Fred Lowassa: Baba hakuwahi kumsaliti rafiki yake

Country first,urafiki baadae,na ndiyo uzalendo wenyewe
Kikwete anastahili pongezi kwa kuwa na uwezo wa mpaka kukata jina la rafiki yake kwa maslahi mapana ya nchi.
pole Mzee. Ukweli ni kuwa hakuna uzalendo hapa ila ilikuwa njia ya kujiponyesha. Neema ya Mungu, Mzee Magu akaewatia moto mpaka mkaamua kumdanjisha.
 
Fred Lowassa akihojiwa na Millard baada msiba wa Lowassa ameongea mambo kadhaa kuhusu baba yake. Moja ya swali aliloulizwa ni kipi hawezi kusahau kutoka kwa baba yake.

Fred amesema kitu kikubwa alichokuwa nacho mzee wake ni 'Loyalty' akiita kama 'kufa na mtu wako' kwani katika historia yake ya uongozi yote hajawahi kumsaliti rafiki hata mmoja na ndio kilichomjengea heshima mzee Lowassa na amewafia rafiki zake wote kwenye siasa.

======

Swali(Mwandishi Paschal): Kipi ambacho hutasahau kutoka kwa Baba?

Fred Lowassa: Niseme Loyalty, yaani ni mtu ambaye mimi amenifundisha kiswahili wanaita 'kufa na mtu wako'. Yaani akisema Paschal ni rafiki yangu hata aje nani kumwambia nini, anasema hapana, mimi Paschal namuamini ni rafiki yangu na angekaa nae mpaka mwisho na ndio jambo limemjengea heshma na upendo kwa watu wengi sana kwasababu yeye hakuwahi kumsaliti rafiki yake hata mmoja katika historia yake ya uongozi yote, ni mtu ambae amewafia rafiki wote mwanzo mpaka mwisho.

Hilo ni jambo kubwa na la kipekee sana ambalo kwakweli kwa wanasiasa ni wachache sana wenye kipawa hicho. Amewafia watu wake wote vizuri sana, nadhani hilo jambo mimi nimejifunza, namshukuru Mungu sana.
1708239925686.jpg
 
Hili jibu la Fred limekuja kupigilia msumari wa mwisho kwa nini jina la JK halikutajwa kwenye mazishi ya Lowassa.

Kumbe JK anaonekana msaliti kwenye familia ya Lowassa. Palikuwepo na muda mrefu wa kurekebisha haya mambo, sijajua kwanini yakaachwa mpaka yafike hapa.

Funzo nimelipata hapa, kumbe duniani kuna wakati mnaweza kuishi kama marafiki, lakini mwishowe mkaja kuzikana maadui.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Maadui kiasili ni marafiki waliotofautiana safarini!
 
Country first,urafiki baadae,na ndiyo uzalendo wenyewe
Kikwete anastahili pongezi kwa kuwa na uwezo wa mpaka kukata jina la rafiki yake kwa maslahi mapana ya nchi.
Kipo wapi sasa? Nchi hii hakuna kiongozi mwenye kulitamka hilo neno toka moyoni .
Country first is not for Africa. Roho mbaya na unafiki mkubwa wa siasa za kichawi ndiyo msingi mkuu wa maisha yao.
 
Kwahiyo mbaya wa Lowasa ni nani
(a) magufuli aliyempora ushindi kama inavyodaiwa na kumsweka gerezani mkwe wake, Mume wa Pamela lowassa.
(b) Jk ambaye wanadai alichagiza jina lake lisipelekwe NEC
(C) sitta na mwakyembe waliomwandama bungeni ajiuzuru.

Huyu ana uspesho gani.
Mbona Pinda na malecela walikatwa?
 
Back
Top Bottom