Frederick Mpendazoe atimkia CCJ...

Nasikia vikao vya juu ndani ya chama vilishapitisha kuwa jamaa atemwe. Ameamua kuwa-pre-empty
Hata mimi ndivyo nilivyosikia, wacha tusubiri tarehe 08/04/2010 tusikie na upande mwingine wa shilingi na kisha wananchi tuamue.

Kuna wengine pia panga linawakaribia, huenda kesho wakaruka pia.
 
Kutofautiana na CCM ni hatua moja kubwa kwa watz kujiletea maendeleo. Kitendo cha Mpendazoe kutoka CCM katika nafasi yake ni hatua kubwa zaidi katika mchakato wa kuwaletea maendeleo watanzania. Kujiunga CCJ huo ni uamuzi wake nauheshimu.


Naona unakuwa makini sana kumuunga mkono Mhe Mpendazoe.

Maoni yangu ni kuwa tayari tuna vyama vya siasa vingi sana. Kinachotokea hapa ni kuwachanganya Wananchi ambao tayari wanachanganywa vya kutosha na Wanasiasa uchwara wa Upinzani. Mhe Mpendazoe ana maamuzi yake binfasi ambayo hatuna budi kuyaheshimi. I only wish angeenda kuvijenga vyama ambavyo tayari vipo na vimesajiliwa usajili wa kudumu.

But then again is only my wish.
 
Candidate Profile - FRED MPENDAZOE TUNGU
email.gif
E-mail this to a friend
print.gif
Printable version
PIC33662.jpg
First Name: FRED Middle Name: MPENDAZOE Last Name: TUNGU Constituent: KISHAPU Political Party: CCJ
 
hii ni kweli katangaza rasmi anahamia ccj na wengine watamfuata nyie subilini.
ni kweli kahama ccm, ila kiukweli ni njama za ccm kutaka kuua upinzani ndiyo maana wameanzisha chama cha ccj ilikitumike kama kivuli kuua nguvu ya upizani haswa chadema, ndiyo madhumuni ya chama hicho hamnalolote watanzania ccj siyo chama chaukweli bali ni chama kile kile cha ccm, hizo ni mbinu watanzania msidanganyike
 
Hapa ninachoona kwa upand emwingine ni kwamba tumapeta single nyingine ya kutupeleka peleka tusahau kinachoendelea kwenye CC huko!

Media nadhani sasa hivi watacamp kwa Mpendazoe na CCJ ambayo baadhi ya magazeti hasa mwishoni mwa waki walishaanz akuidismiss

Tutegemee conspiracy nyingi zaidi kuihusu CCJ sasa hivi...lakini tukisahau kuwa mambo mengine yanaendelea kichini chini na wala hatutapata muda wa kuyahoji tena
 
Dalili zilionekana pale alipompasha Rais J.K kwa kumfagilia Hosea wa Takukuru kule Mwanza badala ya kumkaripia. Mpendazoe aliandika makala kali sana na kumshutumu Rais kwa kitendo cha kumsifia Hosea. Wengi tulijiuliza kapata wapi ujasiri? Matokeo ndio haya. Tumpe hongera. H e is a man and half!
 
huu ni kati ya uamuzi mmbaya kabisa kuwahi kuona maishani mwangu, habari za yeye kuondoka alianza kuwaambia watu wake wa karibu mwezi fenruary siku chache tu baada ya CCM kuadhimisha miaka 33 ya kuzaliwa kwake. alishajadiliwa mara kadhaa na chama hakikuona tishio lolote la ushindi kama angeamua kutelkeleza mpango yake hiyo. kuna wakati inanfika unaona mwenyewe kuwa huwezi siasa za CCM na mh. mpendazote ndio kaona wakati huo ndio huu. tunamtakia kila la heri. lakini wapinzani wasitarajie lolote la maana kutokana na ujio wake. ccj hawatashiriki uchaguzi huu na chadema hawataweza kuongeza ushindi wao kwa kiasi kikubwa hivyo mwisho wa uamuzi kama huu ni kama ule wa augustine mrema.

kila la heri
Sizitaki mbichi hizi
 
Nimeanza kuwa na wasiwasi kuhusu CCJ, is it becoming kapu la makapi? Is this Fred Mpendazoe aliyetetea mafisadi kwa nguvu zote, au nimesahau? CCJ ni chama ambacho mtu yoyote anaweza kujiunga bila hata kujua msimamo wa mtu huyo ukoje?
Bongolander una uhakika na unayosema Mpendazoe alitetea mafisadi?
 
ni kweli kahama ccm, ila kiukweli ni njama za ccm kutaka kuua upinzani ndiyo maana wameanzisha chama cha ccj ilikitumike kama kivuli kuua nguvu ya upizani haswa chadema, ndiyo madhumuni ya chama hicho hamnalolote watanzania ccj siyo chama chaukweli bali ni chama kile kile cha ccm, hizo ni mbinu watanzania msidanganyike

Sidhani kuna mtu mjinga kiasi hicho yaani ajiunge CCJ kwa kusudio la kuua upinzani kwa manufaa ya CCM - no hapa siafiki kabisa. wewe nafikiri upo nyuma miaka 10 iliyopita, kwa leo hii hili jambo haliwezekani kabisa.
 
