Florian Kaijage apigwa chini TFF

hapo wamemuonea Tenga anajitakasa

Heshima kwako King of King,

Mkuu ungefafanua ingesaidia kujua Tenga kajitakasa vipi ?.Mkuu wadhifa wa rais wa TFF ni sawa na wadhifa wa mwenyekiti wa bodi hawajibiki na shughuli za utendaji za kila siku pengine pengo la katibu mtendaji[mtendaji mkuu] Bwana Mwakalebela linaweza kuchangia itilafu iliyojitokeza.
 
Katika uzembe huu ambao umeliingiza taifa katika aibu kubwa,mheshimiwa tenga unapaswa na wewe ujiuzulu.Kwa kuwa katika huu uzembe na wewe unahusika kwa namna furani!
 
Unaweza kuta vyombo na CD zilijaribiwa na zilikuwa safi, lakini mwendesha mitambo alichefuliwa na ujio wa JK kiwanjani hapo na kugawiwa kwa vipeperushi vya CHAGUA CCM, CHAGUA KIKWETE na ndio maana akaamua kumuhujumu!!


inawezekana mkuu unajua wanaoongoza mitambo yao ni wachina yawezekana wamechukia na ujio wa JK maana nasikia wanaishi kwa hida kweli wengine wameamua kuzaa na majirani pale changonmbe wapate msaada wa kupumzikia...ahasanten kwa kutuongezea wajukuu
 
Mh alienda kujiongezea kura matokeo yake jamaa mhusika kaona howcome akachakachua mambo! teh teh teh teh, binafsi namkubali sana kaijage anapiga kazi sema ndo hivyo Mh huenda kahusika kwa namna moja au nyingine. :A S 112:
 
Ni kweli JK ana gundu. Alitaka kuitumia mechi ya stars na morocco kufanya kampeni matokeo yake ime kula kwake. Kaijage Chadema nini kaiharibu kameeni makusdi ndani ya uwanja. Ha ha ha.
 
Ni uzembe wa hali ya juu kwa wimbo wa Taifa kukosekana wakati unahitajika kwa tukio la umuhimu wa kuwepo kiongozi wa Nchi.
 

Heshima kwako King of King,

Mkuu ungefafanua ingesaidia kujua Tenga kajitakasa vipi ?.Mkuu wadhifa wa rais wa TFF ni sawa na wadhifa wa mwenyekiti wa bodi hawajibiki na shughuli za utendaji za kila siku pengine pengo la katibu mtendaji[mtendaji mkuu] Bwana Mwakalebela linaweza kuchangia itilafu iliyojitokeza.

Game lile lilikuwa la KISIASA ZAIDI UKIINGIA GETINI UNAPEWA KIJANI
 
[QUOTE][/QUOTE]Alisema kuanzia sasa, hata kama mitambo ya uwanjani ni mizima, patakuwepo bendi za police/jeshi ama mitambo ya tahadhari kwa ajili ya nyimbo za taifa na matangazo mengine muhimu.
Nimeipenda hiyo hapo juu
 
nadhan hata tenga hawezi kujitoa kwenye aibu hii, kuna kitu kinaitwa collective responsibility,na yeye anatakiwa ajiuzulu, nadhan ingekua ulaya wote wangekua nje sasa ivi!
 
TFF nawashauri mechi ijayo ya Stars wasimualike tena JK kwa sababu ana gundu, wamualike DK SLAA awe mgeni rasmi, wakiendelea na JK hatutashinda kamwe na CD zitagoma kila mechi.
 
mitambo ilikuwa safi ila ile kuingia jk tu basi!aana gundu huyu
 
Kama tatizo la CD kuimba Uwanja wa Taifa ni Kaijage, mbona toka ile ya Brazil hawakumsimamisha kazi?
 
Kwa uzito wa jambo lenyewe Tenga alitakiwa aachie ngazi yeye! Tungemrudisha kwa heshima baadaye!!! lakini kuonyesha alichukizwa yeye ndiye alitakiwa aondoke.
 
umeona eeeh hata alipokuja na brasil ikakataa kuimba y him??

ndo maana mi nimesema kaijage huna kesi hapo..na tume ya uchunguzi ipitishe kweshenea na miongoni mwa maswali liwepo WIMBO WA TAIFA KUGOMA KILA JK AKIWEPO NI GUNDU AU CD ZINAKUWA ZA KICHINA?sikilizia majibu yake sasa
 
TFF nawashauri mechi ijayo ya Stars wasimualike tena JK kwa sababu ana gundu, wamualike DK SLAA awe mgeni rasmi, wakiendelea na JK hatutashinda kamwe na CD zitagoma kila mechi.

ataalikwa lini tena maana mechi yake kama rais ilikuwa hii...labda wamualike kwenye KINESI cup
 
Ingekuwa kipindi cha utawala wa Mwalimu, Kaijage mbali na kusimamishwa lakini pia angetandikwa mikwaju haradhani kwa uzembe.
 
Hii ni kashfa kubwa sana na aibu kwa taifa hili.
Ilitakiwa waziri na manaibu wake ndio wawe wa kwanza kujiuzulu kwa kuliabisha taifa
 
Back
Top Bottom