Freeman Mbowe aanza ziara ya siku 6 Mikoani

Freeman Mbowe aanza ziara ya siku 6 Mikoani

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Mwenyekiti wa Chama Taifa Freeman Mbowe ameanza ziara ya siku 6 mikoani ukiwa ni mwendelezo wa uzinduzi wa programu ya FTP maalum kwa ajili ya mafunzo ya uzalendo kwa vijana ikiwa ni mwendelezo wa shughuli ambayo amekuwa akiifanya tangu Januari.

Leo ataanzia Nzega ambapo atazindua FTP eneo la Ndala kisha atafanya mkutano wa hadhara hapo hapo Ndala.

Kiongozi huyo wa Kambi ya upinzani bungeni kesho atakuwa Itilima-Bariadi, keshokutwa atakuwa Ukerewe, siku inayofuata atakuwa Bukoba Mjini kisha Kyerwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyothibitishwa na msemaji mkuu wa chama Tumaini Makene inasema kote huko Mwenyekiti huyo atafanya uzinduzi wa FTP asubuhi na jioni mikutano ya hadhara katika maeneo husika.

Maeneo yote hayo Jeshi la Polisi limealikwa kutoa elimu ya ulinzit shirikishi na polisi jamii. TAKUKURU nao wamealikwa kutoa elimu ya kupambana na kuzuia rushwa hasa wakati wa uchaguzi. Kuhusu programu ya uzinduzi wa mafunzo ya kukiandaa chama kwenda kushinda dola na kuongoza serikali.

Makamu Mkiti Taifa (B), Prof. Safari atakuwa Korogwe Mjini ambapo atazindua mafunzo hayo kwa viongozi wa Korogwe mjini na Vijijini kisha jioni atakuwa na mkutano wa hadhara Korogwe Mjini.

NKMB Mnyika atazindua mafunzo Bariadi kisha atakuwa na mkutano wa hadhara saa 5/6 hapo Bariadi kisha atakuwa na mkutano mwingine wa hadhara Maswa jioni ya leo.

Kwa upande wa NKMZ Salum Mwalimu yeye atazindua mafunzo mji wa Mbalizi Mbeya kisha atakwenda kufanya mkutano wa hadhara Njombe mjini leo jioni.


Updates...

Standalone akiripoti kutoka Nzega sasa hivi

Mkutano unaendelea hapa Vzur...Bado. Mbowe hajapanda jukwaami....
attachment.php


Alichosema Mwenyekiti Nzega kwa hisani ya Kamanda Standalone

+++Updates++++

IGP Mangu anasema atakaefundisha vijana tunamkama, nasemaMbowe wa kwanza aje anikamate
Vivyo vivyo hivyo wakikuta kijana wa Chadema anaiba kuku wamkamate
Siku ile tunapigwa mabomu Polisi hawakutoa msaada wowote,tukawapa damu kwa kukusanyana watu wa Chadema tukatoa damu kuwasaidia
Chadema tunasema Mutungi sio mlezi wetu, kazi ya siasa atuachiesisi wenyewe
Ukiona Chadema tumeamua kuijenga Red Brigade ujue tumeumia
Mkt anaendelea kusema kuwa yeye amepigwa bomu la kivita Arusha,na bomu lilirushwa na Polisi, wakapiga tena na mashine gun wakafariki wenginekwa niaba yangu
Leo nikizindua mpango huu leo kimefanyika kikao cha vyamavidogo vidogo ambavyo havina diwani, wabunge wala hata bendera

CCM vijana wao wanafundishwa kuiba kura na kushambuliawapinzani. Pamoja na yote vijana wanafundishwa kulinda kura.
Vijana wanafundishwa mchana kweupe sio kwa siri hata polisiwanashiriki, Takukuru na Usalama wa Taifa

Amewaasa vijana kuwa wakimkuta Kijana wa CCM anafanya kosa lajinai wawe wa kwanza kumkamata
Polisi nchi hii hawatoshi- hata hapa Ndala kituo kina polisiwanne tu

Mpango huu wa mafunzo wa FTP 200 unalenga kuwa na vijana200@Kata lwa ajili ya kujengwa kinidhamu na uzalendo pamoja na kupambana nauhalifu kama raia
Mutungi hawezi kuzuia mabadiliko kwa sheria isipokua anaweza kufanyahivyo kwa kuhakikisha haki inatendeka
Mutungi atuachie siasa yetu

Tulisema Bungeni, tukamwambia Rais kuwa waliorisha bomu niPolisi hivyo waunde Mahakama ya Corona. Chadema imekataa kuwapa ushahidi polisikwa sababu wamehusika
++++Updates+++
Kwa sasa tunatekeleza dhana ya Polisi Jamii kwa vitendo
Vijana waliokuwa Kambini wamefundishwa Uzalendo, Afya, Ulinzi Shirikishi, na wamepata semina kutoka kwa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa.

