Frederick Mpendazoe atimkia CCJ...

WildCard

JF-Expert Member
Apr 22, 2008
7,506
2,409
Kuna taarifa kuwa Mbunge huyu machachari amekuwa kigogo wa kwanza kabisa toka CCM kwenda CCJ.

Mpendazoe+031.jpg

Mbunge wa Jimbo la Kishapu (CCM) Fred Mpendazoe (katikati) akitangaza kwa waandishi wa habari jana jijini Dar leo ju ya nia yake ya kuondoka Chama cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chama cha Jamii(CCJ) . Kulia ni Afisa Habari Mwandamizi wa Idara ya Habari Mwirabi Sise na kushoto ni Katibu Muenezi wa CCJ Dickson Nghilily.

Mpendazoe+037.jpg

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kishapu (CCM) Fred Mpendazoe akiwapungia mkono waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam mara baada ya kutangaza nia yake ya kuondoka CCM na kujiunga na Chama cha Jamii(CCJ) leo. Picha na Tinganya Vicent - MAELEZO​
 
Breaking News za Radio One zinahanikiza kwa sasa kuwa Mbunge huyu wa chama cha mapinduzi katika jimbo la Kishapu huko Shinyanga ametimkia CCJ... JOB TRUE TRUE...
 
Hata mie nimeiona kwa Michuzi leo hii, wenye habari kamili hebu tupeni yaliyojiri.
 
Kama ni kweli, basi wapo wengi vigogo wa CCM wenye hisa huko CCJ. Na huyu ameanza tu. Ila siamini kama kweli ameamua kuukacha ubunge, na kukimbilia CCJ. Sidhani kama ameamua kwa dhati akose haya marupurupu ya miezi hii michache iliyobaki. Kwanini asingehama baada ya bunge kuvunjwa?
 
Hii ni kweli katangaza rasmi anahamia CCJ na wengine watamfuata nyie subilini.
 
Breaking News za Radio One zinahanikiza kwa sasa kuwa Mbunge huyu wa chama cha mapinduzi katika jimbo la Kishapu huko Kigoma ametimkia CCJ... job true true...

Mwache aende zake - ameshakuwa "liability" na angebakia CCM "tungempiga chini" katika kura za MAONI!

OFF Topic: TuskerBariiiidi? Siku hizi sikuoni mitaa yetu ya Meeda na B-Bar! Au kwa sababu Tusker imekuwa adimu?
 
Kama ni kweli, basi wapo wengi vigogo wa CCM wenye hisa huko CCJ. Na huyu ameanza tu. Ila siamini kama kweli ameamua kuukacha ubunge, na kukimbilia CCJ. Sidhani kama ameamua kwa dhati akose haya marupurupu ya miezi hii michache iliyobaki. Kwanini asingehama baada ya bunge kuvunjwa?
Maslahi ya Ubunge anayo tu. UTAIFA KWANZA. Tunawasubiri akina Sitta, Ole Sendeka, Selelii..........
 
Kama ni kweli, basi wapo wengi vigogo wa CCM wenye hisa huko CCJ. Na huyu ameanza tu. Ila siamini kama kweli ameamua kuukacha ubunge, na kukimbilia CCJ. Sidhani kama ameamua kwa dhati akose haya marupurupu ya miezi hii michache iliyobaki. Kwanini asingehama baada ya bunge kuvunjwa?
Marupurupu yake atayapata tuu maana nadhani katangaza nia yake ya kujiunga CCJ hivyo haki yake ya ubunge bado anayo.
 
Kama ni kweli, basi wapo wengi vigogo wa CCM wenye hisa huko CCJ. Na huyu ameanza tu. Ila siamini kama kweli ameamua kuukacha ubunge, na kukimbilia CCJ. Sidhani kama ameamua kwa dhati akose haya marupurupu ya miezi hii michache iliyobaki. Kwanini asingehama baada ya bunge kuvunjwa?

Ndugu, sio kila mtu anahusudu vijisenti. Kwa wengine, hata kama ni wachache, uhuru, utu na utashi ni muhimu zaidi kuliko hayo mamilioni ya pensheni!!
 
Ya kweli haya? Je, Ina maana ubunge wake umekoma kwa kipindi hiki kabla ya bunge halijavunjwa?
 
Tupeni source basi tafadhali...Il hizo habari zitakuwa sio za kweli kwani strategically atakuwa wrong..Akeinda sasa maana yake na Ubunge anauvua..I dont think so kama anaweza kufanya hivyo kwa sasa..
 
Ila kwa mtizamo wangu, CCJ nina mashaka kama ni chama imara cha upinzani halisi. Upinzani wa kweli ni lazima utokane na mpasuko ndani ya Chama cha Mapinduzi tu. Yaani ni sawa na kuchora mstari, kundi moja la SSM kule na la pili kule!!
 
Nasikia ilikuwa atimuliwe kwenye kikao cha NEC, kapata habari kaamua aruke kwanza ili awe japo na kisingizio.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom