Flat Screen: Muongozo kabla hujaenda kununua TV

Kwaio hapa chief inaweza ikawa ukidownload vidio QHD isione vizuri kwenye UHD ? Kama sijakisea..

Yaani swali langu ni kama Nina TV ya led ni pixel gani inahitajika hapo ili nipate angalau picha ya kuridhisha..

Sent using Jamii Forums mobile app
Tv za kawaida za LED mara nyingi ni HD ama full HD,

Hivyo utahitaji content za HD,

Mfano mzuri kama una Azam, weka chanell ya Azam sport HD.
 
Tv za kawaida za LED mara nyingi ni HD ama full HD,

Hivyo utahitaji content za HD,

Mfano mzuri kama una Azam, weka chanell ya Azam sport HD.
Chief-Mkwawa ahsante sana kwa maelezo yako murua.
Mimi nahitaji Flat screen ambayo inatumia aina zote mbili za umeme (ac na dc); lakini pia ambayo power consumption yake haizidi Watts 50.
Nitajuaje kwamba flat screen hii inatumia aina zote za umeme (ac na dc)??-Kuna mtu aliniambia zipo za hivyo.
Natanguliza shukrani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
@Chief Mkwawa ahsante sana kwa maelezo yako murua.
Mimi nahitaji Flat screen ambayo inatumia aina zote mbili za umeme (ac na dc); lakini pia ambayo power consumption yake haizidi Watts 50.
Nitajuaje kwamba flat screen hii inatumia aina zote za umeme (ac na dc)??-Kuna mtu aliniambia zipo za hivyo.
Natanguliza shukrani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tv nyingi za Led za nchi 32 kushuka hazitumii zaidi ya watts 50.

Tv za hivyo zipo ila nyingi naona si nzuri maana hatujafikia Technology hio bila ku sacrifice.
 
So, better kuchukua LED ya nchi 32 kushuka chini ya ac tuu?? Chief-Mkwawa

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio mkuu, na ulaji umeme huandikwa nyuma ya TV mara nyingi. Kunakuwa na kama sticker
22.jpg
 
Asante sana chief hapo sasa sijajua ni chaneli gani mfano zitakazopatikana.
Pia antena ipi inafaa
Iwe antena ya ndani au nje?

Sent using Jamii Forums mobile app
Inategemea ulipo na signal zipo vipi hakuna formular maalumu, wengine wanapata chanell nyingi, wengine moja ama hawapati kabisa, wengine antena popote ilipo inakamata, wengine hadi wasake signal etc.
 
lcd ni kioo chenye mwanga wa taa kwa nyuma, kioo kinakuwa mbele na nyuma mwanga unapiga na kusababisha wewe kuweza kuona.

Led yenyewe mwanga wake si wa taa bali kila pixel inakuww na mwanga wake,

zote LED na LCD zinatumia vioo vya lcd lakini utofauti huo wa mwanga ndio huifanya LED iwe kioo kizuri zaidi.

chukulia mfano dari la chumba chako una namna mbili ya kulieka taa

1. eka taa moja kubwa
2. eka vitaa vidogo vidogo dari zima

taa moja kubwa itakupa mwanga mwingi lakini ukitaka mwanga nusu dari au robo dari huwezi.

vitaa vidogo vidogo havina mwanga mwingi lakini unaweza kuvizima nusu au robo na kuwasha unapotaka.

tuje kwenye tv sasa.

-ukiwa na TV ya LED itaonesha vizuri sana rangi nyeusi sababu sehemu kunapoonyeshwa rangi nyeusi taa inazimwa, ila ukiwa na TV ya LCD nyeusi itaonekana kama kijivu sababu taa moja kubwa inamulika kwa nyuma.

backlighting-comparison-625x1000.png

-pia LED hula umeme kidogo sababu mahala pasipo na mwanga taa haziwashwi

-lcd nayo ina faida sababu inatoa mwanga mwingi kama tv ni ya nje ya nyumba itaonesha vizuri zaidi compare na LED

-pia led inaonesha rangi nyingi zaidi maarufu kama HDR 10, ambazo ni mabilioni ya rangi.
Samahani chief-mkwawa.
Naomba muongozo wa hii kitu,tcl led49s6500sf kama itanifaa kwa matumizi hasa kutazama soka.Ntashukulu sana kiongozi
 
lcd ni kioo chenye mwanga wa taa kwa nyuma, kioo kinakuwa mbele na nyuma mwanga unapiga na kusababisha wewe kuweza kuona.

Led yenyewe mwanga wake si wa taa bali kila pixel inakuww na mwanga wake,

zote LED na LCD zinatumia vioo vya lcd lakini utofauti huo wa mwanga ndio huifanya LED iwe kioo kizuri zaidi.

chukulia mfano dari la chumba chako una namna mbili ya kulieka taa

1. eka taa moja kubwa
2. eka vitaa vidogo vidogo dari zima

taa moja kubwa itakupa mwanga mwingi lakini ukitaka mwanga nusu dari au robo dari huwezi.

vitaa vidogo vidogo havina mwanga mwingi lakini unaweza kuvizima nusu au robo na kuwasha unapotaka.

tuje kwenye tv sasa.

-ukiwa na TV ya LED itaonesha vizuri sana rangi nyeusi sababu sehemu kunapoonyeshwa rangi nyeusi taa inazimwa, ila ukiwa na TV ya LCD nyeusi itaonekana kama kijivu sababu taa moja kubwa inamulika kwa nyuma.

backlighting-comparison-625x1000.png

-pia LED hula umeme kidogo sababu mahala pasipo na mwanga taa haziwashwi

-lcd nayo ina faida sababu inatoa mwanga mwingi kama tv ni ya nje ya nyumba itaonesha vizuri zaidi compare na LED

-pia led inaonesha rangi nyingi zaidi maarufu kama HDR 10, ambazo ni mabilioni ya rangi.

Mkuu samsung yangu siku hizi inawaka kama dakika mbili alaf inajizima....tatizo litakua nini?
 
Back
Top Bottom