Field Marshal Mohamed Tantawi afukuzwa Misri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Field Marshal Mohamed Tantawi afukuzwa Misri

Discussion in 'International Forum' started by MVUMBUZI, Aug 12, 2012.

 1. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #1
  Aug 12, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,768
  Likes Received: 487
  Trophy Points: 180
  Kamanda na mkuu wa Majeshi ya Misri aliyesimamia vuguvugu la mabadiliko yaliyomwondoa madarakani Hosni Mubarak wa Misri Field Marshal Mohamed Husein Tantawi amefukuzwa kazi na rais mpya wa Misri Mohamed Morsi leo.

  Ikumbukwe huyu Tantawi aliunda na kuongoza baraza la kijeshi lililosimamia kuondolewa na hatimaye kumfungulia mashataka rais wa zamani wa Misri na mpaka anafukuzwa alikuwa waziri wa Ulinzi wa Misri.

  Tantawi amefukuzwa pamoja na mkuu wa majeshi wa nchi hiyo ;Cheo cha waziri wa Ulinzi amekishilikia kwa kipindi kisichozidi mwezi mmoja.

  Tusubiri nini baada ya hii fukuza fukuza kwani tunajua wazi Morsi kamsaliti mtu ambaye alimtengenezea mazingira ya kuwa rais.
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,058
  Likes Received: 883
  Trophy Points: 280
  Huyu hafiki hata december kwenye huo urais maana ana kiherehere sana
   
 3. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #3
  Aug 12, 2012
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,559
  Likes Received: 339
  Trophy Points: 180
  Makubwa haya.Labda kuna sababu za msingi!
   
 4. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #4
  Aug 12, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 6,835
  Likes Received: 3,959
  Trophy Points: 280
  Always huwa nashindwa kuelewa nchi za kiarabu na wanaofanana nao (Somalis, etc.) huwa zinataka nini hasa! Tawala na watu wao sijui wanatakaga nini.
   
 5. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #5
  Aug 12, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,353
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  hajamfukuza ila amestaafisha kwa manufaa ya umma
   
 6. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #6
  Aug 12, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,094
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Mursi amefanya jambo la maana. Maana mapinduzi ya umma yalikuwa yametekwa na jeshi. Wanaoota kuwa Mursi hafiki Desemba hawajui kitu kuhusu wamisri na upiganiaji haki wao. Wanaodhani hivyo ni wachovu wa kitanzania ambao hawawezi hata kumwajibisha mwekezaji mmoja anapowadhulumu na kuwadhalilisha. Shame on these human sheep.
   
 7. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #7
  Aug 12, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,658
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Waarabu sio watu..hebu ona hata sasa wameungana kabisa wanasomba silaha kwenda Syria kuua waarabu wenzao ili marekani apate faida..wajinga sana mm tangu wamsaliti Ghadafi sina haja nao...
   
 8. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #8
  Aug 12, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,569
  Likes Received: 21,077
  Trophy Points: 280

  muwe mnasoma kufuatilia mambo kiundani
  kabla ya kukurupuka kuongea
  huzijui siasa za Misri
  ungejua usingeropoka
   
 9. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #9
  Aug 12, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,571
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  The inside of politics huwezi kuielewa mpaka uwe inside...
   
 10. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #10
  Aug 12, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,569
  Likes Received: 21,077
  Trophy Points: 280

  Usipotoshe watu
  Misri ni watu ndio walio leta mapinduzi
  na huyu Tantawi alikuwa kikwazio cha 'mapinduzi ya kweli'
  ameweka sheria na kujipachika kwenye serikali kinyume na matakwa ya watu
  Wananchi wanataka 'mapinduzi kamili' na sio 'mapinduzi ya kuwa chini ya jeshi la Tantawi'
   
 11. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #11
  Aug 12, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,571
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Military Chief of Staff Sami Enan naye kastaafishwa!!!
   
 12. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #12
  Aug 12, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,768
  Likes Received: 487
  Trophy Points: 180
  Angeachwa kwenye uwaziri wa Ulinzi afurahie matunda ya mapinduzi. Mkuu huyu hajastaafishwa amepigwa chini bila hiari yake. yetu macho kuhusu mustakabali wa urais wa Morsi ambaye kwa mtazamo wangu anakwenda kasi mno
   
 13. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #13
  Aug 12, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,353
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  sababu kubwa iliyochangia ni yale mauaji ya askari kule sinai na kama waziri wa ulinzi kazi ilikuwa imemshinda
   
 14. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #14
  Aug 12, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,768
  Likes Received: 487
  Trophy Points: 180
  Tukubali tusikubali kama jeshi lingemuunga mkono Mubarak dhidi ya nguvu ya umma mapinduzi yasingekuwa rahisi namna hiyo. Hebu oneni Syria ambako jeshi lime side na serikali na kuyafanya mapinduzi kuwa magumu. lazima tuweze ku-appreciate mchango uliofanywa na jeshi la Misri kuleta mapinduzi kwa kutoshambulia badala yake kuwaunga mkono waanzilishi wa mapinduzi. Ilikuwa lazima jeshi lisimamie smooth transition of power la sivyo ingekuwa anarchy na ktk huo mchakato naweza kusema ndipo pepo la tamaa ya madaraka likaingia ila mwanzo walianza vema.
   
 15. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #15
  Aug 12, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,394
  Likes Received: 1,550
  Trophy Points: 280
  Nchi za kiislam ni matatizo Matupu! Sijui waislam wenzangu wana matatizo gani!
  Nchi nyingi zina vita, penye amani kama Tanzania, choko choko zimeanza...Dah!!
   
 16. steveachi

  steveachi JF-Expert Member

  #16
  Aug 12, 2012
  Joined: Nov 7, 2011
  Messages: 3,658
  Likes Received: 1,164
  Trophy Points: 280
  hv hichi cheo cha field marshal kinatolewa wapi,manake kwa upeo wng mdogo nasikia alikuwa nacho fidel castro tu na yeye cjui alipewa na nani na huyu tantawi naye kapewa na nani,hapo ndo nitajua kama kweli ni field marshal au kuruta
   
 17. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #17
  Aug 12, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,569
  Likes Received: 21,077
  Trophy Points: 280

  jifunze tena siasa za Misri
  Tantawi ni lazima afukuzwe
  'mapinduzi hayana kusubiri'
   
 18. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #18
  Aug 12, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,768
  Likes Received: 487
  Trophy Points: 180
  Mimi siyo mtaalam wa siasa za Misri lakini ni mfuatiliaji wa siasa za middle East sana. Hata kama mapinduzi hayana kusubiri kwa mtazamo wangu namwona huyu jamaa wa Muslim Brotherhood akielekea kuasisi siasa za imani kali; Timu ya akina Tantawi walikuwa moderate kiimani na mtazamo wa kimagharibi zaidi ambao Morsi hautaki.
   
 19. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #19
  Aug 12, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,569
  Likes Received: 21,077
  Trophy Points: 280

  msimamo kali ndo upi?
  nini maana ya mapinduzi?
  si wananchi waamue wanachotaka?
   
 20. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #20
  Aug 13, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,415
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Mnafiki hajifichi !
   
Loading...