Floyd Maywether na Gervonta "Tank" Davis hawaelewani tena

Mokaze

JF-Expert Member
Aug 3, 2018
14,375
14,870
Kwa wapenda masumbwi wote, habari zenu.

Ni habari za kusikitisha kusikia kwamba yule nguli wa masumbwi aliyepata kuwika duniani , pretty boy, money maker Floyd Mayweathear jr the hall of famer amemfurusha kutoka katika (Gym yake TMT Gym) kijana wake aliyemlea katika masumbwi Gervonta "Tank" Davis ili asifanye mazoezi kujiandaa na pambano lake kubwa kati yake na kinara mwingine wa Masumbwi aitwayee Ryan "King" Garcia.

Itakumbukwa kuwa hapo kabla Maywether na Gervonta walihitilafiana na hivyo kutengana, Gervonta akimtuhumu Mayweather "kumuibia" pesa kupitia mapambano ambayo Mayweathear promotion ndio walikuwa wadhamini wa mapambano ya Gervonta, Gervonta akaona isiwe taabu akafukia uadui huo na kuomba atumie Mayweathear Gym kwa ajili ya maandalizi ya pambano hili gumu na lenye hamasa kubwa sana duniani pote, yaani pambano la mabondia hawajapigwa (unbeaten) wote wakiwa katika ubora wao wakipigana katika styles tofauti, kwa kutambua hilo, Mayweathear alimkubalia/alimuacha Davis atumie Gym yake kwa mazoezi na kipindi "dogo" ameingia tu kufanya mazoezi "mwanaume" (Mayweathear) kawaibukia na kuwatoa balu!!😀.

Kwa tukio hilo la Mayweather watu mbalimbali maarufu wametoa maoni tofauti, Wengine wakidai Mayweathear kashikwa na wivu juu ya mafanikio ya Davis na huenda Davis akaivunja rikodi ya Mayweather (50-0) kwani Davis hivi sasa rikodi yake inasimama (28-0-26) ukilinganisha na umri wake hayo ni mafanikio makubwa, Watu wengine wanasema kwakuwa Mayweathear hakuitwa/kukaribishwa kwenye press conference ya kutangaza pambano hilo ndio maana kashikwa na hasira kwani Mayweather ni mpenda ujiko mbele ya camera za waandishi wa habari, Wengine wanadai katika pambano hilo lenye mkwanja mrefu Mayweathear hatopata kitu ndio sababu ya hasira zote hizo, Wengine wanadai ni Gervonta kupuuza ushauri na utaalamu wa Mayweather kumfundisha Gervonta na kumtegemea zaudi kocha wake Calvin Ford ndiyo maana Mayweather kashikwa na donge la inferiority complex ukizingatia yeye bado anachukuliwa na kujichukulia kuwa ni TBE (the best ever), ilmurad kila mtu anayo maoni yake binafsi.

Miongoni mwa mabondia waliosikitishwa na tukio hilo ni Canelo Alvarez ambaye anemuita Mayweathear ni mtu mwenye wivu na amemkaribisha Gervonta kwenye Gym yake kufanya mazoezi, bondia Mwingine aliyesikitishwa na kitendo hicho ni Errol Spence ambaye amesema kitendo hicho hakiendani na umri wa Mayweathear na amemkaribisha Gervonta aende Texas kwenye Gym yake kufanyia mazoezi, kumbuka Mayweather Gym ipo Lasvegas Nevada.

Pambano hilo kati ya hao miamba litafanyika tarehe 22 April, mwaka huu huko Lasvegas T mobile arena, pambano la raundi 12 katika uzito wa lightweight 136 pounds. Dunia itasimama kipindi hicho cha pambano.

Je, ni nani unadhani ataibuka mshindi katika pambano hilo??, ni Tank Davis au ni King Garcia??, maoni yako tafadhali.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom