Fikra za January Makamba Kuhusu katiba Mpya

kinepi_nepi

JF-Expert Member
Aug 16, 2007
869
236

  • January Makamba
    Tuzungumze Katiba mpya. Why is the current one inadequate? Why do we need an entirely new one instead of amending problematic provisions? Are "patches" (amendments) sufficient reason to rewrite the constitution? (USA constitution has 27 amendments). Is the constitution really that critical for development (UK does not have one). What process do we use to determine the contents of new constitution?





 


  • January Makamba
    Why do we need an entirely new one instead of amending problematic provisions? Are "patches" (amendments) sufficient reason to rewrite the constitution?


  • Tanzania Constitution is "Obsolete"...... i can not thesauri when such language like problematic provision are used to relate the current situation regarding the need for a new draft constitution in Tanzania..... it is not a sin to draft a new constitution that will definitely bring hope for change....

    this man was really a presidential aide .... what caliber is he of in terms of intellectual perception... i wonder
 
"Katiba ya nchi ni msingi na chimbuko la sheria zote nchini pamoja na uwezo wenyewe wa kutunga na kuendesha utawala kwa mujibu wa sheria. Katiba hugawa nguvu za dola kwa vyombo vikuu vitatu - yaani vyombo vya utungaji sheria, vyombo vya utendaji na vyombo vya utoaji haki.

Mgawanyo wa nguvu za dola kati ya vyombo vilivyotajwa na kutokuingiliana katika madaraka ya vyombo hivyo ni msingi mojawapo wa utawala wa demokrasia ya kiliberali. Walakini, muhimu zaidi kuliko vifungu vya katiba ambavyo ni wazi, ni itikadi inayo halalisha utawala na matumizi ya madaraka kwa upande wa tabaka-tawala dhidi ya matabaka-tawaliwa.

Tangu Tanzania ipate uhuru wake kumetungwa katiba nne (au tano) mpya na marekebisho mengi ya mara kwa mara. Katiba ya kwanza kabisa ilikuwa Katiba ya Uhuru ya mwaka 1961. Umuhimu wa Katiba ya 1961 ni kwamba ilikuwa kama njia ya kutoa uhuru kwa Tanganyika. Kwa wananchi na viongozi wao katiba hii haikuwa kama muafaka wa siasa kati ya watawala wa ndani na watawaliwa bali ilikuwa hitimisho la mapambano ya kitaifa dhidi ya ukoloni.
Kwa kweli, katiba yenyewe ilitungwa na wataalamu wa ofisi ya koloni huko Uingereza na katiba iliwekwa kama nyongeza (schedule) ya Sheria ya Uhuru wa Tanganyika iliyopitishwa na Bunge la Uingereza.

Ushirikishwaji wa wananchi katika Utungaji wa Katiba: Tukiangalia historia ya utungaji katiba katika nchi yetu, hatujawa na tabia wala utamaduni wa kuhusisha na kushirikisha wananchi kwa jumla yao katika mijadala ya katiba.

Katika nchi za Afrika, ikiwemo Tanzania, kama nilivyoonyesha, katiba ilikuwa na nafasi tofauti. Katiba imekuwa kama ramani ya kurekodi ugawaji wa nguvu na hasa kuweka ukiritimba wa nguvu za dola mikononi mwa chombo cha utendaji chini ya rais, kwa upande mmoja, na kuweka ukiritimba wa mambo ya kisiasa mikononi mwa chama kimoja, kwa upande mwingine.

Kama msomi na kama mwananchi, ningependa kusisitiza kwamba kuna haja kubwa na nyakati hizi ni nafasi nzuri ya kihistoria kuangalia na kutafakari upya hoja ya kutunga katiba mpya.
Kazi kama hii haina budi ifanyike bila jazba na bila ushindani wa kisiasa, bali kwa kuweka matakwa ya taifa mbele ya ubinafsi na maslahi ya chama chochote kile. "

Profesa Shivji
hs3.gif
 
Kwahiyo anataka tuwafuate USA na UK kwenye katiba, ila demokrasia ya kura tufuate tunachokijua sisi?Wenzetu hawachakachui kura maana wanaheshimu demokrasia!
Double standards za waafrika nazo ni tatizo kubwa sana. Kweli kila mwamba ngozi huvutia kwake. Hii katiba inawaneemesha waliomo.
 
Huyu January ndio yule mtoto wa babu jinga Makamba? au ni surname ndio imefanana?
 
  • January Makamba
    Tuzungumze Katiba mpya. Why is the current one inadequate? Why do we need an entirely new one instead of amending problematic provisions? Are "patches" (amendments) sufficient reason to rewrite the constitution? (USA constitution has 27 amendments). Is the constitution really that critical for development (UK does not have one). What process do we use to determine the contents of new constitution?




If English language is obstacle to you, then use whatever language is understood by a majority of your readers. I detest people who use language that they are not comfortable with and as a result they do not convey the right message to their target readers
 
If we agree on genetics theory,no one should expect something different from this son of Leftenant Yusuf Makamba
 
If we agree on genetics theory,no one should expect something different from this son of Leftenant Yusuf Makamba
<br />
<br />
Hakuna cheo kama leftenant katika jeshi,bali kuna lieutenant ambayo kwa kiswahili tunaita luteni ambacho ni moja ya vyeo vya commissioner officers. Naamini ulitaka kumrefer luteni makamba hivyo!
 
Kwahiyo anataka tuwafuate USA na UK kwenye katiba, ila demokrasia ya kura tufuate tunachokijua sisi?Wenzetu hawachakachui kura maana wanaheshimu demokrasia!
Double standards za waafrika nazo ni tatizo kubwa sana. Kweli kila mwamba ngozi huvutia kwake. Hii katiba inawaneemesha waliomo.


Umenena mkuu, kama kuiga tuige yote basi!

 
January kauliza maswali mazuri tu mojawapo ambalo na mimi niliuliza hapa nalo ni la maendeleo. Je katiba mpya ndo itakuwa mwarobaini wa matatizo yetu ya kimaendeleo?
 
If English language is obstacle to you, then use whatever language is understood by majority of your readers. I detest people who use language that they are not comfortable with and as a result they do not convey the right message to their target reader
Mkuu na wewe umerudia yaleyale "tahadhari na kurusha mawe kama unaishi nyumba ya vigae"
 
January Mkamba:
-yeye katiba iliyopo sasa amempa ulaji(ana masilahi nayo)
-yeye ni mtoto wa fisadi
-Yeye is a layman in Legal affairs
-Yeye ana profession ya kushughulika na wakimbizi.
-Yeye anapenda katiba iliyopo ili izae wakimbizi, naye apate kazi.
-Yeye amesoma chuo ambacho ni narrow minded college, I have been once at St. John's college in the US.I know what it very well.
Wherefore now the nation needs a second Republic by created a brand new constitution.
 
Mbona January hajajiuliza kinyume kuwa iandikwe katiba mpya halafu tuchukue ambayo yanatufaa kutoka katiba ya sasa?? Au anaona maslahi yao hayatalindwa anataka tuvisahau baadhi bila kurekebishwa!!!,watz nowdays tumekwenda shule na kuelimika,hapo anachemsha.
 
January Mkamba:
-Yeye is a layman in Legal affairs.

Give me a break! What now...one needs a J.D. to talk about the constitution?

Kuna mtu juzi hapa kaanzisha mada ya kasichana ka lawyer kalikoapishwa juzi kati kuwa kalikataa kuongelea suala la katiba kwa vile hilo ni suala la "kisiasa". Supposedly lawyer huyo...a "learned sister" kama wanavyoitana wenyewe. With a comment like that indeed she is "learned".

Kuisoma na kuichambua katiba na kuonesha mapungufu yake si lazima uwe na L.L.B. ya UDSM!
 
Kweli ukoo wote wa Makamba ni sifuri... Nilitaka kuja kuoa huko,lakn naacha! Mtanzania gani aliyeenda shule mwenye degree anayekataa katiba mpya? Damn and shame 2 u,pompopooo!
 
UK wanayo katiba ila tu haijaandikwa (unwritten constitution). Usijaribu kuleta uzushi,katiba mbovu inalinda wabaka uchumi wasifikishwe mahakamani.
 
JANUARY MAKAMBA ANAWAKILISHA KUNDI LINALONUFAIKA NA UTAWALA WA SASA NA AMBALO NADHANI LINAJIPANGA KUZUIA JITIHADA ZA KATIBA MPYA LABDA MPAKA DAMU IMWAGIKE KAMA KENYA. JANUARY ANAFANYA REFERENCE KATIBA YA USA LAKINI SIAMINI ANAFANYA REFERENCE KWA MAMBO YOTE. ZIPO SABABU NYINGI KUDAI KATIBA MPYA

1. KATIBA YA SASA INARUSU MFUMO MBOVU WA KIUNGOZI KWA SABABU HIYO UCHUMI HAUWEZI KUPIGA HATUA KWA WATAWALA NA MADIKITETA

2. KATIBA YA SASA IMEMINYA DEMOKRSIA YA KUCHAGULIWA NA KUTHIBITI WALIOCHAGULIWA -KWAHIYO HATUWEZI KUPATA TIJA YA MAENDELEO KIUCHUMI, KIUTAMADUNI NA KIJAMII-WATAWALA WA SASA HAWAWAJIBI KWA WATANZANIA -mfano niambie ni watoto wangapi wankufa kwa vifo visivyokuwa vya lazima kama watoto watano waliozaliwa juzi hapa pale shinyanga na watatu kufa kwa sababu ya huduma?

3. KATIBA YA SASA INARUHUSU GENGE LA KINA JANUARY KUTUMIA RASILIMALI ZA NCHI WATAKAVYO BILA MIPAKA-KWA MAANA KWAMBA HAKUNA CHECK AND BALANCE -

HAKUNA AMANI PASIPO NA HAKI NA HAKUNA DEMOKRASIA PASIPO NA HAKI HAKUNA SASA KWANINI TUSICHUKUE KATIBA MPYA. JANUARY NA WENZAKE LAZIMA WAJUE KWAMBA USULTANI UMEFIKA MWISHO WATANZANIA TUNATAKA MABADILIKO.

ZIPO SABABU NYINGI KUDAI KATIBA MPYA
 
Kaitba na J.Makamba:
-Utajua mapungufu yaliyomo kwenye katiba kwa kuisoma katiba yenyewe, siyo tu kwa kusikia majukwaani.
-Huyo learned sister aliyeapishwa, hajui sources of Law. Katiba is the most fundamental source of Law. Sheria yoyote inayoenda kinyume cha kaiba ya nchi ni null and void. Huyo demu ni miongoni mwa mafisadi wa elimu nchini.Ameapishwa bila kuwa na haki ya kuapishwa. Suala la Katiba ni suala zaidi la kisheria kuliko kisiasa. Ndani ya katiba yetu kuna inconsistencies nyingi sana katika vifungu vyake na vingi vimepitwa na wakati.
 
Kusoma na kuielewa katiba wala si kazi ngumu. Katiba ya Tanzania haikuandikwa na Shakespeare!!
 
Back
Top Bottom