FLOYD MAYWEATHER vs. MARCOS MAIDANA

FLOYD MAYWEATHER vs. MARCOS MAIDANA

Paul S.S

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2009
Posts
6,411
Reaction score
3,280
Haya sasa wale wapenzi wa masumbwi aka ndondi aka boxing leo ndio leo kati ya bondia asiyepigwa hata pambano moja la kulipwa The Money vs Maidana
tutumie uzi huu kupeana updates ya kinachojiri
binafsi sijui kwa saa zetu pambano litaanza saangapi
 
ni chanel gani wanaonesha??? mana pambano la mwisho lilifanyika saa 12 asubuh kwa kibongo bongo ila sikumbuk ilikuwa chanel gani?
 
leo ni leo, kwa sisi hardcore fans wa the sweet science ama Boxing, leo the number 1 pound for pound King, WBC welterweight champ Mayweather Jr. anakutana na WBA welterweight Champion Maidana....ambaye ana KO ratio ya zaidi ya 80%. Katika welterweight unification bout.

*Kumekua na taarifa kua Mayweather anatishia kugomea kupigana leo kama gloves anazotarajiwa kutumia Maidana leo hazitabadilishwa.....anadai ni nyembamba mno na hazina 'padd' hivyo anaogopa 'nako' za Maidana zitampiga directly.

Ila CEO wa Golden Boy kasema kua wadau wasiwe na hofu...mambo yatarekebishwa.

*Purses za leo ama hela wanazopata Mayweather atachukua dola 32 million na Maidana dola milioni 1.5 , hizo tunaita flat , kwa maana kua hizo wanapata kwa kupanda tu ulingoni, ila hela zaidi zitaongezeka kulingana na manunuzi ya Pay per views yatavokua.

*Pamoja na hivo hali itakua mbaya kifedha kwa Maidana ambaye si raia wa America, hivyo iyo 1.5M akishalipia kodi ambayo inakua kubwa kama wewe sio raia inaweza kubaki kama dola 800K ...hapo hajamlipa Manager, Trainer wake/ training camp fees etc.

*Inasikitisha sana take home yake itakua around dola 500K, baada ya kulipia gharama zote izo.

*Kwa wale ambao hawatakua na supersport kutakua na link ya kuwatch live ilo pambano cha msingi uwe na internet nzuri yenye kasi,
 
habari yenu wana jamvi, kwa wale wapenda masumbwi asubuhi ya kuamkia kesho kuna pambano kali la masumbwi
las vegas marekani katika uwanaja wa MGM GRAND ARENA kati ya mmarekani bilionea floyd my weather na marcos maidana kijana wa kiargentina

the+moment+fight.jpg


pambano litaanza saa mojakamili muda wa afrika mashariki pambano la la wbc,wba walter weight championship tite kabla ya pambano lao watatanguliwa na mapambano manne ya mwanzo kati yamir Khan vs Luis Collazo, Adrien Broner vs Carlos Molina, na J'Leon Love vs Marco Antonio Periban.

Maidana+vs+Mayweather.jpg


kabla ya pambano la kesho team ya floyd mayweather walitishia kugomea mechi ya kesho iwapo maidana hawatabadilisha gloves zake atakazozitumia kesho,team ya mayweather imedaikwamba gloves hizo hazina godorola kutosha kwenye eneo la vifundo vya mikono ila habari za kuthibitisha ni
kwamba pambano litafanyika kama lilivyopangwa

4.jpg



record za floyd mayweather mpk sasa ni kwamba amepigana mara 45 na ameshinda mara zote na mara
28 kashinda kwa K.O

floyd-mayweather-jr.jpg



na maidana record yakle ni kwamba amepigana mara 38 kapigwa mara tatu tu na kashinda mara
zote zilizobaki na mara 31 kashinda kwa K.O

images



so far link ambayo nimeipata wataonyesha livestreaming ni hii hapa


Floyd.Mayweather.vs.Marcos.Maidana.Live.stream.watch.online.free.fight by Henry Cavill on Prezi
kwa wenye DSTV waangalie supersport maximo na. 221 wanonyesha,kwa vingamuzi vyengine sijajua channeli gani wanaonyesha


pambano likianza kama kawa mtapata update kutoka round ya kwanza mpk ya mwisho panapouzima,naomba kuwasiisha
 
Mkuu muda itakuwa saa ngapi kwa time ya east africa?
 
Itabidi niamke saa kumi


Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
ngumi zitakuwa ngumu hizi Khan Leo atapigwa alafu ndio anataka kupigana na mtu Kama Floyd!.
 
Itabidi niamke saa kumi


Sent from my iPhone using JamiiForums app

kama hautaki kuangalia mapambano ya utangulizi huna haja ya kuamka saa kumi usiku just saa moja kamili asubuhi inatosha sana
 
hujatuambia exact east african time...
 
the money team is gonna whoop some argentine asses.....poor south american....!!!
 
maidana will have to handle some serious ass whoopin...
 
Back
Top Bottom