Matunzo 02
JF-Expert Member
- Jul 7, 2026
- 1,237
- 2,390
sasa huwa mnatakaje et bibieTuikutana kwenye basi safari ya Dar-Arusha. Mkaka mrefu mweusi halafu hb kiasi (mambo nipendayo). Mie nikisafiri sio mtu wa kuhangaika na niliyekaa nae. Nikishasalimia basi ear phone zangu natulia au nasinzia.
Kufika moshi ndio tukaanza kuzungumza baada ya kuniuliza kitu maana mie kidogo nilikuwa mwenyeji. Mwisho wa safari tukabadilishana namba za simu.
Baada ya kuwasiliana kwa miezi mitatu tukapanga kuonana kwa first date Dar hotel fulani hivi. Nilitupia nikapendeza sana. Ile kufika akawa na kazi ya kusifia tu. Tukapata chakula na vinywaji then kufika mida fulani nikamuaga, akaomba niende nae kwake tukalale. Nikamwambia asiwe na haraka maana mambo mazuri hayataki haraka. Hivyo tujipe muda zaidi wa kufahamiana.
Episode 3 ndio ilikuja kunimaliza nguvu , nilivyotoka hapo ndio ikawa nitolee. Alinitafuta sikupokea wala kujibu msg.