First time's an accident. Second time's a coincidence. Third time's a trend! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

First time's an accident. Second time's a coincidence. Third time's a trend!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaFalsafa1, May 21, 2010.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  May 21, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  The heading of this topic is a very interesting phrase and speaks volumes about the attitude of Tanzanians as a whole. We keep making the same mistakes everyday and everyday we give it the same name.....an accident! Road collisions happen daily bu we always call them accidents. Women die in hospitals everyday and we call those deaths accidents. We choose bad leaders and we call them accidents. But what is the side effect of an "accident always" attitude? We don't find the solutions to them. After all who would find a solution to an accident which is supposedly supposed to be a one time thing?

  The point I'm trying to make my fellow JF members is that we as a nation keep making little mistakes which we call accidents which in turn has caused a trend. Failure is now our trend simply because of thinking everything that happens to us is just a mere accident. We should learn to see the chain reaction that our "little" problems are causing us as a nation in the long run. We have left corruption until it has become habitual, we have left nation problems until they have become spiritual and we have kept choosing bad leaders after bad leaders until it has become scriptural. It is as almost we do bad to ourselves now without even thinking about it. it has become a trend!

  So I urge my fellow Tanzanians to sit down and reflect. Look at where we came from, where we are and where we are going. Everything that is happening right now is no accident. We are not poor because of an accident in history. We are not illiterate and unemployed because of an accident. We don't have a high rate of infectious diseases, death and birth mortality because of an accident. We have set a trend and giving excuses for it has gotten us to where we are today. It's sad but it's true.
   
 2. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #2
  May 21, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,197
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Wakati nilipokuwa shule ya msingi tulifundishwa shuleni kuwa ili tuendelee tunahitaji vitu vinne, navyo ni:

  Watu: tunao 44,000,000 and more
  Ardhi : tunayo 945,000 sq km
  Viongozi: bora hatuna
  siasa safi : hatuna.

  So whatever happens is surely because of the absence of the two factors below, siasa safi is brought by a good political party which in turns bring good leadership. Fifty years down the line we have been picking the same party with no serious changes the only way out is to sit down, think and tell others that we lack the two and the only way to get these is to go to the ballot box and vote so that we make the changes that will take us to the land of Honey and Milk.
   
 3. senator

  senator JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  ...will take us to the promised land of Honey and Milk!!..may b 2050 !!
   
 4. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #4
  May 21, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Mkuu tatizo pia lipo kwenye WATU kwa sababu hata kama wakifika BILIONI lakini kama wamejaa uswahili na ubabaishaji kama wa kwetu sisi basi hata hao viongozi bora hatuwezi kuwapata! Lazima tuanze kubadilika kuanzia huku level ya chini...
   
 5. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #5
  May 21, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Umesaema kweli Mkuu..Lakini labda tujiulize ni kwanini tunarudia rida makosa?tatizo ni hasa,kwanini hatujifunzi kutokana na kosa la kwanza?Labda ni tatizo la malezi,au ni nini hasa?
   
 6. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #6
  May 21, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,197
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Just right , that is 40 years from 2010, which is almost the same time that CCM and predecesor has been meesing with the country since independence and nothing so far has been achieved, when you ask them they gonna say University of DODOMA, Secondari za kata, walimu vodafasta basi we are tired of these songs. Change the driver and see where we will be after 40 years. And if you are a doubting Tom you will join the band Wagon in between, before we reach the destination.
   
 7. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #7
  May 21, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,197
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Watu hao wakichagua uongozi bora basi hao viongozi lazima wakiwa na uchungu na nchi wataleta siaisa safi, that is the concept. Lakini kuna kitu cha kweli umesema uswahili na ubabaishaji I can tell you huu ni mkakati uliowekwa kuwafanya idadi kubwa ya watu kuwa wajinga na waamini kuwa Utawala uliopo ndo utamaliza matatizo yao.

  Wakifikiwa na kuambiwa kuwa kama nusu karne hakuna kilichofanyika hawawezi kufanya maajabu kwa miaka mitano au kumi ijayo. Hiki kitu hakijafanyika inabidi kufanyike sasa.
   
