Fly Emirates wana trips ngapi kwa Tanzania?

Heijah

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
4,781
7,541
Jamani naomba msaada hivi Emirates airline wamepunguza trip zao kwa wiki imekuwa mara 5 tu badala ya daily flights. Kama kuna kuna mtu anajuwa please anaweza kuthibitisha. Hata Qatar airline walikuwa twice daily naona hivi sasa mara moja. Ila hii ya Emirates kidogo nimeshtuka au ndio hali mbaya inaanza kuonekana kila sehemu.
 
Kuna vitu jifunze kuwaza nje ya box!.
Sawa Emirates wamepunguza safari labda sababu watanzania wanaisoma namba, je hao watanzania pekee ndio walikuwa wanajaza pipa la watu 200+ daily?..
 
Hiyo ya Qatar x2 kwa siku ni trip za wapi?

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Nadhani swali langu ilikuwa je ni kweli kuwa ndege imekuwa mara 5 badala ya 7? hakuna sehemu nimesema wa Tanzania tu walikuwa wanajaza ndege na hata tufanye kuwa wageni walikuwa wanajaza hao wageni wakija ina maana pesa au fursa zilikuwepo sasa ukiwaona watu hawaji kwako ujuwe kuna tatizo. Tunasema tuongeze utalii unadhani kwa njia hii tutaongeza au investors. tatizo ni kubwa hii ni mara ya kwanza inatokea.
 
Hiyo ya Qatar x2 kwa siku ni trip za wapi?

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
Qatar ilikuwa inatua Dar asubuhi na nyingine saa 8 mchana kwa muda mrefu tu kutoka Doha, hii ya Qatar sio tatizo kuwa na moja inatosha ila Emirates nadhani wamepunguza trip 2 kutokana na website yao. unajuwa tumenunua ndege na kusema itasaidia kukuza utalii ila sisi hatuka connections kama za Emirates au Qatar. kuna program ya flights na ukweli ukiangalia ndege nyingi ziko katika anga za nchi zenye uchumi mzuri ukiwa unashuka Africa ni chache ila sasa hata hizo chache zinapunguwa. Ettihad ndio wali cancel kabisa route ya Tanzania.ukitaka kujuwa ndege inakupa dalili kuwa nchi ina uchumi mzuri angalia ndege zinazoenda South Africa zaid ya mara mbili daily.
 
Kuna vitu jifunze kuwaza nje ya box!.
Sawa Emirates wamepunguza safari labda sababu watanzania wanaisoma namba, je hao watanzania pekee ndio walikuwa wanajaza pipa la watu 200+ daily?..
... uchumi wa nchi ukiathirika sio watanzani peke yao wanaoathirika; kuna wageni kwa namna moja au nyingine wanaathrika pia. Ni mchina, mmarekani, mjapani, au mwingereza gani atakuja nchini kuangalia fursa wakati uchumi uko hohehahe? Obviously, mashirika ya ndege lazima yaathirike pia.
 
Qatar ilikuwa inatua Dar asubuhi na nyingine saa 8 mchana kwa muda mrefu tu kutoka Doha, hii ya Qatar sio tatizo kuwa na moja inatosha ila Emirates nadhani wamepunguza trip 2 kutokana na website yao. unajuwa tumenunua ndege na kusema itasaidia kukuza utalii ila sisi hatuka connections kama za Emirates au Qatar. kuna program ya flights na ukweli ukiangalia ndege nyingi ziko katika anga za nchi zenye uchumi mzuri ukiwa unashuka Africa ni chache ila sasa hata hizo chache zinapunguwa. Ettihad ndio wali cancel kabisa route ya Tanzania.ukitaka kujuwa ndege inakupa dalili kuwa nchi ina uchumi mzuri angalia ndege zinazoenda South Africa zaid ya mara mbili daily.
Nimekuelewa vizuri sana mkuu

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
... uchumi wa nchi ukiathirika sio watanzani peke yao wanaoathirika; kuna wageni kwa namna moja au nyingine wanaathrika pia. Ni mchina, mmarekani, mjapani, au mwingereza gani atakuja nchini kuangalia fursa wakati uchumi uko hohehahe? Obviously, mashirika ya ndege lazima yaathirike pia.
1. Iwapo uchumi umeathirika wangetoa kabaisa na kupeleka safari zao Kenya
2. Kupunguza safari za ndege haimaanishi uchumi wa nchi pekee.
3. Mleta mada slitakiwa uliza lakini kamaliza na conclusion.
 