Huyu anachemka tu, akawaulize akina Njelu Kasaka, think before you leap!

Kama kweli ana uchungu na nchi au ana hoja dhidi ya CCM angehama mapema angalao labda 2006, sasa huyu anakurupuka jioni hii baada ya kuona uchaguzi umekaribia na pengine ana uhakika hatorudi kwenye kinyang'anyiro cha ubunge! Sheer opportunism! Chama chenyewe cha opportunists, hawana lolote, ni waviziaji tu wenye malengo yaleyale ya kutuachia maumivu.

Kachemsha.
 
Bonge la shoo. Mwaka huu shoo kibao, kombe la dunia nalo limo, CCJ nao wamo, CCM sisi tumo, Mpendazoe naye yumo. Burudani kweli kweli.
 
Kwasasa Mpendazoe anastahili pongezi,rekodi yake inaonyesha ni mtu asiyetaka upuuzi...wengine ni budi wafuate,cha muhimu wasigawane kura na kuipetesha ccm.....Hatutaki kuamini kwamba ni mbinu ya ccm kuudhohofisha upinzani.
 
Bonge la shoo. Mwaka huu shoo kibao, kombe la dunia nalo limo, CCJ nao wamo, CCM sisi tumo, Mpendazoe naye yumo. Burudani kweli kweli.

bado shoo lingine ni kupigana chini kwenye kura za maoni ,,,,hahaaaaa.........ngoja niweke order ya pop corn pale mlimani city for the coming 6 months
 
-Hivi Mpendazoe ktk kuhitimisha mjadala wa Richmond alisimamia upande gani?

-Ni jambo la busara kama amejitoa,kama kajiunga na CCJ pia ni uamuzi wa Busara, na kama wapambanaji walioko CCM watajiunga na CCJ, basi wadhihirishe dhamira yao ya kweli kwa kuunganisha nguvu yao na vyama vya upinzani vyenye nguvu

Ila pia kwa sasa ina mana wananchi wa kishapu hawana mbunge,anyway kuna majimbo mengine yako wazi tangu 2005 hayana wabunge .

Kuna ambao wanasema kafanya uamuzi mbaya just because hajasubiri marupurupu yaani inasikitisha sana tuna watu wa aina hii,yaani mawazo ya watu walio wengi yamejaa unafiki na ubinafsi tu.Nasema kafanya jambo jema ikiwa kweli lengo ni kupigania maslahi ya taifa,angalao atapata muda wa kushirikiana na wenzake kuujenga au kuuandaa upinzani imara mapema kabla ya uchaguzi

Mtu kutoka CCM si uhaini,subiri uone jinsi watakavyompaka aonekane kama vile kafanya uhaini.Mpendazoe umeonyesha Moyo wa ujasiri,hii ndiyo aina ya siasa ninayoitaka,lakini bado swali langu nauliza,ktk hitimisho la RICHMOND alisimamia upande gani?
 
Unatenganisha vipi nia na kuwa mwanachama? Mwache Fred aonyeshe njia. Nadhani ile dharura ya vikao vya CC na NEC ya CCM ilitokana na hili pia.

Tunataka majasiri kama hawa. Sio unanang'ania usipoamini kwa sababu ya vijisent vya pension. Siasa ni zaidi ya fedha, wanaoipinga CCM wakiwa humo humo ndani ni waoga wa maslahi binafsi, sio wanasiasa.
 
Jamani, tusimlaumu Marehemu Mwl, Nyerere kwa kumuachia Mkapa madaraka. Kwa wakati ule, Mkapa kweli alikuwa clean lakini ujinga wote wa wizi aliufanya baada ya Nyerere kufariki dunia. Ujinga wote alioufanya Mkapa akiwa madarakani aliufanya katika kipindi chake cha pili cha oungozi, wakati huo Nyerere hatukuwa naye tena!!!

Tiba

Pamoja mkubwa. Mkapa wa kipindi cha Nyerere siyo yule wa miaka mitano ya mwisho. Hata hii sisiemu ilikuwa imekwishaanza kufanya ujinga ndiyo maana Mwalimu aliamua kutundika madaruga (Kurudi Butiama) Tunahitaji mabadiliko, whether Fred atakuwa mamluki (Of which sidhani ni sahihi kutokana na msimamo wake kwa kipindi nilichosikia hoja zake) or atakuwa na dhamira ya kweli, kile kitendo cha kunyoosha kidole na kusema no, enough is enough inatosha kuonyesha njia kwa watu wenye dhamira ya kweli. Mambo ya Chama chajenga nchi yametufikisha pabaya sana. Nchi inajengwa na sisi wenyewe Watanzania na inatafunwa na chama..By the way naona correlation kati ya fund rising ya uchaguzi huu 40 Billion na ile iliyokwapuliwa BOT kipindi kile kwa kutumia kampuni ya kastuli ambayo hadi leo haiguswi. Hapa chama kilijenga nini na hiyo 40 Billion zaidi ya kubomoa nchi?Bravo Fred.
 
Back
Top Bottom