 8. M

  Mkandara Verified User

  #8
  May 21, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Tatizo ni UJINGA (kutojui) na ULIMBUKENI (tunajua) unaotufanya kuwa watu wanaojua wakati hawajui..Nitakupeni hadithi moja nilipokuwa Bongo ni vichekesho vitupu. Sikumbuki vizuri tulianzia wapi lakini nachokumbuka ni kwamba nilikuwa nawaambia kwamba DVD ndio chombo kinachotumika kuonyesha sinema sio CD...eeeh bwana wee! waliniita kila majina, wengine wakidai wanazo music system nyumbani na kwenye magari yao zinacheza CD na sinema zote kwa hiyo CD player inaweza kuonyesha vyote. Nitawambia hizo system zao ni DVD player sio CD player, kwani DVD ina uwezo wa kuonyesha both sinema na kupaza muziki lakini CD ni muziki peke yake haiwezi kuonyesha sinema.

  Mkuu nilibakia peke yangu.. wakaniona najifanya kujua sana ili hali mimi niliwanmshangaa kwamba hii ni kitu kidogo sana ambacho mimi nilitegemea wao wanajua kama Wabongo wengi wanavyojua..Well, ktk kundi la watu kama sita hivi nilikuwa peke yangu na mbishi ambaye walicheka sana wakisema ama kweli Mkandara mbishi hawajapata kuona..Pamoja na kuwafahamisha kwangu, akili zao walifikiri mimi nawafanya wao washamba sana wasiojua kitu wakati wao wanajua. Hii ndio Bongo yetu jamani, toka viongozi hadi wasomi habari ndio hiyo hiyo!
   
 9. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #9
  May 21, 2010
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,763
  Trophy Points: 280
  Mkuu....I bet, its not an accident.

  By the way last time I checked the definition of stupidity I found out that: It is doing something over and over again expecting different results. Sasa wewe for the past 50 years tunachagua chama kile kile, watu wale wale..and yet we expect different results? common people...we can do better!

  Jamaa anasema kwamba kusudi tuendelee tunahitaji mambo manne. Siasa safi, viongozi bora, ardhi na watu. Unfortunately, Tanzania tunacho kimoja tuu! Ambayo ni ardhi. Watu, viongozi bora na siasa safi hakuna. Maana viongozi wetu ni reflection yetu sisi tunaowachagua! Go figure!
   
 10. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #10
  May 21, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,197
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Kama ingekuwa hivyo wasingetafuta shilingi 50 billion za nini kama wana ridhaa ya watu. I m sure hizo hela ni za kununua kitu ni kitu gani wanachotaka kununua??????
   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  May 21, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Masanja,
  Mkuu sidhani kama watu ni stupid as such..ila hawajaona njia nyingine zaidi ya ile kama wale wanyama wanaovuka mto Mara kila mwaka wakiliwa na Mamba lakini watarudia hivyo hivyo mwaka unaofuatawatavuka paleplae lakini kwa kutafuta mbinu ya kuvuka haraka na wepesi zaidi. Pengine hawana jinsi ya kufikiria zaidi ya kivuko hicho.

  Mimi nadhani tatizo kubwa la wananchi ni Elimu ya Utawala wenyewe..CCM ndio kivuko chao toka tupate Uhuru na hawaoni njia nyingine zaidi ya kivuko hicho. Itachukua nguvu kubwa sana ya kuwaelimisha wananchi hasa ktk kuelewa tofauti ya haki zao ktk Kutawaliwa na Kuongozwa..Maadam bado tunatumia neno Kutawala badala ya Kuongozwa, siku zote wananchi watakuwa wakisema bora kutawaliwa na zimwi likujualo kuliko...
   
 12. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #12
  May 21, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Viongozi bora hatuna kwa sababu kuchagua viongozi wabovu imekua mazoea(trend) na hatuna siasa safi kwa sababu kukubali siasa mbovu imekua mazoea. Tukumbuke kuwa siasa ni utamaduni na una tofautiana kila sehemu na utamaduni una tokana na watu wenyewe. Viongozi wabovu nao wana toka kati yetu sisi wenyewe kwa hiyo badla ya kuchagua walio bora kati yetu imekua mazoea kuwa chagua waliyo wabovu kati yetu kutuongoza.
   
 13. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #13
  May 21, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135

  Tunaendelea kuona yote yanayo tokea ni bahati mbaya. Wengi wetu tunaendelea kusubiria hiyo bahati nzuri ituokoe.
   