Jamani naomba msaada hivi Emirates airline wamepunguza trip zao kwa wiki imekuwa mara 5 tu badala ya daily flights. Kama kuna kuna mtu anajuwa please anaweza kuthibitisha. Hata Qatar airline walikuwa twice daily naona hivi sasa mara moja. Ila hii ya Emirates kidogo nimeshtuka au ndio hali mbaya inaanza kuonekana kila sehemu.
Kwanini uhisi vyuma kukaza na si hoja nyingine?
Mfano:- Kwasasa kuna ndege 2 ambazo zinapiga rout za Dubai to Dar na sio Emirates tu pekee kama zamani.
Kwasasa kuna Fly Dubai na hiyo Emirates, Je, uhisi uenda sababu ya kuongezeka kwa ndege hiyo nako kumepelekea kumpa changamoto Emirates kupunguza safari zake Jijina Dar es Salaam?
1066819
 
Ndugu yangu mimi sikusema hii ndio sababu moja kwa moja nimesema au labda athari zake zinaonekana sasa. Kusema ndege zote ziende Kenya huko ni kuangamiza nchi haiwezekani kabisa na tukifikia huko basi ujuwe tumeisha. Pia inawezekana tumepandisha gharama za kutumia uwanja sina uhakika ila kwa kuwa tumejenga uwanja mpya na mzuri inatakiwa kuongeza ndege na hii itapunguza gharama za wasafiri. Mimi nimeuliza tu na inawezekana kuna sababu nyingi sijui ila haikutakiwa kwenda kimya kimya. Tufungue Airport yetu mpya ikiwa na ndege nyingi zinatuwa kwetu mambo ya kusafiri mpaka uende Nairobi itakuwa tumerudi 1980's huko.
 
Kwanini uhisi vyuma kukaza na si hoja nyingine?
Mfano:- Kwasasa kuna ndege 2 ambazo zinapiga rout za Dubai to Dar na sio Emirates tu pekee kama zamani.
Kwasasa kuna Fly Dubai na hiyo Emirates, Je, uhisi uenda sababu ya kuongezeka kwa ndege hiyo nako kumepelekea kumpa changamoto Emirates kupunguza safari zake Jijina Dar es Salaam?
View attachment 1066819
Jamani naomba msome vizuri sikusema vyuma vimekaza nimesema au ndio athari zinaanza kuonekana sijaandika sehemu yoyote vyuma vimekaza. najuwa kuwa Fly Dubai inakuja na hii ni budget airline soko lake tofauti kidogo na sijasema ndege haziji nimesema Emirates ndio kama mwamba ukiona na yeye anaanza kupunguza ujuwe sio salama kuna kitu nini mimi sijui inawezekana abiria wachache au kodi zetu kubwa kwa hiyo wanaweka operating cost sawa.
 
Lengo la kuleta uzi wako lililenga kuonesha kuwa hali ya uchumi unasinyaa na uchumi kusinyaa ndiyo vyuma kukaza.
Nimebold humo niwekee tafsiri ya hayo maneno niliyo bold na umeandika mwenyewe
 
zaidi hizi ni ndege za nchi moja na mmiliki ni mmoja Dubai ni wao kujitanua soko tu Fly dubai tu alianza daily sasa kapunguza tatu anakuja mara 4 sasa sielewi ni kama dalili nzuri. kukuwa wa uchumi ni biashara na ndege ina mchango mkubwa sana katika kukuza yote haya.
 
Sio dhambi uchumi kusinyaa kuna tofauti ya vyuma kukaza. uchumi ni wa jumla hata mataifa makubwa yanapitia huko ni kawaida tu lakini vyuma kukaza inaweza kuwa kwangu lakini sio kwako. Kuna viashiria vingi kuonesha uchumi unakuwa ukiona purchasing power ya watu inapungua ujue tatizo. Mfanyakazi vyuma haviwezi kukaza maana kaajiriwa na mshahara atapokea tu hasa wa serikali ina uchumi unaathiri biashara zaidi na uwekezaji sio employees.
 
zaidi hizi ni ndege za nchi moja na mmiliki ni mmoja Dubai ni wao kujitanua soko tu Fly dubai tu alianza daily sasa kapunguza tatu anakuja mara 4 sasa sielewi ni kama dalili nzuri. kukuwa wa uchumi ni biashara na ndege ina mchango mkubwa sana katika kukuza yote haya.

