feedback ya kikao na mkurya

feedback ya kikao na mkurya

Nakushauri uhame hapo maana kuanzia sasa wote mke na mume watakuwa wanakueleza matatizo yao kwa sababu mke anakuamini kwa sababu umemueleza ukweli kuhusu hali ilivyo hapo home kwake na pia mume atakususimulia kwasababu anaona uko understanding ndio maana amekueleza kwa undani juu ya ndoa yake. In short utakuwa kama sehemu ya kupunguzia stress zao kwani watakuwa wanakuelezea matatizo yao kila wanapokuwa na tension/frastrution. Je huyo kazi utaiweza? maana hapo inabidi ugeuke kuwa mshauri wa hiyo ndoa bila kupenda. Kinachoweza kutokea

1. Ugomvi ukiwa mkubwa sana kiasi cha kuleta matatizo makubwa zaidi, mume atakuona kama wewe ndio ulikuwa chanzo ingawa sio kweli. yeye ndio chanzo cha matatizo yake, lkn siku zote binadamu hutafuta sababu ya tatizo hata kama sio.
2. Huyo aleyeingilia ndoa pia ataambiwa kwamba wewe ndio umetoa hiyo siri hivyo watendelea na mahusiano yao kwa siri lkn huyo msichana atakuwa na donge na wewe kuasi ambacho ataona ananyang'anywa hilo buzi lake kwa sababu ya wewe
3. Huwezi jua tofauti zao zitafikia wapi pengine hata kuumizana au kutoana roho (siunajua akina Mushi siku hizi wako wengi. wapo wanaotumia panga pia hasa wakurya). Hivyo all the time wewe ndio utakuwa reference ya ugomvi wao.
4. Upeo wa huyo jamaa ni mdogo, ndio maana ameweza kufanya hicho alichokifanya kwa style hiyo. wapo wengi wanao cheat lkn sio kwa namna hiyo. Kwahiyo mtu wa namna hiyo anaweza kufanya mengine mengi ambayo huwezi tegemea kama hilo la kuingiza demu mwingine ndani kwake. Hivyo usiamini kirahisi kwamba matatizo yao yataisha na mambo yatakuwa poa, maana anaweza kufanya vituko vingine pia. Hivyo wewe jiondoe kwenye list ya kuja kuwa shahidi kwa lolote hapo baadae. Nakushauri, select problems to deal with (lkn kama unaona hilo unaliweza basi endelea), pia select firends to be with you, itakusaidia hapo baadae mbeleni maishani mwako.
5.Endelea kuwashauri vyema kwa hayo matatizo yao, hata hivyo ulivyofanya ni vyema na umewasaidia kujiweka sawa hasa jamaa aleyekuwa amejisahau kiasi hicho. Lkn kuwasaidia kwako pia kusikuletee matatizo wewe. JARIBU KUWA MAKINI NA HILO SWALA LAO.

Nakutakia siku njema.
 
Duh behind any ugomvi kuna historia nyuma yake km unaangalia Jerry springer show vile
 
...next tym dont do that..
Umepona tu
 
ukiwa mjini hivi huwezi kujua hali ilvyo huko ukuryani yaani unaambiwa huko mwanamke asiye tahiriwa si mtu na wanadai anatengwa kabisa.

aisee! Kuna makabila mengne ni yakuskia tu kwa wenzio loh! Pole yao mana i cant imagine!
 
DEMBA, ulitaka kutoroka bure mdogowangu na ungefanya hivyo jamaa angezidi jenga chuki dhidi yako. Lakini sasa si unaona ulivyomsaidia? kawa mdogo ka-piriton!! Siku zote simamia kweli hata kama ni Chungu.
Hoja ya wakurya kutairi wanawake hii ni mbaya kuliko ubaya wenyewe, madhara yake ni makubwa sana sana wanapaswa kubadilika mara moja, ndo maana wengi wao (wakurya-ME) wanaoa makabila mengine tofauti!!!!
 
