Field Marshal Mohamed Tantawi afukuzwa Misri

Field Marshal Mohamed Tantawi afukuzwa Misri

Mimi siyo mtaalam wa siasa za Misri lakini ni mfuatiliaji wa siasa za middle East sana. Hata kama mapinduzi hayana kusubiri kwa mtazamo wangu namwona huyu jamaa wa Muslim Brotherhood akielekea kuasisi siasa za imani kali; Timu ya akina Tantawi walikuwa moderate kiimani na mtazamo wa kimagharibi zaidi ambao Morsi hautaki.

Imani kali ni ipi, kaongeza nguzo ya sita ?
 
Wananchi wa Misri HAWAHITAJI WANAJESHI WAWEPO KWENYE SERIKALI MPYA;Rais Morsi kafuata matakwa ya wananchi waliompigia kura na JESHI LILIKUWA KIKWAZO KWAKE KUTAWALA!
 
Always huwa nashindwa kuelewa nchi za kiarabu na wanaofanana nao (Somalis, etc.) huwa zinataka nini hasa! Tawala na watu wao sijui wanatakaga nini.

Uwe unatumia akili kabla hujakurupuka na kuropoka upuuzi wako. Mtu mzima hutumia busara badala ya kucheua pumba kama unavyofanya wewe. Jiheshimu.
 
Ikumbukwe kamba jeshi lilikuwa linatamani na kwa hakika lilionyesha dalili za kubaki madarakani baada ya Mubarak. Tantawi ndiye kinara wa harakati hizo. Si sahihi kabisa kulinganisha hali ilivyokuwa Misri na nchi nyingine kama Syria. Hakuna nchi mbili zilizo sawa kabisa. Kila moja aina mazingira tofauti, majirani tofauti, marafiki tofauti, silaha tofauti, historia tofauti, utamaduni tofauti, ....... need I list everything?
Tusipende siasa za kishabiki bila kuangalia kwa undani historia na mazingira ya mahali. Tutakuwa tunalopoka tu.
 
Kuna watu wanapenda kuingiza udini ktk kila jambo kwa namna ambayo inatia kichefuchefu. Mtu ambaye amesoma historia na kufuatilia matukio mbalimbali ya shari na vita hapa duniani atagundua mara moja kwamba watu wa dini zote wamehusika katika uovu usiomithilika na mauaji ya kustaajabisha. Tuache ushabiki wenye kuleta shari.
 
Let him rest at home...kwani hatujui kila kitu kina kiasi? Kwanini afikiri yeye ndio Egypt?
 
nimeangalia movie ya black gold, nikahisi mungu aliweka mafuta halafu akayawekea laana, kila mwenye nayo basi ni mwendo wa kuchapana ndio kinachowakumba waarabu, wamalawi wakiyapata na sisi tutaingia humohumo
 
Huyo Tantawi na wenzie walitaka jeshi liwe na nafasi ya kipekee na ya kikatiba katika utawala wa Misri, hata rais asiwe na udhibiti na jeshi. Kabla ya uchaguzi waliweka kipengele kinachosema rais mpya asingekuwa amiri jeshi mkuu, hii yote kwa lengo la kumfanya awe rais aliyeko chini ya jeshi. Mabadiliko haya ni lazima ili kujenga demokrasi.
 
Waarabu sio watu..hebu ona hata sasa wameungana kabisa wanasomba silaha kwenda Syria kuua waarabu wenzao ili marekani apate faida..wajinga sana mm tangu wamsaliti Ghadafi sina haja nao...
Mwafrika naye vipi hayuko mbali na warabu mana kazi zenu ku-uwana tu...Tazama huko Congo mfano mdogo sana...Rwanda na uganda wanafanya nini, sa kabla ya kucheka warabu ungenza kujicheka wewe :biggrin1:
 
Nchi za kiislam ni matatizo Matupu! Sijui waislam wenzangu wana matatizo gani!
Nchi nyingi zina vita, penye amani kama Tanzania, choko choko zimeanza...Dah!!

Naomba utafakari kwa makini kama Ivory coast, Liberia, Ethopia, Msumbiji, Angola, Uganda, Rwanda, Burundi, Zaire........ nk. ni nchi za Kiislam??? Halafu tafakari pia waanzilishi wa vita wafuatao kama nao ni waislam, Hitler, Joseph Kony, Charles Toylor, Jonas Savimbi, Slobodan Milosovich, Jean Kambanda, Jonas Savimbi, Foday Sankoh, Jean-Bedel Bokassa hawa wameweka rekodi duniani ya Mauaji ya kikatili. Fanya utafiti kama ni waislam kama unachoamini ni sahihi.
 
Mkuu nakushauri tu pitia upya historia ya Misri katika medani ya siasa uliachoandika hapa naona unamtetea Mohamed Tantawi na kupotosha kuwa yeye ndio alimtoa Hosn Mubaraka, wakati raia wa Misri ndio wamefanya mapinduzi hayo...hivi hunafahamu kuwa Mohamed Tantawi na wanajeshi wenzake ndio walivunja bunge lilichaguliwa na wananchi, na walivyoona Rais Morsi anakalibia kushinda kiti cha urais wakabadilisha katiba kupunguza madaraka ya Rais na jeshi kuwa na madaraka makubwa ya kiutawala.
 
Naomba utafakari kwa makini kama Ivory coast, Liberia, Ethopia, Msumbiji, Angola, Uganda, Rwanda, Burundi, Zaire........ nk. ni nchi za Kiislam??? Halafu tafakari pia waanzilishi wa vita wafuatao kama nao ni waislam, Hitler, Joseph Kony, Charles Toylor, Jonas Savimbi, Slobodan Milosovich, Jean Kambanda, Jonas Savimbi, Foday Sankoh, Jean-Bedel Bokassa hawa wameweka rekodi duniani ya Mauaji ya kikatili. Fanya utafiti kama ni waislam kama unachoamini ni sahihi.

Mkuu kamili,
Tatizo watu wanakurupuka bila data wala facts zozote wanaongozwa na hisia na chuki.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kamili,
Tatizo watu wanakurupuka bila data wala facts zozote wanaongozwa na hisia na chuki.
Mkuu hakuna chuki
Libya,Somalia, Iraq, Syria, Afghanstan, Pakistan, Palestina, Misri, Tunisia, sio nchi za kiislam?
 
Waarabu sio watu..hebu ona hata sasa wameungana kabisa wanasomba silaha kwenda Syria kuua waarabu wenzao ili marekani apate faida..wajinga sana mm tangu wamsaliti Ghadafi sina haja nao...

Ukitukana waarabu unakosea kwani tatizo ni uongozi mbovu. Viongozi viherehere na wasioona mbali. wanashindwa kung'amua mbinu za kibeberu za Marekani na waitifaki wake.
 
Back
Top Bottom