1. Ni kweli maridhiano yalifikiwa Arusha. Na yalitakiwa kueshimika na pande zote mbili serikali ya wakti huo na RPF....Lakini kabla ya kuanza kutekeleza maridhiano hayo, inatokea kadhia inayoondoa uhai wa mtu/watu muhimu katika makubaliano hayo, Rais wa Rwanda (Mungu amurehemu) na kufuatiwa na mauaji ya kutisha yanayosemekena kufanywa kwa kiasi kikubwa na baadhi ya viongozi na askari wa serikali ya wakati huo, na kikundi cha RPF kilichokuwa kikipigana kuiteka Kigali kwa madai ya kukomesha mauaji. Mpaka RPF wanafika Kigali viongozi wa serikali ambao walitakiwa kutekeleza kwa pamoja na RPF, makubaliano ya Arusha walikuwa ama wamekimbia nchi au kuuwawa wakati wa harakati za RPF kuikamata Kagali. Sasa katika mazingira haya RPF/Kagame angetekelezaje makubaliano hayo bila kuwepo upande wa pili?
Kagame kwa kutambua umuhimu wa upande wa pili katika kuwaunganisha tena waafrika wa Rwanda akaona ni vyema kuwa na mfumo wa kimaridhinao ambao ulikuwa na lengo kama lile la makubalino ya Arusha. Mfumo huo ndiyo GACACA. Na ni katika GACACA ambapo upande wapili ulikuwa umepewa nafasi ya kurudi mezani kutekeleza maridhiano (rejea post na.44 ya uzi huu na soma nukuu ). Upande wa pili haukukubali...wakaenda mafichoni huko misitu ya Kongo(FDLR) wakaanza kuleta chokochoko za kuhatarisha usalama wa waafrika wenzao walioko Rwanda.....kilichoendela unakijua. Narudia tena katika mazingira haya utamlaumu vipi Kagame kushidwa kutekeleza maridhiano ya Arusha?
2. Nashukuru sana kwa kukutambua kuwa na wewe pia ni mwafrika mwezetu. Ni wie radhi kwa kutokutambua mapema kuwa na wewe ni mwafrika mwenzangu. Na sababu ni moja tu ya kutokukutambua nikuwa nilipoangalia JF ID yako nikaona wewe siyo Verified user hivyo imeniwia vigumu kutumia mbinu za kukutambua kuwa wewe ni Mwaafrika.
Uwenda ukawaza kuwa nilifanya makusudi kuwa sijakutambua kuwa wewe ni mwafrika kwani unaweza kuandika lugha ya kiswahili vyema! kwamba hiyo inatosha kukutambua. Siku hizi kiswahili kinazungumzwa na kuandikwa kwa ufasaha na wachina, wazungu, nakadhlika nakadhaliaki.
Kwa leo naishia hapa.
1. Nashukuru kuwa umekubali kuna ombwe la serikali ya Habyarimana kutokana na serikali hiyo kupinduliwa na kagame. Katika hali hiyo tunakubaliana kuwa Kagame hakuwa na uhalali wa kukamata madaraka and therefore jukumu la kujifanya analeta maridhiano wakati upande mmoja wa maridhiano ni yeye mwenyewe, na upande wa pili uko msituni DRC.
Serikali ilishakubali maridhiano via Arusha accord, na hata sasa FDLR ambao baadhi yao ni "serikali ya habyarimana" wako tayari kwa mazungumzo.
Tatizo hapa ni kuwa mazungumzo yoyote yale kagame hayuko tayari, kwa sababu mwisho wa mazungumzo atapoteza madaraka.
2. Inaonekana historia yako ya FDLR imeathiriwa na propaganda za kagame. Usichanganye serikali ya Habyarimana na FDLR. FDLR ni kitu tofauti na serikali ya Habyarimana ingawa baadhi ya waliokuwa wanajeshi wa Habyarimana wamo ndani ya FDLR. FDLR is a different entity iliyoundwa mwaka 2000, kutokana na mashambulizi ya kagame ndani ya DRC ambayo documetary imeonyesha, mashambulizi ambayo hata UN inayaita genocide kwenye report zake ambazo ziko suppressed kutokana na shinikizo la kisiasa. FDLR ni defense force, na kwa maneno yao wenyewe walishasema hawawezi kuvamia Rwanda kwa sababu hiyo itahatarisha usalama wa wahutu majority ambao wanaishi chini ya udikteta wa Kagame. Silaha ambazo wanazo ni kwa ajilii ya kujilinda na mashambulizi ya kagame huko huko waliko.
mashambulizi yote yanayodaiwa na kagame kuwa yanatoka FDLR ni matukio ya kutunga, FDLR wamekataa na independent sources pia zimebaini kuwa kagame ni muongo. Just like the recent UN report on DRC ilivyothibitisha kuwa kagame alikuwa analipua mabomu Rwanda akisingizia yametoka Monusco ili apate kisingizio cha kupeleka majeshi yake DRC. Na indeed alifanya hivyo!
However, while FDLR does not represent serikali ya habyarimana per se, it is the closest representation of the Hutu majority ndani ya Rwanda.
Kilichotakiwa kufanyika ni kwa kagame kutochukua madaraka, kuacha international community ihukumu wahusika wa genocide ndani ya serikali halafu Arusha accord iendelee.
3. Hapo kwenye uafrika wangu naomba nikuulize nini kilifanya udhani kwa maneno yako kuwa mimi sio mwafrika? Kuna mahala popote pale kwenye data ninazotoa kuhusu mjadala huu ambazo labda zimekosewa sana kiasi cha kuleta shaka uafrika wangu? what was your basis of your assumption?