feedback ya kikao na mkurya

feedback ya kikao na mkurya

nasikia makabila mengine yamepunguza na yanafanya kwa siri sana, ila wakurya wanafanya hadharani na wanadai ni uchafu.

Kumbe kile kidude kwa wenzetu ni uchafu. Kweli kule hata dhahabu mpaka leo yawezekana wanabadilishiwa kwa Shanga
 
kwenye msafara wa mamba kenge nao hawakosi. hivyo ww ndio kenge hapa. umesamehewa bure.

juu ya shingo yake kawekewa koroma. pole kwa yaliyokukuta.
please, be very careful unapongea nao. mi nilijifanya mshauri wa wanandoa fulani hivi, jamaa akaenda kumwambia mkewe kuwa nilimshauri A, B, C, D. Wacha ninuniwe na huyo mke na wao wakaendelea kula bata. nilikosa sana amani.
 
hulazimishwi kuamini. shida
ya baadhi ya watu huona kila mkasa ni story ya kutunga. hata hizo story
za shigongo zinatokana na matukio halisi ndani jamii. mfano, kuna
kitabu kinaitwa Rais Anampenda Mke wangu cha Shigongo. hivi hakuna
marais wanaowapenda wake za watu? use your brain!
ahsante, nadhan atakuwa ameelewa.
 
hii hapa!!

dai tena nyingine!!

kuria-cultural-music-december-2009.jpg
haiendani na kisa, tafadhali. weka picha hapo! teh teh teh
 
Kumbe kile kidude kwa
wenzetu ni uchafu. Kweli kule hata dhahabu mpaka leo yawezekana
wanabadilishiwa kwa Shanga

hata mimi nimeshangaa. basi kama ndio hivyo wachafu ni wengi mjin hapa.
 
Mjini umkamate binti naniii..Aisee hyo fgm labda wakurya waliopo vijijini,aftrol mtu ukishajua umuhm wake ht kwenu utakimbia kuikwepa
 
Nakushauri uhame hapo maana
kuanzia sasa wote mke na mume watakuwa wanakueleza matatizo yao kwa
sababu mke anakuamini kwa sababu umemueleza ukweli kuhusu hali ilivyo
hapo home kwake na pia mume atakususimulia kwasababu anaona uko
understanding ndio maana amekueleza kwa undani juu ya ndoa yake. In
short utakuwa kama sehemu ya kupunguzia stress zao kwani watakuwa
wanakuelezea matatizo yao kila wanapokuwa na tension/frastrution. Je
huyo kazi utaiweza? maana hapo inabidi ugeuke kuwa mshauri wa hiyo ndoa
bila kupenda. Kinachoweza kutokea

1. Ugomvi ukiwa mkubwa sana kiasi cha kuleta matatizo makubwa zaidi,
mume atakuona kama wewe ndio ulikuwa chanzo ingawa sio kweli. yeye ndio
chanzo cha matatizo yake, lkn siku zote binadamu hutafuta sababu ya
tatizo hata kama sio.
2. Huyo aleyeingilia ndoa pia ataambiwa kwamba wewe ndio umetoa hiyo
siri hivyo watendelea na mahusiano yao kwa siri lkn huyo msichana
atakuwa na donge na wewe kuasi ambacho ataona ananyang'anywa hilo buzi
lake kwa sababu ya wewe
3. Huwezi jua tofauti zao zitafikia wapi pengine hata kuumizana au
kutoana roho (siunajua akina Mushi siku hizi wako wengi. wapo wanaotumia
panga pia hasa wakurya). Hivyo all the time wewe ndio utakuwa reference
ya ugomvi wao.
4. Upeo wa huyo jamaa ni mdogo, ndio maana ameweza kufanya hicho
alichokifanya kwa style hiyo. wapo wengi wanao cheat lkn sio kwa namna
hiyo. Kwahiyo mtu wa namna hiyo anaweza kufanya mengine mengi ambayo
huwezi tegemea kama hilo la kuingiza demu mwingine ndani kwake. Hivyo
usiamini kirahisi kwamba matatizo yao yataisha na mambo yatakuwa poa,
maana anaweza kufanya vituko vingine pia. Hivyo wewe jiondoe kwenye list
ya kuja kuwa shahidi kwa lolote hapo baadae. Nakushauri, select
problems to deal with (lkn kama unaona hilo unaliweza basi endelea), pia
select firends to be with you, itakusaidia hapo baadae mbeleni maishani
mwako.
5.Endelea kuwashauri vyema kwa hayo matatizo yao, hata hivyo ulivyofanya
ni vyema na umewasaidia kujiweka sawa hasa jamaa aleyekuwa amejisahau
kiasi hicho. Lkn kuwasaidia kwako pia kusikuletee matatizo wewe. JARIBU
KUWA MAKINI NA HILO SWALA LAO.

Nakutakia siku njema.

ahsante mkuu Papii. nimekuelewa vizuri. hapa sio mahali salama kwangu ninafanya utaratibu.
 
Last edited by a moderator:
Pole hata hivyo wewe ni jasiri. Ukiweza hama kabla ya huyo mkewe kuja. Watakuwekea kinyongo.
 
