Kulingansha wanamuziki au watu walio katika fani moja ni kitu cha kawaida, lakini lazima kuwe na uwiano wa aina fulani kati ya hao wanao linganishwa. Katika hili kumlinganisha Franco na Madilu kwa kiasi si sawa. Madilu alipotoka Afrisa International baada ya kuachwa safari ya nje na Tabu Ley 1980 alihamia TP OK Jazz ambako aliimba hadi 1983 Franco baada ya Chock Chock Chock session alitoka na kibao Non. Inasemekana Franco alitaka kubadilisha upepo wa waimbaji wake hivyo akamjaribu Madilu na kumkubali na hiyo siyo kama wengi wanavyofikiri ndiyo rekodi iliyomtoa Madilu System na kumsogeza katika kundi la Ntessa Dalienst na Josky Kiambukuta (waimbaji na watunzi mahiri wa TP OK Jazz). Na Franco akawa anatunga nyimbo zinazo endana na uimbaji wake na Madilu. Franco na Lutumba ndio waliomuweka Madilu kwenye kundi la waimbaji mahiri. Madilu baada ya kufariki kwa Franco alisema "anapoingia studio huwa "anamuona Franco" ambaye "humuongoza" kwenye muziki wake. Hivyo hakuna swali la kuwlinganisha kama mhusika mwenyewe anakiri.
Kama ni kumlinganisha Franco nita mlinganisha na Grand Kalle, Tabu Ley, Vicky Longomba, Dr Nico na Le Grand Poete Lutumba Simarro ingawa ukimuuliza Simaro atakuambia Franco ni habari nyingine na amekua bossi wake toka 1961 hadi 1989.