Forex : Mirejesho imepungua mno kulikoni?

Bado sijaenda kwa ontario training lakini nimesoma kwa miezi mi4 na demo juu. Na nimeingia live, forex is real faida ipo na hasara ipo... Kuna siku naweza ingiza hata usd100 na kuna siku naweza kupata loss pia, na ndo changamoto zenyewe sasa sijajua unataka mirejesho ya nini watu wanapambana ndo mana hawapost..
Na sioni ulazima wa kupost anaeamini aamini na asieamini pia ni vizuri.
 
hii pair itatoa pesa mingi wiki hii.endelea ku hold mkuu,imeanza toa hela leo
22d287e7de8bb60093b71aa1552ea950.jpg
 
Forex ndonini wadau? Naonaga tu humu forex forex sikuwahi kufatilia. Mwenye uelewa kidogo anijuze
 
nijuavyo mimi forex ndio biashara pekee duniani unaweza kufanya pasipo kumdhurumu mtu ,pili ni biashara inayohitaji akili,umakini na uvumilivu wa hali ya juu la sivyo loss ni kugusa lazima uwe zaidi ya risk taker.

tatizo nililoliona kwa watu wengi na litawafelisha wengi ni kuchukulia forex kama kazi rahisi ya kufanya kama part time kitu ambacho sio kweli.forex ni zaidi ya kazi maana kuna uchambuzi wa taarifa za kiuchumi na kisiasa za kidunia lazima uzifatilie kwa kila wakati na ikibidi kila baada ya saa moja.
 
''Watu tunanunua magari na majumba kupitia forex, we unauliza maswali ya mirejeshe, we zubaa watu tunapiga pesa we umelala naona uende ukafuge kuku na mbuzi tu''. ALISIKIKA MDAU MMOJA WA FOREX AKIMJIBU JAMAA FULANI KWENYE NYUZI FULANI.

Tukutane kwa Wazee wenzangu wa kuweka mzigo, jukwaa la michezo, mambo ya forex na mimi nangoja mrejesho.
hahahaha
 
Hiki kitu mi roho yangu inagomaga asee sijui kwanini!?

Mi navyopenda hela but kwa Forex imegoma! Sitaki hela through forex
 
Forex is really guys,and money is being made...huo ndo ukweli
Forex ni kweli ipo real ila inahitaji akili kubwa sana..understanding ya hali ya juu kinachotokea duniani..soros kasemaje leo..trump yupo Vietnam kazungumzia nn litakaloleta effets ya $ against other currencies!lazima uumize kichwa na on top of that economics iwe ipo kichwani..ni very complex play..sio ya kitoto..umegusa st kayumba halafu uingie kichwakichwa utaungua!
 
Wacha na mimi niseme kidogo
Mimi ni mwanafunzi ktk hii bishara nina siku 15 tu leo toka nianze nimeianza kwa uoga sana sana lakini mpaka leo tarehe 15 asubuhi saa 1 nimesharudisha zaidi ya asilimia 80 ya pesa nilio anza nayo kama mtaji.natumaini mpaka mwezi uishe nitakuwa nimepata faida zaidi ya asilimia 100.naendelea kujifunza kwa makini huku nikiifanya hii biashara.na kwa jinsi ninavyoiona inaweza kuwa main business yangu.sasa wanaofikiri ni ya kizushi haya sisi tunaendelea.
 
Salaam Wadau,

Nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa mada mbalimbali zinazokuja humu JF hasa za biashara na uwekezaji na nyingine nimechukua hatua moja mbele na kwenda kuzitekeleza...matunda si haba,ukiwekeza muda,nguvu na mtaji kiasi ikiambatana na maombi ahh faida utaiona.

Hapa karibuni pametokea uwekezaji mpya wa FOREX ambao umejizolea mashabiki,watafiti na wanachama wengi sana hadi kupelekea ile thread ya Ontario kutapika jinsi replies zilivyokuwa nyingi.Chochote kizuri huja na maswali mengi hasa kama ni kipya kwenye soko la watumiaji.Mimi kama mfuatiliaji mzuri ningependa kujikita zaidi kwenye mirejesho iliyokuwa inakuja kwa wingi sana hapo mwanzoni na yote ikiwa ni yenye habari chanya na zikihubiri mafanikio na hata zikashawishi wengine kufikiria kuacha kazi zao na kujikita zaidi kwenye hii biashara mpya.

Napenda kuwauliza wale waliokuwa wanaleta mirejesho mbona hapa karibuni imekuwa michache na ni baada ya muda mrefu ??? Au ile nadharia ya kwamba hakuna mshindi wa siku zote na biashara yenye boom wakati wowote imeanza kupata uhalisia ??


Chonde chonde msinipovushe...900 tu inapendezaaa :):)

Featured-Image-785x442.jpg
we subiri habari mpaka unakufa.mda wakuja kukupa fursa unapewa siku moja kwani unataka matangazo ya kila siku.
we kaa hapo hapo unataka marejesho
uzuri muafrika akiona fursa huwa hataki ujue,kwa kuwa utataka kujua zaidi kuliko yeye
 
Back
Top Bottom