Sioni tatizo la pesa cha msingi ni kama Everton wanawauza hao wachezaji,kama wanauzwa ManU wanaweza peleka ofa nyingine kubwa zaidi ya hiyo (Kama walivyofanya kwa Cesc),hata Chelsea walipeleka ofa ManU kwa ajili ya Rooney ilikuwa ndogo na still wanataka kupeleka ofa kubwa zaidi
Nafikiri Moyes angeachana na Baines ambaye ana miaka 28,naamini still Evra anaweza cheza kiwango cha juu kwa misimu miwili zaidi kuna dogo yuko Southampton anaitwa Luke Shaw wangemwahi mapema kabla hajapanda bei.Fellaini huyu ndio anafaa Manu wana tatizo la kiungo kama yeye kumbuka Fletcher huend hasirudi tena
Tujikite kwenye context ya hili saga, Man Utd hawana tatizo la pesa na hakuna aliyesema hivyo ila offer waliyoweka mezani was "derisory and insulting"
Moyes anamtaka Baines kwa sababu ya chance anazocreate akipanda mbele, kumbuka kuwa msimu uliopita, Baines alitengeneza chances nyingi kuliko mchezaji yoyote yule Ulaya, bahati mbaya striker ya Everton ilikua butu. So nadhani Moyes anafikiria hizo chance zikikutana na RVP au Rooney zitatengeneza magoal mangapi?
Mkuu age is nothing, kwangu mimi nadhani Baines yuko kwenye pick, ashakomaa kisoka na kiakili na ana uzoefu wa kutosha na EPL na huwezi jua anaweza kucheza at top level mpaka umri wa kina Lampard (35) coz it's hardly kumsikia na majeruhi, ni injury free sort of player + anamjua na anaujua ufundishaji wa Moyes vizuuri
Huyo Luke Shaw ni mzuri lakini ndio kwanza anakuza soccer lake, bado ana mengi ya kujifunza na ana msimu mmoja tu kwenye EPL, labla kama unamnunua huyo kama back up ya Baines au Evra.
Mimi nadhani kumfukuzia Fellaini ni matokeo ya kumkosa kiungo mliyekua mnamtaka sana, a midfield general, kama hao wacatalunya wawili mliowakosa.
Ideal midfield anayehitajika Man Utd ni Modric baada ya kuwakosa hao wacatalunya, Fellaini ni mtibuaji flan hivi na mtu wa mabavu mabavu, sio mpiga pass mzuri na hana uwezo mkubwa kwenye transition, ku-link vizuri kati ya beki na washambuliaji, me sioni tofauti yake na Jones wakicheza kwenye kiongo ya chini though Fellaini ni mzuri kwenye kufunga ila hana qualities kama za Carrick kama kiungo.
Mkimpata Modric akacheza na Carrick kwenye midfield na play maker mmoja hapo mbele yao mtakua vyema.