Uchaguzi 2020 Felister Njau: Tulikamata mabegi matano ya kura za CCM ktk Uchaguzi Mkuu 2020

Mbunge wa viti maalumu, Felister Njau amepewa siku saba kuthibitisha kauli yake aliyoitoa bungeni kuhusu kukamatwa kwa mabegi matano ya kura wakati wa uchaguzi mkuu 2020.

Felister ametakiwa kupeleka uthibitisho huo na naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson leo Jumatano Februari 3, 2021 kutokana na kauli yake hiyo aliyoitoa bungeni wakati akichangia hotuba ya Rais John Magufuli ya ufunguzi wa Bunge la 12.

My Take
CCM wamepita kwa wizi wa kura, Covid19 wamepita kwa wizi wa vifungu vya katiba. Ngoma droo
Huo ni mpango maalum uliopangwa kishamba ili kuwapumbaza watanzania na kuwaaminisha kuwa bunge hili ni sawa na lililopita lenye wapinzani.

Hiyo ni kete ya Ndugayi kuwahadaa watanzania kuwa bunge lipo active kumbe ni sawa na kikao cha wana ccm tu
 
Mbunge wa viti maalumu, Felister Njau amepewa siku saba kuthibitisha kauli yake aliyoitoa bungeni kuhusu kukamatwa kwa mabegi matano ya kura wakati wa uchaguzi mkuu 2020.

Felister ametakiwa kupeleka uthibitisho huo na naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson leo Jumatano Februari 3, 2021 kutokana na kauli yake hiyo aliyoitoa bungeni wakati akichangia hotuba ya Rais John Magufuli ya ufunguzi wa Bunge la 12.

My Take
CCM wamepita kwa wizi wa kura, Covid19 wamepita kwa wizi wa vifungu vya katiba. Ngoma droo
Huyo anautaka ubunge au hautaki?

Hii ndiyo iliyomfanya mkuu 'Britanicca' kuwa na mashaka na Mbowe, au kuna jingine?
 
Wameambiana kuwa wakianzisha hizo episode ndio watapata mvuto. Kumbe tumeshawapotezea muda tu.
Mkuu 'tindo', nilikuwazia nilipobandika maoni yangu hapo juu kabla ya kukusoma hapa.

"'Episodes"' za namna hii zinaweza kufikirisha kidogo hasa kama zitaendelea hivi hivi hadi hao tunaodhani ni 'sponsors' wa hawa wabunge wakiamua kuchoka nazo na kuamua kuwafanya hawa wabunge kama walivyokuwa wakiwafanyia akina Mbowe, Sugu, Henche na wengine.

Hali ikifikia huko, nitaamini kwamba CHADEMA kweli wanajua kuchanga karata zao.

Sasa hapo sijui akina Halima na wenzie tutawaangalia vipi sisi tulio/tunao apa juu ya usaliti wao!

Hivi umekwishalifikiri hili kwa upana wake?

'Anyway', bado siamini kuwa CHADEMA kama chama wanaouwezo wa kusuka mpango kama huo.

Hivi yule kichaa 'Dugai' ikifika huko ataanza kuwafukuza na kutumia sababu ya kutotambuliwa na chama chao? Kuwa walifukuzwa? Kwa huyo kufanya uamzi kama huo sishangai, kwa sababu ni kichaa.
 
Swali:
01.Endapo ushahidi utawasilishwa, wapo tayari kuupokea?
02. Endapo wataupokea ushahidi huo, wapo tayari kuukubali, kuutoa ili jamii ijue na kushughulikia wahusika kisheria ili aliyeporwa haki yake aipate?

HOJA: Huu ni mkakati maalumu ili baadaye itangazwe ameshindwa kuwasilisha ushahidi na kuvunja hoja ya upinzani kuwa madai yao ya kura kuibiwa ni uzushi tu.
 
Polepole alishathibitisha hilo kwa kusema kuwa kura fake zilikuwa za CHADEMA.
 
Wabunge hawa wakiendelea hivi hakika bunge litarudishwa gizani.

Hakuna mwenye kifua cha kuyavumilia haya.

Watatishwa na pengine kupigwa; lakini wakiendela kukomalia haya, hata sisi tuliowabatiza hawa COVID-19 tutaanza kuona aibu.
 
Back
Top Bottom