File Langu Limepotelea Halmashauri, Nifanyeje?

Posho City

JF-Expert Member
Mar 15, 2012
643
250
Mimi ni mtumishi mwalimu katika halmashauri x Niliondoka kazini bila ruhusa na mwezi uliopita nilirudi kituoni na nkamwandikia barua mkurugenzi kumuomba anirudishe kwenye payroll maana nshafutwa tangu Sept. 2013.

Afisa elimu yeye alipendekeza nifukuzwe kazi ila mkurugenzi aliwaomba TSD ndo watoe uamuzi wa suala langu. TSD waliamua kesi na kuamuru nirudishwe payrole kwa sababu licha ya kutokuwa kazini muda mrefu mwajiri hakuwahi kunionya au hata kunituhumu kwa utoro, then wakapeleka mapendekezo kwa DED.

Cha ajabu file linaonekana kwa DED limetoka baada ya kufanyiwa kazi na likaelekea kwa DEO lakini masjala ya DEO halijapita na kwa DEO halipo na nimelitafuta leo siku ya pili halmashauri nzima hakuna.

Wameniambia niwe mvumilivu hadi jumatatu ili walitafute kwa utulivu.

Je likiendelea kutoonekana nichukue hatua gani?
 
Elli Mshana

Verified Member
Mar 17, 2008
40,080
2,000
Acha utoto Mpwa as if hujawahi kukutana na vitu vya namna hii, ukishakutana na mazingira kama hayo (just for future use) zama mfukoni toa buku mbili au tano mpatie halafu fumba macho, nakuhakikishia kuiyafumbua tu, faili utakua nalo mkononi na limeshasainiwa kila kitu......usiwe mgumu, hawa watu wana njaa sana. Ukienda hospital, polisi na kwenye maofisi mengine ya serikali, omba au tafuta chochote utapata hata mhuri wa Rais na signature yake utapata ONLY that usiwe mgumu............

Sishabikiii rushwa lakini ndio nchi yetu pendwa ilipofikia, ukijifanya mgumu una-lost. Take care
 
Mbekeche

Member
May 5, 2013
65
0
Wakufukuze tu, tena ikiwezekana upelekwe mahakama ya kazi kwa vile kuna watu wengi wamekosa huduma yako na kufeli kutokana na utoro wako. Kama ulikua hauna wito ni bora usinge enda ualimu kwa maana inaonekana hiyo kazi unaifanyia kwa dhiki ya ajira tu. Halafu mkikaa vijiweni kazi ni kuwaponda watoto hoo! division 5.
 
Posho City

JF-Expert Member
Mar 15, 2012
643
250
Wakufukuze tu, tena ikiwezekana upelekwe mahakama ya kazi kwa vile kuna watu wengi wamekosa huduma yako na kufeli kutokana na utoro wako. Kama ulikua hauna wito ni bora usinge enda ualimu kwa maana inaonekana hiyo kazi unaifanyia kwa dhiki ya ajira tu. Halafu mkikaa vijiweni kazi ni kuwaponda watoto hoo! division 5.

sasa na wewe ndo umeandika nn?sababu ya kuniondoa payrole wanasema utoro ila utoro gani mtu nilienda masomoni? nisisome kisa watoto wapate huduma yangu?
huna akili timamu maana hata nilichoandka sicho ulichochangia..
 
Maukiddo

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
207
225
sasa na wewe ndo umeandika nn?sababu ya kuniondoa payrole wanasema utoro ila utoro gani mtu nilienda masomoni? nisisome kisa watoto wapate huduma yangu?
huna akili timamu maana hata nilichoandka sicho ulichochangia..
Kweli nyie walimu hamnazo kabisaaa...wewee unasema mwenyewe uliondoka bila ruhusa halafu unakuja humu kuomba ushauri tena na kuwaka faili lako limepotea sijui taifa gani hili...
Nilizani serikali inawanyima stahiki zenu inakosea kumbe ipo sahihi kabisa kwa wewe ulichofanya yaani wapo sawa asilimia mia moja maana hauna hata chembe ya kuitwa mwalimu mtu kama wewe...
Na lipotee hivyo hivyo lisionekane kwani watu wanaoenda kusoma wanatumia njia kama zako hizo si ndio...!!!
 
Mbekeche

Member
May 5, 2013
65
0
sasa na wewe ndo umeandika nn?sababu ya kuniondoa payrole wanasema utoro ila utoro gani mtu nilienda masomoni? nisisome kisa watoto wapate huduma yangu?
huna akili timamu maana hata nilichoandka sicho ulichochangia..

Bora serikali imeondoa udahili wa waalimu wenye division4 maana Mwl kama wewe inaonekana haujitambui kabisa, unawezaje kuondoka ktk kituo chako cha kazi bila ruhusa kisha ujione sio mtoro eti kwa vile ulienda kusoma? Inaonesha hata cheti uliiba tu.
 
Mbekeche

Member
May 5, 2013
65
0
Kweli nyie walimu hamnazo kabisaaa...wewee unasema mwenyewe uliondoka bila ruhusa halafu unakuja humu kuomba ushauri tena na kuwaka faili lako limepotea sijui taifa gani hili...
Na lipotee hivyo hivyo lisionekane kwani watu wanaoenda kusoma wanatumia njia kama zako hizo si ndio...!!!
Huyu ticha hamna kitu kabisa, eti anaona kaonewa, eti wameniondoa ktk payrole sijui ndio anamaanisha payroll au? Hapo ndoa ametoka kuongeza elimu ila hajitambui je kipindi hicho ajaongeza?
 
Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Sep 29, 2012
3,409
0
sasa na wewe ndo umeandika nn?sababu ya kuniondoa payrole wanasema utoro ila utoro gani mtu nilienda masomoni? nisisome kisa watoto wapate huduma yangu?
huna akili timamu maana hata nilichoandka sicho ulichochangia..

Unafahamu maana ya utoro????? Hujawahi kusikia mwanafunzi aliondoka shule akarudi kwao akafukuzwa kwa kesi ya utoro???? wewe ni wakufukuzwa tu, watu wazembe wazembe kama wewe ndio mnafanya taifa hili lina yumba, nitalifatilia suala.LAZIMA NIKUSHUGHULIKIE
 
Posho City

JF-Expert Member
Mar 15, 2012
643
250
Huyu ticha hamna kitu kabisa, eti anaona kaonewa, eti wameniondoa ktk payrole sijui ndio anamaanisha payroll au? Hapo ndoa ametoka kuongeza elimu ila hajitambui je kipindi hicho ajaongeza?

kweli dada taarabu unaweza
 
meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,158
2,000
Ukikutana na bosi strict kama mimi,kamwe hurudi kazini!
Chezea mshahara sio kazi
 
Kind

JF-Expert Member
Oct 29, 2011
247
0
Acha utoto Mpwa as if hujawahi kukutana na vitu vya namna hii, ukishakutana na mazingira kama hayo (just for future use) zama mfukoni toa buku mbili au tano mpatie halafu fumba macho, nakuhakikishia kuiyafumbua tu, faili utakua nalo mkononi na limeshasainiwa kila kitu......usiwe mgumu, hawa watu wana njaa sana. Ukienda hospital, polisi na kwenye maofisi mengine ya serikali, omba au tafuta chochote utapata hata mhuri wa Rais na signature yake utapata ONLY that usiwe mgumu............

Sishabikiii rushwa lakini ndio nchi yetu pendwa ilipofikia, ukijifanya mgumu una-lost. Take care

Kweli ndipo tulipofikia hawaombi kwa nguvu ila wanataka kama kuhurumiwa
 
Posho City

JF-Expert Member
Mar 15, 2012
643
250
Unafahamu maana ya utoro????? Hujawahi kusikia mwanafunzi aliondoka shule akarudi kwao akafukuzwa kwa kesi ya utoro???? wewe ni wakufukuzwa tu, watu wazembe wazembe kama wewe ndio mnafanya taifa hili lina yumba, nitalifatilia suala.LAZIMA NIKUSHUGHULIKIE

Hilo file limepotea tangu february hadi leo na payroll nazungushwa kisa file hakuna.sasa wewe unaleta porojo hata hujui undani wa ishu.kakojoe ulale bwana.
 
Cartoo

Member
Jan 21, 2014
72
70
Hilo file limepotea tangu february hadi leo na payroll nazungushwa kisa file hakuna.sasa wewe unaleta porojo hata hujui undani wa ishu.kakojoe ulale bwana.
Duh! Wewe mwalimu, enzi zile tunasoma tungekuita mwl Payrole. Ukiwa kama mwalimu yaani unashindwa kweli kujibu watu vizuri! maana kila mtego unaingia mzima mzima. Nyie ndio mnadhalilisha wahaya kwa kuonekana kazi mnapeana kiukoo, kwa kweli naona unawaharibia hata hao walikusaidia kwa kuleta majigambo yako.
 
NetworkEngineer

JF-Expert Member
Jun 21, 2012
1,864
2,000
Walimu kweli mnadekezwa, hivi fikilia haya ayafanye mtumishi mwingine kama mhasibu wa TRA, kwa kuondoka ofisini bira ruhusa kwenda kusoma akitegemea akirudi aendelee na kibarua chake..hivi huu mtindo ukifanywa na kila mtumishi wa ummaa tutaendelea kweli? Harafu anasema eti hajatoroka kisa kaenda kusoma. Haijarishi ulikokwenda umekwenda kufanya nini, kitendo cha kuondoka bira ruhusa ni utoro na ulipaswa kufukuzwa kazi..kweli Tanzania ni zaid ya uijuavyo na ndio maana hatuendelei, mtu anajiondokea tuu, anakwenda kufanya mambo yake.
 
NetworkEngineer

JF-Expert Member
Jun 21, 2012
1,864
2,000
Mtoa mada acha kutuibia wewe hukwenda kusoma, ulikimbia mazingira magumu ona post yako hii

IFUBA KYA ITAHWA 08:25 13th March
2014
Wadau mimi tangu 2007
nimeajiriwa katika halmashauri ya
Biharamulo kama mwalimu.2012
niliamua kuondoka kituoni na
nkaenda shule ya private hapa
Mwanza,mwaka jana kuna kazi ya
ualimu katika mojawapo ya shule
za mashirika ya umma ilitangazwa
na tume ya ajira nikaomba na
nimepata kazi.
Tatizo walipoenda kuniingiza
kwenye system ikaonekana
nshaajiriwa serikali.Kwahyo
natakiwa kurudi Biharamulo na
kuomba nirudishwe payroll na
nihamishe datasheet.
Je wadau ni njia gani nyepesi
nitumie ili nifanikiwe katika hili na
ukizingatia niliondka kazin kwa
kukimbia mazingira magumu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom