Kwa nyakati tofauti Lowassa na viongozi wengine wa chadema wamekuwa wakitoa kauli kuhusu Wafanyabiashara wakubwa , kauli ambazo hapana shaka , endapo Chadema wangefanikiwa kuunda serikali chini ya Edward Lowassa, basi kwenye upande wa kukusanya kodi wafanyabiashara wakubwa wasingeguswa kabisa au kungekuwa na hali kuwanyanyasa wale wafanyabiashara ambao wangeonekana kutokiunga mkono chama hicho.
1. Juzi alikaririwa na vyombo vya habari kutoka Monduli akisema Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa maelekezo ya Serikali imekuwa ikiwatoza kodi kubwa Wafanyabiashara kwa sababu waliifadhili Chadema kwenye kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka jana. Kauli kama hii pia aliitoa jijini Mwanza akiwa kwenye msiba wa aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema wa mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo.
2. Wakati wa harambee ya CHADEMA iliyofanyika septemba 22 mwaka jana , mwenyekiti wa Chamahicho, Freeman Aikaeli Mbowe alisema kulikuwa na matajiri watano wenye uwezo wa kiuchumi ambao walikuwa tayari kukisaidia kwenye shughuli zake za kampeni lakini hawataki kutajwa majina yao kwa hofu ya kufuatiliwa na vyombo vya dola.
TAFAKURI:
1. Ni wazi kabisa Lowassa angekuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania asingeweza kabisa kuwabana Wafanyabiashara wakubwa katika swala zima la kukusanya kodi hasa ukizingatia kuwa walikifadhili chama hicho. Aidha dhana ya kwamba wafadhili wa Chadema wananyanyaswa na TRA ni uthibitisho kwamba hizi ni hisia ambazo alifikiria kuwafanyia wale wafanyabiashara ambao wasingejitokeza kukifadhili chama chake na kufikiria kuwa Serikali ya JPM nayo ina mawazo ya kipuuzi kama hayo. MAGUFULI siyo mtu wa visasi kama LOWASSA.
2. Lowassa kusema kwamba siyo suala la kutaja majina ya wafanyabiashara wanaonyanyaswa bali CCM ifanye utafiti(Reseach) ni makosa na pengine labda hajui wakati gani na nani wa kufanya utafiti. Serikali ya CCM ndiyo anayoituhumu kuwanyanyasa wafanyabiasha waliofadhili Chadema. Kwa mantiki hiyo CCM kama mtuhumiwa hawezi kufanya utafiti. LOWASSA na CHADEMA yake ndiyo waathirika na kwa maana hiyo wao ndiyo wanawajibika kufanya utafiti kama wamekurupuka kuyasema haya bila kufanya hivyo au kama wamefanya utafiti na kujiridhisha, wanawajibika kutaja majina hayo ili Umma kuujua ukweli.
3. Kikubwa kabisa. Zama za kukumbatia Wafanyabiashara kwa sababu tu ya ufadhili wao kwa vyama vya siasa zimepitwa na wakati. LOWASSA anapaswa kuona AIBU kutamka maneno kama ufadhili wa wafanyabiashara kwa vyama siasa kwani yanazidi kurutubisha UFisadi wake wa tangu enzi na enzi. Lowassa anataka kutuambia wafanyabiashara wanaonyanyaswa ni akina nani? ROSTAMA AZIZ na kundi lake au wale Wafanyabiashara watano wakubwa kiuchumi ambao Mwenyekiti alisema wanaogopa kutajwa majina yao? AIBU HII.
Kinachotakiwa tu ni kufuata sharia za nchi na sharia za kodi, hawa wanasiasa waache blaa blaa siasa zimeisha. Unapofuatwa kulipa kodi kinachotakiwa kufanya ni kuthibitisha umelipa kodi stahiki na sio vinginevyo. Hata tunaofanya kazi kwenye - Makampuni makubwa TRA wanafanya hivyo hivyo. Tatizo la wafanya biashara wetu wanafanya biashara kisanii sanii. Hata anayeuza bia tu/soda hajui kwamba VAT - 18% ni kodi ya serikali. Walipe tu au wathibitishe kama wamelipa na sio kuanza blaa blaa kupitia wanasiasa.