SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 5,150
- 7,916
Mimi ni mmoja wa watu ambao nimeipigania sana Simba huku mitandaoni ila ikafika wakati nikaamua kupumzika maana kuna mambo yanakatisha tamaa sana ndani ya Simba yangu.
Simba ina wachezaji bora sana shida ni jinsi wanavyotumika. Kuna mentality inabidi ibadilishwe pale kuanzia kwa viongozi fulani, hadi baadhi ya wachezaji. Inaonyesha hakuna spirit ya teamwork pale Simba, kila mtu anajiangalia yeye kama yeye kwanza. Kukaa benchi au kuanzia nje, kuna wachezaji wanaona kama watadharaulika. Kuna approach ambayo Yanga wameichukua inawasaidia sana. Kwa mfano upande wa mabeki, wamewachukua wachezaji wanaopendana sana na wengine wanaotoka sehemu moja. Hii inawafanya hali yote ya husda, au kuharibiana kwa njia za ajabu ajabu isiwepo. Na inachowasaidia zaidi, kila mtu anapewa fursa ya kucheza.
Mimi nikimuangalia Chilunda najiuliza huyu anakosa hata mechi moja ya ushindani na kupewa dakika 15, kweli? Hivi Phiri amekuwa mchezaji wa kuingia dakika za nyongeza, kweli? Kuna wakati kisingizio kilikuwa bado hajapona, sasa hivi kisingizio ni nini? Achana na rekodi za zamani alipoingia Simba akawa anaibeba Simba katika mabega yake hadi kuingia makundi, angalia aliporudi baada ya majeraha, hata alipokuwa anapewa vidakika vichache, kuna mechi muhimu sana kwa mfululizo yeye ndiyo alikuwa anatoa assist za magoli muhimu. Angalia sasa, mechi ngapi muhimu ambazo anaingizwa vidakika vya mwisho na bado yeye anakuwa mwokozi wa timu lakini hayo yote hayawashtua hao wanaopanga timu? Nitaingia katika maombi maalumu Phiri aende Yanga na siku tukikutana nao watuchakaze vibaya sana.
Hivi kweli wenye mamlaka ya hii timu wanaitakia mema hii timu? Simba imekuwa na baadhi ya wachezaji walevi, wahuni, wakorofi na walikuwa hawasugui benchi. Hakuna anayeamini Phiri ana sifa zozote mbaya kustahili kusugua benchi. Alishaprove uwezo wake na wote tunaujua. Sasa unamuacha anasugua benchi kwa sababu zisizoeeleweka, eti visingizio kuwa hakabi, eti siyo mrefu, hao wanaopangwa badala yake wanajigonga gonga tu uwanjani, mechi inaanza hadi anatolewa hajapiga pasi hata moja, hayawin hata mpira mmoja wa juu au wa 50/50. Ninavyoamini mimi, kama mechi inahitaji kuongeza mchezaji mkabaji, viungo ndiyo wachezaji sahihi wa kujaza siyo striker tena ambaye siku zake zimeisha kitambo. Mchezaji anapangwa ili tu aotee kagoli kamoja wapate nafasi ya kutunanga tunaokosoa maamuzi yao.
Na nyie mnaotetea ujinga unaoendelea tunajua mnalinda maslahi yenu yanayotokana na ukaribu mlionao na timu na viongozi ila ukweli wote tunauona. Kuna msemo wa kilatini unaosema "Vox populi, vox Dei", yaani "sauti ya watu ni sauti ya Mungu". Wengi tunayasema haya na tunayasema kwa kuwa ndiyo ukweli wa nafsi zetu, nyie mnaongea ukweli wa matumbo yenu. Haya mambo ya kuishia njiani kila msimu ni matokeo ya kujitakia tu. Wiki hii nimeshuhudia wanasimba wengi wanaangalia mechi zake kwa unyonge sana maana wanajua uwezo wa timu na wanaona kabisa inakwama wapi. Wengi wanasononeka na kulalamika kwa sauti ya chini ili wasionekane wanaleta chokochoko au hawataki kuwapa mtaji upande wa pili. Wengine tulishayaona haya yanakuja ndiyo maana tulishaanza kukaa pembeni ili mioyo yetu isiumie. Na tusipojirekebisha na kuacha mapuuza haya group stage safari hii hatuvuki, hatutakuwa tena mwakarobo tutakuwa mwakakundi hadi tutakapojielewa.
Hii naweza kulinganisha na suala la utamu, yaani unataka utamu wa asali, halafu unaenda kuutafuta kwa kitu kichungu. Unataka utamu halafu unaenda kuutafuta kwenye sehemu isiyo safi. Kuna uzi nilileta mwanzoni mwa msimu nikisema Yanga watakuwa na mafanikio bora msimu huu kimataifa kuliko Simba na hizi ndiyo sababu zilizopelekea kusema hayo.
Tukisema haya wanasema tuna chuki binafsi, je hao wanaosugua benchi wakati uwezo wao tunaujua tusemeje?