Kikao hicho kilihudhuriwa na mtu anaitwa Mtungi na IGP Mango
Mpango huu umezua hofu kwa sababu vijana hawa wamesambaa nchi nzima
CCM wanafanya kila mbinu kuisambaratisha Chadema, wanatumia Polisi, Msajili wa vyama, wanapiga propaganda za Red Brigade. Lakini hawatuondoi kwenye mstari

Kuhusu uchaguzi Mkuu: Serikali za Mitaa ziligubikwa na vurugu nyingi mpaka kufikia hatua ta kutangaza watu ambao sio washindi. Polisi na Usalama wa Taifa wanajua lakini hawakuchukua hatua yoyote
Mwaka huu ni wa Uchaguzi, nategemea mabadiliko makubwa kutoka Mkoa wa Tabora
Mutungi utafuta vikosi vya ulinzi kisheria lakini hutaondoa ari katika mioyo ya wanachadema
Mpaka sasa nina kesi 11 kwa hiyo IGP ajue siogopi kukamatwa hata kidogo. Kesi zote ni za uchochezi, je Mbowe nafanya kazi ya uchungaji ili nisiizungumze CCM na ufusadi wake?
Mwenyekiti Mbowe alimtaka Mwenyekiyi huyo wa kijiji kuonesha tofauti ya kiuongozi. Watende haki, bila rushwa na wala upendeleo.

Kabla ya Mwenyekiti kuhutubia alikaribishwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Uhemeli Kata ya Ndala anaetokana na Chadema. Kijiji hicho ambapo mkutano unafanyika kinaongozwa na Chadema kwa 98
Walilazimisha kura ya maoni tukawaambia hawawezi leo wameahirisha kura hiyo
CCM wanatamani uchaguzi usiwepo na pia hawataki kuwaandikisha wapiga kura. Ccmmtaogopa mpaka lini kuandikisha wapiga kura???
Tumebakiwa na miezi minne kuanza kampeni za Uchaguzi Mkuu. Kwa kuwa kama sheriaitafutwa tar 15 Aug ni tarehe ya kuanza kampeni
Tume imeshindwa kuandikisha wapiga kura na hakuna anaewajibika

Mwenyekiti Mbowe alimtaka Mwenyekiyi huyo wa kijiji kuonesha tofauti yakiuongozi. Watende haki, bila rushwa na wala upendeleo.
Mwenyekiti kabla ya hotuba yake alizindua mpango wa FTP 200 ambao ni mpango wakuwa na Red Brigade nchi nzima na kwa kila Kata
Kiongozi yeyote wa kisiasa ni lazima achaguliwe na wananchi sio uteuzi

Chadema tunasimamia sera ya Majimbo ambayo inasema kuwa itakua marufuku kwakiongozi wa kisiasa kukamata mamlaka ya kiserikali kama hajachaguliwa nawananchi. Lengo lake ni kuzuia wimbi la uteuzi ambao hautokani na wananchiwakiwemo wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa
Chadema hatuwezi kukubali vyeo vya kuteuliwa leo kama mashindano ya miss Bantu
Tunazungumza uchaguzi mkuu mwaka huu lakini hatujui kama utakuwepo kwa kuwa kwamiezi minne Tume haijamaliza hata Mkoa Mmoja wa Njombe
Suala hilo liliwekwa vizuri na Tume ya Katiba lakini wakachakachua

Tunawasubiri Oktoba, sisi Chadema hatulali na tumesambaa nchi nzima.Kitaeleweka tu
Na hakuna kiongozi anaeweza kumwajibisha yeyote.
Kuna udhaifu na ufisadi mkubwa katika nchi hii na waathirika wakubwa niwananchi. Wizi wa Escrow ni tone kwenye ufisadi ambao unafanyika katika sektambalimbali nchini
Mwenyekiti aliwataka viongozi wa Chadema kuungana na wenzao wa Ukawa kwa kuwa Cufau Nccr sio adui wa Chadema zaidi ya CCM
 
Last edited by a moderator:
Twende kazi.Tulianza na Mungu Tutamaliza na Mungu.Mungu akulinde kamanda


swissme
 
Hapo sasa ndio Utajua uwezi pambana na taasisi....Mwenyekiti Kule, Naibu katibu kule,Naibu mwenyekiti kule.....Yaan nchi nzima Elimu ya Ukombozi......Hatuwezi kwenda pamoja kama wazee wa mbio za mwenge.......

Hii ndio chadema bwana,,,Asante molemo najua uko Jikoni...Utusaidie Updates..
 
Hiyo ndio CHADEMA bana, twanga kote kote.

Maccm yakisikia hizi habari huchanganyikiwa sana
 
Hapo sasa ndio Utajua uwezi pambana na taasisi....Mwenyekiti Kule, Naibu katibu kule,Naibu mwenyekiti kule.....Yaan nchi nzima Elimu ya Ukombozi......Hatuwezi kwenda pamoja kama wazee wa mbio za mwenge.......

Hii ndio chadema bwana,,,Asante molemo najua uko Jikoni...Utusaidie Updates..

sema kajamaa katatuhalibia kura nyingi mkuu.

swissme
 
Zitto anawatoa watu ofisini. Safi sana ACT endeleeni kukaza hivyo hivyo.
 
safi sana mbowe kwenda kyerwa. kule kuna batinoruho na bebedicto mutungirehi. wai kule hadi mwez wa 7 watakuwa wamemaliza kura za maoni na zoez wanalosubili ni kuapisha mbunge. kyerwa naomba utembelee vijiji ccm ilivyoshindwa wakarazmisha matokeo na wana cdm wakafunguliwa mashtaka
 
Back
Top Bottom