Mbona Zambia imekuwa inaleta sana chokochoko kwa Tanzania kama Kenya hapo zamani? Kuna nini Nyuma ya Pazia?

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,114
49,840
Wakuu kwa miaka ya hivi karibuni Nchi ya Zambia Imekuwa Inaleta Sana chokochoko na usumbufu kwenye issue ya kufanya biashara na Tanzania.

Mara Wazuie Malori yetu,Mara waseme yamebeba magogonyao,mara Waseme Mizigo Iishie Mpakani Madereva Wao Waendeshe,mara Waseme Uviko 19 nk nk.

Upuuzi huu wanafanya Zambia ndio Kenya walikuwa wanafanya miaka ya nyuma dhidi ya Tanzania, Wakati mwingine Huwa wanakata umeme Kwa kusudi bila taarifa harafu wanakuja kusema eti ooh Kuna matengenezo utadhani umeme wanatupa Msaada ilhali tunanunua.

Hawa Zambia wamekuwa wanahujimu sana Tanzania hasa kwenye mpaka wa Tunduma na tunakoelekea Watatusumbua zaidi maana Sasa wanaelekeza Nguvu kwenye bandari za Angola na Msumbiji..

Wiki kadhaa zilizopita walizua taharuki Kwa kisingizio Cha kusema eti Scanner imeharibika na ukifuatilia ni hujuma,wivu na husda Wala hamna kitu kingine..

Sasa hivi wamezuia mahindi ya wafanyabiashara wa Tanzania waliyonunua huko huko kwao Zambia yasiuzwe Nje ya Nchi..

Watanzania walipewa ruhusa ya kununua na kuuza kokote Sasa wamekamata Malori Wakija na visingizio vya kusema wauze ndani ya Nchi Yao..


My Take
Serikali anzeni kutafuta njia nzuri ya kuifikia DRC bila Kupitia Zambia,Hawa watu Kwa Sasa Wana wivu uliopitiliza na unaotoshia Ustawi wa biashara na Uchumi Wetu..
 
  • Mazungumzo na Tsheked yafabyike ili ili aboreshe usafiri kuelekea Lubumbashi; kisha ile reli ya Mpanda isogezwe mpaka Kasanga;
  • Kuendelea kutegemea njia ya Hichilema ni kujidumaza.
  • Watanzania wapunguze 'janjajanja'; Watanzania ni wapole kama twiga, Zambia ni wapole zaidi ila wako makini kwenye mambo yao.
 
DIPLOMASIA ya kiuchumi.....

Ikiwa ndivyo basi waziri wetu wa mambo ya nje,balozi na wanadiplomasia wanaohusika na nchi za kusini wakae chini kuangalia nini ni tatizo la hayo....wajipange halafu waongee na wenzao wa Zambia.....

Tunategemeana.....rabsha za hapa na pale hazikosekani.....hakuhutajiki mihemko bali UHALISIA na kuangalia maslahi yetu na ya wenzetu.

#SiempreJMT
 
  • Mazungumzo na Tsheked yafabyike ili ili aboreshe usafiri kuelekea Lubumbashi; kisha ile reli ya Mpanda isogezwe mpaka Kasanga;
  • Kuendelea kutegemea njia ya Hichilema ni kujidumaza.
  • Watanzania wapunguze 'janjajanja'; Watanzania ni wapole kama twiga, Zambia ni wapole zaidi ila wako makini kwenye mambo yao.
Kwanza Barabara yenyewe kuanzia Nakonde mpk Isoka ni tabu tu ..
 
Back
Top Bottom