Flyover TAZARA Imetengewa Bajeti - Magufuli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Flyover TAZARA Imetengewa Bajeti - Magufuli

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tume ya Katiba, Jul 5, 2012.

 1. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #1
  Jul 5, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Wadau,

  Serikali yetu sikivu, kupitia chama kilichopewa ridhaa ya kuongoza nchi na wananchi weengi, imetangaza bungeni kupitia jemedali MAGUFURI kuwa pesa zimetengwa kwa ajili ya flyover TAZARA.

  Tuiunge mkono serikali ya JK katika kutimiza ahadi.
   
 2. S.Liondo

  S.Liondo JF-Expert Member

  #2
  Jul 5, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 2,154
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  Kwani katika jiji zima la Dar wameona junction ya Tazara tu. Vipi ubungo na junctions nyingine kibao zilizopo Dar na hata kwenye majiji mengine?

  Hizo wamemuachia nani? Nafikiri wamewaachia chadema waje kuzifanya 2015. Na hiyo flyover ni lazima itajengwa chini ya kiwango maana fedha ni lazima ziliwe. Embu angalia Kilwa road jinsi ilivyooza na ni barabara ya juzi tu.

  Ninaiambia serikali kwenda kujifunza kwa wakenya na Waethiopia. Sio kutuletea maendeleo ya "peremende danganya toto"
   
 3. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,638
  Likes Received: 1,427
  Trophy Points: 280
  Ubungo vipi? mbona ubungo ndio pana congestion ya kutisha kuliko Tazara? au tunataka kuonyesha wageni wanaopita hapo toka Airport kwamba nasi tuna FLyover?
   
 4. BASHADA

  BASHADA JF-Expert Member

  #4
  Jul 5, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 487
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kampeni imeanza tayari? Haya bwana 2012,pesa imeshatengwa, 2013, pesa imeshatengwa, 2014 tunatafuta mkandarasi, 2015 ujenzi utaanza muda wowote. Atakayebisha asubiri.
   
 5. Kireka1980

  Kireka1980 JF-Expert Member

  #5
  Jul 5, 2012
  Joined: Mar 18, 2008
  Messages: 304
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  simply kwa sababau wageni wa kitaifa wakija wanapita pugu road
   
 6. paty

  paty JF-Expert Member

  #6
  Jul 5, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,256
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  time alone., time will tell ,am much interest na final product sio theories wala tactics za kufikia malengo , nangoja , nagoja iyo fly over
   
 7. K

  KAPONGO JF-Expert Member

  #7
  Jul 5, 2012
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,374
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Hata waungwana wanaponawa huanza usoni!
   
 8. M

  Mmwaminifu JF-Expert Member

  #8
  Jul 5, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 1,096
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Mkuu, hiyo ndo nchi yetu ilivyo bora katika priorities.
  Unanunua bajaj vijijini (kwenye miundombinu hafifu) ziwe ambulance, halafu mjini (kwenye lami) unaweka landcruiser.
   
 9. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #9
  Jul 5, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapo kwenye Rangi unamaana gani? Miaka 50 ndio wanayakumbuka hayo?
   
 10. Zanta

  Zanta JF-Expert Member

  #10
  Jul 5, 2012
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 2,017
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Watu hamna jema humu khaa! mfanyiwe lipi mpende?
   
 11. controler

  controler JF-Expert Member

  #11
  Jul 5, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 1,537
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Kwani tumefanyiwa nn! Kuambiwa tumeshaambiwa sana! By the way Lile daraja kule Igunga kashalijenga?
   
 12. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #12
  Jul 5, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Hapa ndo Tanzania inapotia kinyaa! Ethiopia nchi isiyo bahari na iliyokumbwa na majanga ya kimaumbile hasa ukame na ya kisiasa (vita na mapinduzi ya kijeshi), kimiundo mbinu iko mbele kuliko Tanzania iliyojaaliwa na kila kitu na bado tunalishwa ahadi tu.
   
 13. Zanta

  Zanta JF-Expert Member

  #13
  Jul 5, 2012
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 2,017
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kwani hapa tunajadili nini?
   
 14. controler

  controler JF-Expert Member

  #14
  Jul 5, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 1,537
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  1. Kwamba Kigoma itakuwa ndo dubai ya Tanzania na watajengewa uwanja wa ndege wa kimataifa
  {Terminal Three hapo dar Imeshakamiliki si unaona ma AirBus yanavyoshuka hapo}

  2. Kwamba Ziwa victoria watanunuliwa meli kubwa mpya
  {Meli Dar/zenji zimeshatosha kwani mkondo wa Numgwi ushasikia tena umelamba meli}?

  3. Kwamba Folen Daslam itakuwa historia
  {Kwani Ipo}?

  4. Kwamba Mgao wa Umeme utakuwa Historia
  {Kwani ushauona Mgao wewe kwenye awamu hii ya Ari na Kasi na Nguvu}?
  .
  .
  .
  .
  .
  .
  na kadha wa kadha
   
 15. Zanta

  Zanta JF-Expert Member

  #15
  Jul 5, 2012
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 2,017
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Bora umejiuliza na kujijibu
   
 16. K

  Kikwebo JF-Expert Member

  #16
  Jul 5, 2012
  Joined: Aug 25, 2006
  Messages: 352
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Naunga mkono, Ubungo ni worse zaidi. Ila nadhani Ubungo kuna kazi kubwa zaidi. Lile gorofa la Tanesco na ile mitambo ya umeme pale.

  Otherwise nadhani Ubungo ndio wangeanza nayo. Ila labda pia wanataka waanze na TAZARA kama majaribio huku wakiangalia performance ya upanuzi wa Moro Road kwa kuweka Bus Lanes kabla hawajaenda kwenye miradi mikubwa zaidi. All in all, a good start na tuombe ifanyike kweli.
   
 17. w

  wakuziba Senior Member

  #17
  Jul 5, 2012
  Joined: Jun 24, 2012
  Messages: 123
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hongera magufuli na erikali kwa yale mnayoyafanya ktk sekta ya barabara! hapa mmecheza karata dume!!!!!!!!!!!!
   
 18. mcfm40

  mcfm40 JF-Expert Member

  #18
  Jul 5, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,142
  Likes Received: 1,779
  Trophy Points: 280
  Fly over tazara bila fly over ubungo haina maana yoyote ni mzaha tupu. Ni sawa na hiyo barar ya mendo kasi inaishia kimara badala ya mbezi. Wakati siku hizi foleni ya kufa mtu inaanzia kimara kwenda mbezi jioni
   
 19. Mzalendo Mkuu

  Mzalendo Mkuu JF-Expert Member

  #19
  Jul 5, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 738
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Ni jambo zuri ingawa ningependa sana kutoa angalizo. MAGUFULI huyuhuyu wakati akiwa waziri wa MKAPA alitangaza hapohapo kwenye Bunge FLYOVER 6 ikiwemo na ya TAZAZA. Miaka 7 baadaye FLYOVER zimerudi tena. Labda this time zitajengwa. Tuombe uzima!
   
 20. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #20
  Jul 5, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Hongera sana Waziri Magufuri ni mpango mzuri wa kuondoa foleni kwenye Jiji letu la Dar es Salaam, naona kazi zinafanyika ukipita barabara ya Morogoro unakutana na Strabag Kampuni kutoka Ujerumani wanatengeneza barabara za mabasi yaendayo kasi.
   
Loading...