 14. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #14
  May 21, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  I can do you one better mkuu. Nilipo kuwa mtoto binamu yangu alikuja nyumbani na rafiki yake. Kama ilivyo jadi yetu mgeni hukaribishwa kupata cha kula. Ilikua asubuhi kwa hiyo waka karibishwa mezani kwa ajili ya chai na vitafunio. Sasa birika letu la chai lilikua yale ya kubonyeza juu chai itoke.....very simple device. Sasa rafiki yake yule binamu yangu akawa hafahamu na ana pata tabu sana kuweka chai. Binamu yangu ikabidi amuonyeshe na kumuelekeza. Eh yule rafiki yake aka kasirika na kusema "Najua bwana unaona mimi mshamba au?" Sasa mtu kama huyu ambae hataki kuelekezwa kitu ambacho ni wazi hajui ina maana ataendelea kurudia kosa hilo hilo. Kosa dogo ambalo angeondokana nalo siku hiyo. Watanzania tuna attitude ya ujuaji sana na kila akili zetu zikiwa challenged tunaona ni insult to our intelligence.
   
 15. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #15
  May 21, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu I agree with Masanja. Viongozi wetu ni reflection yetu wenyewe. Ni watu wangapi wana fanya ufisadi maofisini na makazini? Kila sehemu watu wana fanya mambo haya sema serikalini kuna kuwa na access kubwa zaidi kwa resources kubwa zaidi. Niamini ni wananchi wengi wange fanya walivyo fanya mafisadi kama wange pata nafasi hiyo.
   
 16. kui

  kui JF-Expert Member

  #16
  May 21, 2010
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 6,478
  Likes Received: 5,146
  Trophy Points: 280
   
 17. M

  Mkandara Verified User

  #17
  May 21, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Pamoja na mjumuiko wa yote haya..tukumbuke tu kwamba Mkandara akipiga Billioni 3 bank nitapongezwa kwa ushujaa na kupata marafiki wengi zaidi..Nitaitwa mimi ndio mwanaume na hata wazazi wangu kunitolea mfano bora. Fikra hizi hazina mpaka kwa wananchi tu na ndio maana watu kama Lowassa, Rostam, Manji wanapendwa hadi huko Ikulu na hakuna uharamu.

  Je, Fikra au utamaduni huu wa kimaskini ambao unaotokana na NJAA utakwisha vipi pasipo kuondoa njaa yenyewe..Je elimu pekee inaweza au kuna mbinu zaidi inatakiwa kutumika - napofika hapa yanikumbusha maneno ya Mh. Magufuli kuhusiana na Polisi jamii!
  Let's deal na majambazi, tuwapige vita wao hizi siasa za reflection tuziache kwa sasa pamoja na kwamba kuna ukweli.
   
 18. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #18
  May 22, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Falsafa hii alizaa Nyerere, Mwinyi kaipeleka ICU ilipougua, Ikafa wakati wa Benjamin Mkapa, Jakaya Mrisho kikwete akaizika kabisa. Naomba tuachane nayo ingawa ilikuwa ni falsafa nzuri sana kuliko hii ya sasa ya maisha bomu kwa kila mtanzania.
   
 19. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #19
  May 24, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,197
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Umesema kweli, Watu wanaona mambo yanayofanyika lakini wanakaa kimya na kuyabaririki. Sababu kubwa ni kuwa kwa njia moja au nyingine wanafaidika ndio sababu baadhi ya watu wanaamini kuwa hata viongozi wabaya wakiwepo wao wanafaidi tu kwa hiyo kwao haijalishi kama kiongozi ni mbaya au mzuri kwao ni matumbo ndio yana matter.
   
 20. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #20
  May 24, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,197
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Mchukia Fisadi kwa nini tuachane nayo hii falsafa mimi binafsi naona hii falsafa ni valid leo, kesho, keshokutwa , milele na milele. Nchi yenye utajiri kama huu what more do we need, watu tumesomeshwa angalau kidogo, std 10 mambo yalikwenda kwelikweli sasa hivi qualifications kibao hata kulima tunamuita muarabu, mkenya , MsouthAfrica , mzimbabwe jamani tumelogwa. Ukiuliza oh wawekezaji utajiri wote huu wawekezaji wa nini tunashindwa nini sisi wenyewe.

  Siasa tunyoamini hivi sasa ni nini, hakuna kiongozi anayejua, katiba anasema ibara ya 3 (1) Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa.

  Katiba ya chama cha mapinduzi nayo inasema kuwa imani ya CCM ni : Ujamaa na Kujitegemea ndiyo njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru. Wakati huohuo malengo na madhumuni yao ni :Kuhimiza ujenzi wa Ujamaa na Kujitegemea kwa mujibu wa Azimio la Arusha.

  Sasa tujiulize viliandikwa vitabuni ndivyo vinavyofanyika? Mimi binafsi naona ni tofauti kabisa siasa ya sasa hivi ni mchanganyiko wa madudu mengi tu ambayo hayapo kwenye chama wala katiba ya nchi.
   
Loading...