FIFA wakataa ombi la Zelensky la Kuhutubia kabla ya Fainali za Kombe la Dunia ili kuhamasisha Amani

Mocumentary

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
769
1,959
Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA) linadaiwa kuwa limekataa ombi la Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kutaka kuhutubia kabla ya mchezo wa Fainali ya Kombe la Dunia kati ya Argentina na Ufaransa siku ya Jumapili kuchezwa, ichezwe video yake uwanjani hapo ili kuhamasisha amani.

Zelensky inadaiwa kuwa aliomba hilo huku akitaka kuonekana katika video hiyo akitoa ujumbe wa kuhamasisha amani wakati huu Ukraine ikiwa katika vita kati yake na Urusi.

Taarifa za ndani kutoka MailSports zinaeleza kuwa FIFA wamemkatalia Rais huyo wa Ukraine ombi hilo pasipo kumpa sababu za kukataa.

Rais Volodymyr Zelensky amekuwa akihutubia kwa njia mbalimbali katika matukio makubwa Duniani kuhusu amani ikiwa inatafsiriwa kama ishara ya kuomba ushirikiano katika vita dhidi ya Urusi.

Milliard Ayo
 
Zelensk alikaa kimya wakati wakongomani huko wakiuwawa

Alikaa kimya sudani kukiwa kumechafuka

Alikaa kimya wakati iraq na nchi nyinginezo zikivamiwa

Nchi yake anataka ipewe special attention ili iweje?
Ulitaka afanye nini ?
 
Wanaanzaga Kukataa hivyo hivyo lakini mwisho wanakubali. Subiri uone Kama Kesho hatahutubia.
 
Back
Top Bottom