For those who fall in love with someone here

Mapenzi yaanziayo humu kizungumkuti mtupu!

Mmekutana kwa majina feki ndani ya msitu msitegemee la maana sana, japo kuna mapekee ya hapa na pale.

We waweza kudhani huyo uliyempata ndo wako pekee kumbe huko kwenye maPM ni wa wengi.

Waweza dhani (unajua) kuwa ana anatumia jina moja kumbe wapi, hola!

Ana mijina lukuki na kila jina lina bebi na la'aziz wake.

Sisemi hakuna wakweli lakini kujua kama ni wakweli ndo kazi.
 

Ni kweli kabisa

Kama unaingia kwenye mahusiano ni bora ukawa makini ili kuepuka matatizo yasiyohitajika

Ukijidai wewe ni wa kumuamini kila mmoja itakuja kula kwako

Hii mambo ya ID kibao nayo ni tatizo lingine!
 
Nimejikuta nacheka sana
Asante sana mkuu kwa kunifurahisha jioni hii!

Ha,ha mkuu mbona wanaokosea namba huwa tunajilipua? Nikibahatika itakuwa Furaha kwangu ila nikipatikana atajisifu sana, loh! Liwalo na liwe!
 
Ha,ha mkuu mbona wanaokosea namba huwa tunajilipua? Nikibahatika itakuwa Furaha kwangu ila nikipatikana atajisifu sana, loh! Liwalo na liwe!

Kwahiyo una ka mpango ka kujilipua?
 
Ni kweli kabisa

Kama unaingia kwenye mahusiano ni bora ukawa makini ili kuepuka matatizo yasiyohitajika

Ukijidai wewe ni wa kumuamini kila mmoja itakuja kula kwako

Hii mambo ya ID kibao nayo ni tatizo lingine!

Halafu sasa watu kwa kujifanya wajuaji huko kwenye maPM.

Jitu halikujui lakini linajifanya linakujua utadhani lilikuzaa.

Sasa likifuma mjinga mjinga ndo kabisaa...litamjaza ujinga weee na yeye ataumeza tu kama peremende.

Anyway, ni heri mijitu ijifanye inakujua ilhali haikujui kuliko kukujua kidogo na kupata chanzo cha uzabinazabina na uhasidi.
 

point... seen.. saved!

its the matter of sinking in and come out with a thought of importance..
 

Mkuu umenichekesha sana

Hiyo "mijitu" isamehe bure tu

Mtu amekujulia hapa lakini utadhani aliwahi kukulipia hela ya dawati shule ...lol!!

Huko kukujua kidogo nako ni tatizo

Mtu alioneshwa tu barabarani yule ndie Ngabu

Anakuja hapa na kuanza "kukuchana"

Kumbe Ngabu mwenyewe ni mweusi hivyo ..lol!!!!

Kumbe aliyemuonesha alikosea yule sio Ngabu ni Eiyer ...lol!!

Hii "mijitu" hii ...lol!!!!!!!!!!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…