Uenda nikianza kupekea huko nyuma michango yako humu JF usikute nikaja kuona ukimponda John kwa kuifufua ATCL
 
Kabisa huko mimi nilikuwa mtu wa kwanza kumpongeza tena sana na nikasema sio kila kitu kuponda ndege naunga mkono train ndio kabisa. Mimi kitu kizuri nachodhani naunga mkono kabisa penye kukosa kwa maoni yangu nasema. ndege ni kitu kizuri na nilisema leo mtu anaweza kuwa na kazi Mwanza akaenda kumaliza na kurudi hii ni faida mimi sijaponda ndege.
 
Uenda nikianza kupekea huko nyuma michango yako humu JF usikute nikaja kuona ukimponda John kwa kuifufua ATCL
Ndugu yangu Joka kuu, hakuna sehemu nimesema kigezo lazima mji uwe katikati hapana ila kila nchi in sababu zake mimi binafsi sijajuwa sababu zetu inawezekana zipo na zina nguvu ndio maana wameamua. ilikuwa sababu zianishwe halafu kupimwa. kila nchi ina mazingira yake ziko usafiri uko wa haraka na nchi zingine kama majimbo yanakuwa na huduma zote kila jimbo sisi kwetu ilikuwa kila kitu Dar hata ukiwa Mwanza au Songea huko ni lazima uende Dar. kosa ilikuwa kuweka kila kitu pembeni ya nchi ila kama ingekuwa kila mkoa unatoa sawa hapo hakuna shida hata mji mkuu uende Pemba tatizo mfumo wetu wa huduma. Kuhusu ndege sio shida ni kitu kizuri cha maendeleo watalii wakija ndani ndege ni kuwafanya wepesi wa kusafiri ndani ila sikuona sababu ya kununua ndege kubwa kama Airbus ilikuwa tujikite na safari za ndani ni muhimu sana. leo kama mtu ana business meeting Mwanza anenda asubuhi jioni karudi kazi zinafanyika zamani hakuna hizo mtu akifikiria safari ya Mwanza hata kama kuna fursa inabidi aache. ndege ni kitu kizuri na sio ndege tu train na usafiri wetu wa mabus hii itachangia ukuaji wa uchumi ni kama kupunguza foleni mjini inachangia uchumi kazi ya kufanya masaa 3 labda robo saa tu. (huu ulikuwa mchango wangu mwezi March)
 
Jamani naomba msaada hivi Emirates airline wamepunguza trip zao kwa wiki imekuwa mara 5 tu badala ya daily flights. Kama kuna kuna mtu anajuwa please anaweza kuthibitisha. Hata Qatar airline walikuwa twice daily naona hivi sasa mara moja. Ila hii ya Emirates kidogo nimeshtuka au ndio hali mbaya inaanza kuonekana kila sehemu.
unauliza swali au unatuambia? post yako imekaa kinafiki sana...fatilia mwenyewe usituchoshe sisi
 
Jamani naomba msaada hivi Emirates airline wamepunguza trip zao kwa wiki imekuwa mara 5 tu badala ya daily flights. Kama kuna kuna mtu anajuwa please anaweza kuthibitisha. Hata Qatar airline walikuwa twice daily naona hivi sasa mara moja. Ila hii ya Emirates kidogo nimeshtuka au ndio hali mbaya inaanza kuonekana kila sehemu.
angalia hiyo updated taarifa from offical website ya Fly Emirates(screenshot ikionesha monday to sunday)
 
Attachments

  • Screenshot from 2019-04-09 14-56-52.png
    Screenshot from 2019-04-09 14-56-52.png
    10.5 KB · Views: 16
angalia hiyo updated taarifa from offical website ya Fly Emirates(screenshot ikionesha monday to sunday)
Unajuwa sababu ya kuandika niliyoandika kuwa nimetaka kufanya booking Thursday wala Sunday hakuna sasa ingia katika site yao fanya booking siku hizo mbili halafu utaona majibu.
 
Back
Top Bottom