TSD vs katibu mkuu utumishi

Posho City

JF-Expert Member
Mar 15, 2012
648
416
Nilipata matatizo nikaondoka kazini bila taarifa kwa mwajiri wangu.Kilichofata mwajiri akanifuta payroll. Baadae nikapata kazi nyingine ya serikali kwenye taasisi nyingine..lakini ishu ikaja kwamba nilishawahi ajiriwa kwahyo siwezi fanya chochote hadi nirudi kwa mwajiri wa zamani anirudishe payroll then anihamishe au niombe kibali cha katibu mkuu kiongozi cha kuniruhusu kuajiriwa upya.
Niliomba kibali hicho na pia nkaenda kwa mwajiri wa zamani na nkakuta tsd( kamati ya nidhamu kwa walimu) ishanifungulia mashtaka ya utoro.

Kabla tsd hawajatoa uamuzi wa shitaka lao kibali cha katibu mkuu kikatoka huku kikiniruhusu kuhamisha cheki namba na kuajiriwa upya...Kibali nilikipeleka kwa mwajiri wa zamani na cheki namba ikahamishwa na sasa nipo kwa kazi mpya yapata huu mwezi wa tatu.

Dukuduku langu je..tsd wa mwajiri wa zamani ikitokea siku wakitoa uamuzi maybe wakasema nifukuzwe kazi..Je naweza athirika kwa kazi mpya nilipo sasahivi au ndo imetoka?
 
Wakati nahamisha cheki namba tsd hawakujua maana kibali kile ni nyaraka ya siri kwhyo ilitumwa kwa DED na yeye akampa afisa utumishi akamaliza kazi.
 
TSD sio mamlaka yako ya nidhamu tena maanake ni kwamba hata wakikufukuza watakuwa wanajisumbua bure.
 
Mh nijuavyo mimi hiyo ndo imetoka maana haupo tena chini ya tsd, wanaweza wakatoa huo uamuzi wao but hautakugusa
 
Nimewaelewa wadau....kibali cha katibu mkuu kimeniokoa...Maana kuna mjumbe mmoja wa ile kamati ashanidokeza kuwa...walipendekeza nifukuzwe kazi bila utumishi..
 
Back
Top Bottom