Fossils of the empire: We become what we are!

Fossils of the empire: We become what we are!

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
371,651
Reaction score
860,929
A fossil is sometimes regarded as dead rock but with engraves of dead insects, tiny animals or plants...... That's is our life, we leave footprints to whatever we do... From beginning to the very end...

Building an empire is not something very easy like having intimation with someone you have been hallucinating with. ....

Ngoja niandike kibantu tuu....

Kujenga himaya sio kitu rahisi kama kungonoka na mchepuko uliofukuzia kwa muda mrefu hata kama uko chini ya milki ya mwingine. Himaya zinajengwa kwa misingi taratibu na kanuni. Halafu zinalindwa na kusimamiwa na sheria

Hapa kuna mihimili huundwa ili kuweza kuifanya himaya isimame istawi na kushamiri.... Himaya sio majengo, miundombinu na mipaka tuu... Ustawi wa himaya hustawishwa na wakazi kupitia ile misingi kanuni na taratibu... Halafu sheria anakuwa mlinzi

Maono ya anayekalia kiti cha usukani wa himaya ni muhimu sana kwakuwa maono yake ndio kama nuru na kurunzi la kumulika mbele... Kurunzi la maono ni muhimu sana... Kama likiwa halina mwanga wa kutosha lazima shida itokee mbeleni... Kurunzi hili la maono hupata miongozo toka kwenye misingi kanuni na taratibu za himaya.. Hiyo ndio mikono na miguu yake.. Hiyo ndio glopu na nishati yake...

Hayo yote kwa Pamoja ukichanganya na wakazi wake kwa kufuata misingi na falsafa ya himaya... Ndio ustawi hutokea. Mkalia kiti cha himaya kamwe hawezi kuwageuza wabeba kiti shomoro. Shomoro ni ndege asiye na thamani ukinunua wawili unapewa nyongeza ya mmoja kwa bei ile ile ya wawili.

Tusijenge himaya ya utando wa buibui akishatandika utando wake yeye hukaa kati na kusubiri ayakayenasa... Na akishanasa haraka huzingirwa na kuviringwa utando asiweze kupumua wala kujisogeza tena.. Kisha hufyonzwa damu yote mpaka kifo... Hii haina tofauti na ile biashara ya billion 5.

Tujenge himaya kama chungu.. hana akida wala haendi kwa mjeledi kama punda. Tujenge himaya kama nyuki au siafu. Tutende pamoja. Hatubaguani.. Hatuumizani.. Hatuchukiani. Adui wa mmoja ni adui wa wote. Rafiki wa mmoja ni rafiki wa wote. Akida awepo kama alama ya kurunzi lakini asiwe na buibui na utando wake.

Kama wadudu kama siafu na nyuki wanaweza kujipanga na kutenda kwa shirika. Kutenda kwa umoja.. Kutenda kwa muktadha wa makubaliano sawia nitajishangaa sana kama wanahimaya watalishindwa hili. Yani kuzidiwa akili na maarifa na kiumbe kidogo kabisa!!!!

Mwambie AKIDA atafakari sana....
Fossil ni jiwemwamba mfu halifai kujengea kwenye msingi bali nakshi tu. Lina matobo na mipasuko mingi. Tusijenge himaya ya jiwemwamba mfu. Itakapokuja tufani. Tutashindwa kuhimili.. Tusiwe na himaya na mbweha wala fisi. Kanuni ya survival of the fittest....

Hatujachelewa bado tunaweza kuamua kusitisha chaguzi zote za marudio kwa faida yetu sote.. Pesa ambayo tungepoteza huko tuipeleke kwenye huduma muhimu za jamii kama elimu tiba lishe afya na miundombinu
 
IMG-20180125-WA0110.jpg
 
Kaka inabidi hili andiko uliandike katika vitabu vyako vya kumbukumbuku ili kizazi na kizazi kije kulisoma kuna haya kubwa ya kujenga himaya iliyobora na yenye nguvu katika jamii iliyogizani na watu walifungwa macho kuona mwanga wa mahala walipo...
 
Kitu ambacho sijaelewa kutoka kwako ni kuwa tukisitisha uchaguzi hayo majimbo yabaki bila wabunge au??
mshana jr
 
Kitu ambacho sijaelewa kutoka kwako ni kuwa tukisitisha uchaguzi hayo majimbo yabaki bila wabunge au??
mshana jr
Tunaweza kuingia kwenye mjadala wa maridhiano kwakuwa mwisho wa siku ni kuponya majeraha na kutengeneza sio kuharibu wala kubomoa
 
Kaka inabidi hili andiko uliandike katika vitabu vyako vya kumbukumbuku ili kizazi na kizazi kije kulisoma kuna haya kubwa ya kujenga himaya iliyobora na yenye nguvu katika jamii iliyogizani na watu walifungwa macho kuona mwanga wa mahala walipo...
[emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji120]
 
mshana jr Bila katiba ya Warioba tutaendelea kujenga himaya kwa jiwe la fossil. Sitaki kuamini eti Yale mabilioni ya mchakato wa katiba mpya ndio yameyeyuka Na hamna anayeumizwa kwa hayo matumizi mabaya ya fedha za umma
spidersInTheWoods.jpg
811.jpg
tutafakari kwa Pamoja dhima ya buibui... Jeshi la mtu mmoja na utando wake... Na mchwa kama shirika... Tufani ikija majibu yatapatikana
 
Naona umeamua kupunguza nguvu kwenye thread za uganga na uchawi na kuzihamishia kwenye siasa kuokoa jahazi.

Kweli awamu ya tano imewashika pabaya.
 
Naona umeamua kupunguza nguvu kwenye thread za uganga na uchawi na kuzihamishia kwenye siasa kuokoa jahazi.

Kweli Magu amewashika pabaya.
Mbweha na fisi tabia zao zinashabihiana... Ni tofauti kabisa na chui na Simba japo wana nguvu kuliko hao moroni... Chui na Simba hawali mpaka wahakikishe wameua na hula kwa staha kidogo sometimes wameketi kama FAMILIA moja... Hii ni dhana ya kujali na mmoja
Mbweha na fisi ni viumbe wasio na tafakuri wakiwa wamejawa na ubinafsi na choyo... Watashirikiana kwenye kukamata tuu.. Lakini kwenye kula utashuhudia zahama kubwa.. Ni walafi na watagombana hata kama watakula na kusaza... Kuna wakati hula kitu ambacho bado kiko hai na pia wakikosa chakula hukulana wenyewe kwa wenyewe
 
Swali la kesho,hivi ukisikia "green book" humo ndani tutegemee kukuta vitu vinavyohusu mambo gani?
 
Naona umeamua kupunguza nguvu kwenye thread za uganga na uchawi na kuzihamishia kwenye siasa kuokoa jahazi.

Kweli awamu ya tano imewashika pabaya.
Na wewe unatuhamisha kwenye utamu wa hoja na kututajia majina ya watu wasioonekana kwenye hoja! Aliyekuambia Magu kamshika vibaya mwambie aende akaripoti polisi ili ashtakiwe kwa kosa la kumshika pabaya!
Mshana jr tufikirishe tuimalize weekend angalau kwani hiyo kesho ni bluu monday na ina hangover za kila aina yaani tunaomba nauli kwa wake zetu ilihali hatujui tutaishije kazini!
Nisaidie na hili la ni kwanini jumatatu ni siku ngumu mno kwa wafanyakazi? Au hali hii hunikuta mimi tu?
 
Ila kwa kweli sidhani kama ni sahihi Hata
Kidogo.

Watu wanataabika mapato yanafyujwa.

Sijaipenda hii, lazima wabadilike wasikariri
Sio poa hata kidogo

Wanashindwa hata uteuzi wa Mda..!
 
Mshana...,

Huenda kuna wengi wenye akili wanao ona mambo haya jinsi yasivyo mema kwetu sote.., ila kwa kua wanafaidi fedha za kodi za malofa sie ...., basi wanafikiri watasema kesho wakishamaliza kula ..

Liko genge hili ... [emoji196] [emoji216] [emoji217] [emoji218] [emoji246] [emoji426] [emoji147] [emoji61] [emoji379] [emoji378] linafikiri Tanzania ni kama koloni lao...! Wao ndio wenye Hati miliki ya kufanya chochote hata kiwe ni cha kuleta hasara kubwa kwa nchi.., " they don't give a damn " ... Wao wana [emoji379] [emoji378] [emoji61] . . , kwa hiyo lazima washinde hata kama watanzania hawatajitokeza kupiga kura...

Mungu yupo lakini... ! [emoji34]
 
Ila kwa kweli sidhani kama ni sahihi Hata
Kidogo.

Watu wanataabika mapato yanafyujwa.

Sijaipenda hii, lazima wabadilike wasikariri
Sio poa hata kidogo

Wanashindwa hata uteuzi wa Mda..!

Mwanzoni Nyalandu alipotoka CCM na kuhamia CHADEMA na kabla ya kususia uchaguzi hamkusema haya

Nongwa ni pale tu CCM inapo gain si ndio?
 
Na wewe unatuhamisha kwenye utamu wa hoja na kututajia majina ya watu wasioonekana kwenye hoja! Aliyekuambia Magu kamshika vibaya mwambie aende akaripoti polisi ili ashtakiwe kwa kosa la kumshika pabaya!
Mshana jr tufikirishe tuimalize weekend angalau kwani hiyo kesho ni bluu monday na ina hangover za kila aina yaani tunaomba nauli kwa wake zetu ilihali hatujui tutaishije kazini!
Nisaidie na hili la ni kwanini jumatatu ni siku ngumu mno kwa wafanyakazi? Au hali hii hunikuta mimi tu?
[emoji3] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji123] [emoji109] [emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji120]
 
Back
Top Bottom