ushindani ni ukuaji. Amefanya makubwa kuliko wale tunaowaheshimu kwa kuwa wako madarakani.

Mnyonge mnyongeni lakini mpeni haki yake.

Freeman Mbowe aheshimiwe
Anakazi kubwa Sana kuwapika vijana wake (makamanda ushuzi)

CCM DAMUDAMU!!!,CHAMA CHA MAMA &BABA
 
Kwa lipi? Kwa kutuuza sie wapinzani wa kweli na kubadili gea angani...! Abadan ..hili kosa linahitaji toba ya kweli na malipizi ya dhati..!! Maweeee
 
Kweli ni lazima aheshimiwe kwanza ni mwenyekiti wa maisha hilo si jambo dogo, hata serikali ya awamu ya 5 ilifanya makosa kumtupia vitu vyake nje yeye hastahili kulipa kodi yeye ni mkwepa kodi wa maisha. Hata hayo matumizi mabaya ya fedha za chama ni kosahata kumtaja kwani yeye ni mtumiaji wa pesa za chama wa maisha.
Ni kweli lazima tumueshimu sana Mbowe kwani alibadilisha Gia box angani kama futi 300 kutoka usawa wa bahari bila kuangalia usalama wa watu na chombo chenyewe wakati giabox inabadiliswa ndege ikiwa chini.

Anaitaji kuheshimiwa sana kwani ameleta kitu ambacho hakijawa kuonekana tangia 9 Desemba 1961 hadi alipofika yeye tabia ya kuwafundisha wabunge wake kususa na hata kususia chaguzi na inasemekana uchaguzi wa 2020 amesha andaa utaratibu huo wa kususia uchaguzi hili kuingia barabarani tujiandae.
Ata uteuzi wa viti maarumu pia amekuwa anaitaji heshima kwani ametimiza amli ya Mungu kwenda kuijaza dunia.
Kichwa kibovu kama hiki vimebaki vichache sana mjini, itabidi zifanyike juhudi za makusudi utafutwe popote ulipo tukuweke "karantini" makumbusho ya taifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata alivyobadilisha gia angani amesaidia kuionyesha sisiemu kwamba wanaweza kuchomolewa kukiwa na tume huru ya uchaguzi!
Chukua kura million 6.8 x 5000 kura za mgombea urais pekee(ruzuku)...harafu utajiuliza hata garizao walisambaza halmashauri zote nchini zimetokanaje unaza magufuli kuzuia mikutano ya hadhara mchezo ,tayari chadema walikua na uwezo kufika hadi ngazi ya shina anakojivunia ccm kupata kura wazee kabisa .....magufuli anavosema anatamani kukimbia ikulu sio maskhara na ikosiku ATASEMA.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sidhani kama kuna binadamu mstaarabu asiyeheshimu mwenzake, ila ukiondoa kuheshimiana tunaruhusiwa kutofautiana kimtazamo.
Nikuulize mara moja hii, kwa sababu mstari wako una maana kubwa ambyo pengine hukuiweka maanani.

Kwani kumheshimu binaadam kunatokana na nini?

Au kutomheshimu, kunatokana na nini?

Nadhani Mh. Mbowe sasa amejijengea heshima kwa watu kwa sababu maalum wanazoziona hawa watu kuwa zinamjengea heshima katika uongozi.
Hili ndilo la mhimu kulizingatia.
 
Back
Top Bottom