Alisema kuanzia sasa, hata kama mitambo ya uwanjani ni mizima, patakuwepo bendi za police/jeshi ama mitambo ya tahadhari kwa ajili ya nyimbo za taifa na matangazo mengine muhimu.
Amesema jambo hilo halikustahili kutokea kwa kuwa liliishawahi kutokea wakati wa mchezo na Brazil ambapo safari hii wahusika walipewa jukumu la kuhakikisha kuwa wanazijaribu nyimbo zote siku mbili kabla ya mchezo na kuhakikisha kuwa hakuna hitilafu yoyote na wahusika walimuhakikishia kuwa hakutatokea dosari yoyote.
Amesema TFF imemua kumwajibisha Kaijage kwa kuwa ndiye aliyekuwa amepewa jukumu la kusimamia jambo hilo. Aidha alisema wakati amesimamishwa kaijage ataisaidia timu itakayoundwa kuchunguza jambo hilo na kuongeza kuwa hatua zitachukuliwa kwa yeyote Yule atakayebainika kuhusika kwa tukio hilo.
Kama Chenge na yona na mramba walivyofanya sio?Kwa uzito wa jambo lenyewe Tenga alitakiwa aachie ngazi yeye! Tungemrudisha kwa heshima baadaye!!! lakini kuonyesha alichukizwa yeye ndiye alitakiwa aondoke.
Wadau mimi hili suala la Kaijage kufukuzwa kwa kushindwa kusimamia suala la nyimbo za Taifa (national anthems) siku Tanzania na Egypt walipocheza naona halijakaa vema. Maswali yangu ninayojiuliza ni haya:-
- Kama TFF kupitia Kaijage walimpa mtu kazi, kwa tenda, ili atumbuize siku hiyo, mwenye dhamana ya kutoa tenda ni "Msemaji wa TFF" au mtu mwenye dhamana ya PROCUREMENT? Kwenye tender document si kuna mkataba na unaelekeza nini huyo atakaye tumbuiza afanye siku hiyo na endapo hataweza kuna hatua za kuchukua? (AU TFF KUPITIA KWA BW TENGA WALITOA TENDA KIENYEJI?? Kama sheria ya procurement haikufuatwa basi uwajibikaji ni kwa wengi, si Kaijage pekee....
- Kwa uozo huu uliofanywa mimi naona TENGA na timu yake wote wangejiuzulu kwa dhana ile ya COLLECTIVE RESPONSIBILITY maana ni TFF nzima, si Kaijage pekee aliyechemsha. Kama TENGA anamuona Kaijage hakutimiza wajibu yeye kama msimamizi mkuu wa shughuli za TFF ALICHUKUA HATU AGANI KUHAKUKISHA KUWA TIMU YAKE IMEJIPANG AVEMA NA KUWA KILA KITU KILIKUWA TAYARI (na alipaswa kufika uwanjani kucheki at least hours before)...sasa kama wote walikuwa busy kufuatilia HELA ZA VIINGILIO inakuwaje kumtoa kafara FK pekee??
- Nadhani TENGA na yeye yupo VICARIOUSLY LIABLE