Flat Screen: Muongozo kabla hujaenda kununua TV

lcd ni kioo chenye mwanga wa taa kwa nyuma, kioo kinakuwa mbele na nyuma mwanga unapiga na kusababisha wewe kuweza kuona.

Led yenyewe mwanga wake si wa taa bali kila pixel inakuww na mwanga wake,

zote LED na LCD zinatumia vioo vya lcd lakini utofauti huo wa mwanga ndio huifanya LED iwe kioo kizuri zaidi.

chukulia mfano dari la chumba chako una namna mbili ya kulieka taa

1. eka taa moja kubwa
2. eka vitaa vidogo vidogo dari zima

taa moja kubwa itakupa mwanga mwingi lakini ukitaka mwanga nusu dari au robo dari huwezi.

vitaa vidogo vidogo havina mwanga mwingi lakini unaweza kuvizima nusu au robo na kuwasha unapotaka.

tuje kwenye tv sasa.

-ukiwa na TV ya LED itaonesha vizuri sana rangi nyeusi sababu sehemu kunapoonyeshwa rangi nyeusi taa inazimwa, ila ukiwa na TV ya LCD nyeusi itaonekana kama kijivu sababu taa moja kubwa inamulika kwa nyuma.

backlighting-comparison-625x1000.png


-pia LED hula umeme kidogo sababu mahala pasipo na mwanga taa haziwashwi

-lcd nayo ina faida sababu inatoa mwanga mwingi kama tv ni ya nje ya nyumba itaonesha vizuri zaidi compare na LED

-pia led inaonesha rangi nyingi zaidi maarufu kama HDR 10, ambazo ni mabilioni ya rangi.

Mkuu samsung yangu siku hizi inawaka kama dakika mbili alaf inajizima....tatizo litakua nini?
 
Kinachosababisha ubora wa picha ni KIOO au CARD?

Mfano kama inawezekana na wataalamu mtaniambia nichukue CARD ya LG original Niifufunge kwenye STAR X je picha itabadilika? au kioo virse versa?
 
Kinachosababisha ubora wa picha ni KIOO au CARD?

Mfano kama inawezekana na wataalamu mtaniambia nichukue CARD ya LG original Niifufunge kwenye STAR X je picha itabadilika? au kioo virse versa?
mchawi kioo,halafu kadi.

ukichunguza hata kampuni kubwakubwa zinawekeza sana katika tech ya kioo maana ndio kila kitu.
 
Card ndio chipset?
Ndio hiyo mkuu huku mtaani ndio inavyoitwa na mafundi njaa. Wamenishauri niibadili na kusema kuna kadi za kachina zenye picha bomba ila kabla sijafanya hivyo ndio nafatuta ushauri usije ukakuta kinachofanya picha ionekane kuwa ina ukungu ni kitu kingine Zaidi ya hiyo kadi
 
Ndio hiyo mkuu huku mtaani ndio inavyoitwa na mafundi njaa. Wamenishauri niibadili na kusema kuna kadi za kachina zenye picha bomba ila kabla sijafanya hivyo ndio nafatuta ushauri usije ukakuta kinachofanya picha ionekane kuwa ina ukungu ni kitu kingine Zaidi ya hiyo kadi
Inaweza kuongeza ama isiongeze quality mfano kama chipset inayohandle HDR10 na oled display inategemea kioo kiweze ku produce rangi bilioni 1, kama una display ya kawaida haitasaidia,

Ila kuna vitu vyengine kama calibration inaweza saidia na mambo mengine artifical.

Na mafundi wa kibongo sio wa kuwaamini sana, ukiona anang'ang'ania kitu sana ujue sio kwa faida yako ye anaangalia tu faida yake.
 
Unajua unapounganisha tv yako na ama deki au king'amuzi unatumia ule waya wenue vichwa vitatu rangi za njano, nyekundu na nyeupe? Na kama unaunganisha tv na computer unatumia waya wa vga wenye 'meno"? Basi vile vichwa vitatu kimoja hubeba picha na kingine hubeba sauti. Katika ulimwengu huu wa kisasa huhitaji kuchomeka hvo vichwa vitatu bali kichwa kimoja tu cha wire wa HDMI kinabeba mawimbi yote ya picha na sauti na katika ubora zaidi. Kwa kifupi tu HDMI cable ni mbadala wa zile wire tatu zenye rangi za njano, nyekundu na nyeupe.
Asante chief kwa maelezo haya...nami nmejifunza kitu hapa...
 
Back
Top Bottom