FIFA yaishika pabaya Simba, ratiba ngumu kwa mpambano wao na Al Alhy

CAPO DELGADO

JF-Expert Member
Aug 31, 2020
7,621
16,700
WAKATI Simba ikiendelea kujiandaa na mechi ya ufunguzi wa michuano mipya ya African Football League (AFL) dhidi ya Al Alhy ya Misri, ghafla imejikuta ikianguka kwenye mtego kutoka Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kutokana na ratiba ya mechi za timu za taifa ilivyo.

Hivi sasa ligi nyingi ikiwemo ya Tanzania zimesimama huku mastaa wengi wakiitwa kuzitumikia timu zao za taifa katika mechi za kirafiki na zile za kuwania kufuzu michuano mbalimbali ambazo zipo kwenye kalenda ya FIFA jambo lililotikisa kidogo kikosi cha Simba inayojiandaa kuivaa Al Ahly Oktoba 20, mwaka huu uwanja wa Benjamin Mkapa katika mechi ya AFL.

Hadi sasa mastaa wa Simba wa tano kutoka kikosi cha kwanza, hawapo kambini Msimbazi wakiwa kwenye timu zao za taifa ambapo beki Henock Inonga, yupo nchini New Zealand na kikosi cha DR Congo, kiungo Clatous Chama yupo Misri na Zambia na Kibu Denis, Mzamiru Yassin na Ally Salim walioitwa Taifa Stars watapaa kesho kwenda nchini Saudi Arabia.

Inonga leo atakuwa sehemu ya kikosi cha DR Congo kitakachocheza mechi ya kirafiki na New Zealand ugenini lakini pia timu yake hiyo itakuwa na mchezo mwingine nchini Angola dhidi ya timu ya taifa hilo, Oktoba 17, siku tatu kabla ya Simba kuvaana na Ahly.

Hali iko hivyo hivyo kwa Chama aliye nchini Misri na timu yake ya taifa la Zambia baada ya mechi ya jana ya kirafiki, na timu hiyo itacheza tena nchini Zambia Oktoba 17, dhidi ya Uganda, siku tatu kabla ya Simba kuivaa Ahly.

Pia Kibu, Mzamiru na Ally walio taifa Stars, watacheza mechi ya kirafiki na Sudan mchezo utakaopigwa nchini Saudi Arabia Oktoba 15 na baada ya hapo timu hiyo itarejea nchini.

Kwa maana hiyo huenda mastaa hao watano ambao ni muhimili wa Simba wakaingia kambini kwa Wanamsimbazi hao, siku moja au mbili kabla ya mechi kutokana na safari za kutoka walipo kuja Dar es Salaam zitakavyokuwa.

Hata hivyo uongozi wa Simba umeyaomba mashirikisho ya soka nchini wanakotoka wachezaji hao, kuwaparuhusu kujiunga na klabu zao lakini bado hawajajibiwa.

Wakati huo huo VIONGOZI wameomba kwa Mashirikisho ya Timu ZAO wawape muda waweze kurudi kambini mapema kujumuika na wenzao ili kujiandaa na mechi ya Ahly lakini hadi sasa, hawajapata jibu la jumla.

Wakati huo huo, mpinzani wa Simba, Al Ahly aliomba na kuruhusiwa kubaki na wachezaji wake muhimu walioitwa kwenye timu zao za taifa ikiwemo kiungo Mmali, Aliou Dieng na mshambuliaji kutoka Afrika Kusini Percy Tau, na wote wapo kambini wajiweka tayari kuivaa Simba
 
Nafikiri Kuna uzembe kwenye uongozi wa Simba, wenzao Al ahly wakiomba mapema wachezaji wao wasijiunge timu ya Taifa wakati Simba wametumia maombi baada ya wachezaji kuitwa. Kama wangetoa maombi mapema uwezekano wa kutoitwa ni mkubwa.
Sijui habari ya Al Ahly kuomba wachezaji wao wasijiunge na timu za taofa umezitolea wapi mkuu. Nanukuu moja ya vyanzo vya taarifa " international players’ position on the Tanzania trip?

A: Al-Ahly officials have completed the procedures for international players to join the Red Giants before Tanzania’s trip to face Simba, as it was decided that Tunisian Ali Maaloul will travel from Japan to Tanzania after the end of his participation with his country’s national team in a friendly match to be held in Japan on October 17, while Mali Dieng will return to Cairo after his participation with His country’s national team in a friendly match against Saudi Arabia in Riyadh.

As for Percy Tau, he apologized for his presence with the South African national team in the Côte d’Ivoire friendly due to personal circumstances and traveled with Al-Ahly from Cairo, while Al-Ahly’s international players for the first and Olympic teams will return to Cairo after the end of their participation in the international matches of the agenda, to travel with Al-Ahly on the 18th of this month to Tanzania on board. A private plane for the upcoming meeting.

Mwisho wa kunukuu
Source: How is Al-Ahly preparing to face Simba in the opening kickoff of the African League? - CN
 
Sasa hivi kuna vyanzo tofauti vingine vinatoa habari za ukweli vingine vinapotosha, inawezekana chanzo changu so sahihi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom