Mutual funds simply means kwamba kikundi cha watu kinachanga pesa na kufanya biashara.
Kinaweza kuamua kununua hisa kwenye makampuni yaliyosajiliwa, kinaweza kuanzisha biashara zake, kinaweza kuinga ubia, inaweza kufungua fixed deposit acc, kinaweza kununua treasury bills etc.
Mfano wake ni NICOL ambayo sasa hivi account zake zimefungiwa kwa sababu imeshindwa kujiendesha kwa kufuata taratibu.
Story na NICOL ni ndefe lakini in a nutshell ni kwamba viongozi wa NICOL ni Mengi na wenzake, later NICOL ikanunua kiwanda cha mdogo wake Mengi kwa bei kubwa kuliko thamani ya kiwanda kinyume na ushauri wa consultants. Jambo hilo pamoja na maamuzi mengine yasiyo sahihi yamesababisha NICOL kufirisika.
Ukiangalia utaona watu kama Mengi ambao biashara zao zinaenda vizuri kwa mafanikio lakini wanapoongoza biashara ya wengi tayari wanajifanya hawana uwezo wa kufanya maamuzi sahihi! Hii ni dalili ya ubinafsi na ndio sababu watu hawataki kushiriki kwenye biashara za watu wengi wasiowafahamu.
Mimi ninaadvocate vikundi vya watu wanaofahamiana vya watu kati ya 50-100. Nilishaandika mradi unaitwa 100 millionaires project na kuwapa vijana. hata hivyo vijana walikuwa wazito kwenye utekelezaji. Mradi ulitaka kila kijana achange sh. mil 10 ili wakiwa 100 wapate sh. bil 1 na kuanzisha bishara ya maana. mnaona Dewji alianza na almost the same amount lakini sasa hivi ana revenue ambayo ni about 3% ya GDP ya Tanzania! Just imagine vijana 100 wangeweza kujijengea uwezo wa aina hiyo, isnt that amazing?
Ili biashara za watu wengi au vikundi zifanikiwe ni lazima kuwe na wachache kati yao ambao ndio wanaotekeleza mipango ya pamoja na kuisimamia kwa moyo wote. Biashara haiwezi kuendeshwa kama vyama vya siasa. NICOL iliendeshwa kama chama cha siasa, ndio maana ikafirisika.