Umefanya la maana kuamua
kuhama hapo. Hiyo ndoa ina mengi na wala mke kujua hautakuwa mwisho wa
mahusiano na mjita kama wameshazaa na anadai ndio chaguo lake.
Hama uwaachie sakata lao watatu watajua jinsi ya kulimaliza.
Gud luck!!!!!

mi nashangaa hivi inakuaje chaguo lake ameshindwa kumuoa lakini anaendelea kuwa naye tu.
 
Pole hata hivyo wewe ni jasiri. Ukiweza hama kabla ya huyo mkewe kuja. Watakuwekea kinyongo.

yaani nitakuwa adui wa watu watatu. maana mambo ya mapenzi atamsimulia hadi kimada wake.
 
DEMBA,
ulitaka kutoroka bure mdogowangu na ungefanya hivyo jamaa angezidi
jenga chuki dhidi yako. Lakini sasa si unaona ulivyomsaidia? kawa mdogo
ka-piriton!! Siku zote simamia kweli hata kama ni Chungu.
Hoja ya wakurya kutairi wanawake hii ni mbaya kuliko ubaya wenyewe,
madhara yake ni makubwa sana sana wanapaswa kubadilika mara moja, ndo
maana wengi wao (wakurya-ME) wanaoa makabila mengine
tofauti!!!!

hivi hizi ngo's mbona sinaishia mijini tu. yaan huko vijijini wanahitaji elimu sana. kuna mila zao nyigi tu si za kiungwana.
 
mi nashangaa hivi inakuaje chaguo lake ameshindwa kumuoa lakini anaendelea kuwa naye tu.

Anajifanya ana balance equation,wazazi waridhike kaoa wamtakaye na nafsi yake iridhike anavinjari na ampendaye! Kazi ipo hasa maana njia mbili zilimshinda fisi
 
nasikia makabila mengine yamepunguza na yanafanya kwa siri sana, ila wakurya wanafanya hadharani na wanadai ni uchafu.

Wakurya ni mambo hadharani yaani kila baada ya miaka 2 mida ya November na December wanatahiri, mfano mwaka jana 2012 walitahiri hivyo mwakani mida ya November to December 2014 wanatahiri tena, niliwahi kuwauliza baadhi wenye uelewa wanasema siku hizi wanatahiri ki-CCM kwa kuchanja kidogo ili angalau raia waone kwamba mtoto ametahiriwa
 
Anajifanya ana balance
equation,wazazi waridhike kaoa wamtakaye na nafsi yake iridhike
anavinjari na ampendaye! Kazi ipo hasa maana njia mbili zilimshinda
fisi

yaani ni ujinga ujinga tu.
 
kwanza kabisa naomba nitoe shukran zangu za dhati kwa wadau waliochukua muda wao na kunishaurii nini nifanye baada ya tukio la jana kwa kweli mlinipa ujasiri mkubwa. ahsanteni sana na mungu awabariki daima
kwa wale ambao mlinizodoa vile vile nawashukuru kwani kwa kiasi fulan mlinielimisha.
turudi kwenye mada
kikao kilifanyika kwenye majira ya sa mbili na jirani alikuja akiwa amepoa kabisa. aliniambia mengi ambayo yaliniacha mdomo wazi.
kumbe huyu kimada ndio chaguo lake na alishazaa naye ila wazazi wake walikataa asimuoe kwa sababu sio mkurya (ni mjita) na ni mchafu (hajatahiriwa) ndipo wakamtafutia huyo shost ambaye anasoma huko nairobi. kipindi hicho alikuwa binti mdogo wa sekondari. alipomaliza tu sekondari akamuoa na akatakiwa amuendeleze.
mimi nikamwambia kwamba ni kweli mimi nilimwambia lakini alishakuwa na taarifa na mimi nilifanya finishing tu.

ameniomba tubadilishe story lakini mimi nimekataa kujihusisha na mambo yao nimemwambia amalizane nalo yeye mwenyewe. na nimeamua kwamba nisiendelee kukaa hapa kwani anaweza kuwa na kinyongo.

hivi wakurya hii mila ya kutahiriwa bado wanaifanya haaa!!!!! sikujua kama bado inamashiko. mmh inabidi muache jameni.

cc Sista chakii 'Valentina' Asprin watu8 sungura1980 mwekundu Gefu IROKOS BADILI TABIA kuberwa miss wa kinyaru Nambe gfsonwin Ruttashobolwa Mentor atoto miss chagga Munkari Mapi jamiif amu King'ast Mamndenyi Heaven on Earth Baba Wawili 2012 Ennie Malafyale josephmasamaki bahatika SUZANE mwallu mshana jr charminglady matmafcha pipii ushiboy nameless girl Chimunguru Kiboko PetCash amu

Namalizia kukushauri hivi, siku nyingine usithubutu kuingilia ugomvi wa watu walio wahi kushea shuka au wanao endelea kushea shuka! hii milango ya vyumba vya baba na mama ikishafungwa huwa hatujui nini kinaendelea huko! ni vyema ukahama hapo maana nahisi kuna aibu inakunyemelea rafiki!
 
Back
Top Bottom