Huyo mkurya wako bana,
Kama ujasiri wa kupinga alichoamriwa na wazazi hakua nao kwa nini sasa anamkosea heshima mwanamke mwenzenu?
Kama ni kimada mambo yao ndo aje kufanyia mkewe anapolala.
Hivi ukilala sehemu ambayo unajua mwenzi wako alilala na mtu mwingine unajisikiaje?
 
kwanza kabisa naomba nitoe shukran zangu za dhati kwa wadau waliochukua muda wao na kunishaurii nini nifanye baada ya tukio la jana kwa kweli mlinipa ujasiri mkubwa. ahsanteni sana na mungu awabariki daima
kwa wale ambao mlinizodoa vile vile nawashukuru kwani kwa kiasi fulan mlinielimisha.
turudi kwenye mada
kikao kilifanyika kwenye majira ya sa mbili na jirani alikuja akiwa amepoa kabisa. aliniambia mengi ambayo yaliniacha mdomo wazi.
kumbe huyu kimada ndio chaguo lake na alishazaa naye ila wazazi wake walikataa asimuoe kwa sababu sio mkurya (ni mjita) na ni mchafu (hajatahiriwa) ndipo wakamtafutia huyo shost ambaye anasoma huko nairobi. kipindi hicho alikuwa binti mdogo wa sekondari. alipomaliza tu sekondari akamuoa na akatakiwa amuendeleze.
mimi nikamwambia kwamba ni kweli mimi nilimwambia lakini alishakuwa na taarifa na mimi nilifanya finishing tu.

ameniomba tubadilishe story lakini mimi nimekataa kujihusisha na mambo yao nimemwambia amalizane nalo yeye mwenyewe. na nimeamua kwamba nisiendelee kukaa hapa kwani anaweza kuwa na kinyongo.

hivi wakurya hii mila ya kutahiriwa bado wanaifanya haaa!!!!! sikujua kama bado inamashiko. mmh inabidi muache jameni.

cc Sista chakii 'Valentina' Asprin watu8 sungura1980 mwekundu Gefu IROKOS BADILI TABIA kuberwa miss wa kinyaru Nambe gfsonwin Ruttashobolwa Mentor atoto miss chagga Munkari Mapi jamiif amu King'ast Mamndenyi Heaven on Earth Baba Wawili 2012 Ennie Malafyale josephmasamaki bahatika SUZANE mwallu mshana jr charminglady matmafcha pipii ushiboy nameless girl Chimunguru Kiboko PetCash amu

Safi sana! Sasa ktokana na Kuwa umeamua kuhama hapo mahili emu nipm mandhari ya nyumba nihamie Mimi japo nisave ile pesa ya dalali!
 
Last edited by a moderator:
Nimesoma kisa kizima,nimekukubali kwa utungaji wa stor fupi fupi za uongo na umbea,kwa mtu anaefikiri stori yako haina mashko,wala sio ya kweli,ni kama stor za shigongo.hamia uwazi au ijumaa,unafaa sana kwa stori za uongo na stori za kubuni.
 
DEMBA ungebadilishana nae tu story bibie!

kwani uliogopa nini!

au uliogopa kuombwa utamu?
 
Last edited by a moderator:
Weka picha;

hii hapa!!

dai tena nyingine!!

kuria-cultural-music-december-2009.jpg
 
Daaah yeye keshazoea king'amuzi mke kila akipapasa anakuta kipara.....kweli chaguo lake.
Hii tamu la muhimu hama tu
Si unajuwa bila king'amuzi huwezi kuona chaneli hata ya bure
 
Nimesoma kisa
kizima,nimekukubali kwa utungaji wa stor fupi fupi za uongo na umbea,kwa
mtu anaefikiri stori yako haina mashko,wala sio ya kweli,ni kama stor
za shigongo.hamia uwazi au ijumaa,unafaa sana kwa stori za uongo na
stori za kubuni.

nawewe hebu kakojoe ulale huko. kila kitu mnadhan ni uwongo tu.
 
Ukiendelea kujihusisha na huyo mkuriya
utaishia kuwa mke wa tatu very soon....
 
Nimesoma kisa kizima,nimekukubali kwa utungaji wa stor fupi fupi za uongo na umbea,kwa mtu anaefikiri stori yako haina mashko,wala sio ya kweli,ni kama stor za shigongo.hamia uwazi au ijumaa,unafaa sana kwa stori za uongo na stori za kubuni.

Nyie ndo walewale,,,,
 
uamuzi wako sio mbaya

Ila pia pole zake huyo kaka, na pole kwa mkewe maana wote 3 wanakosa Penzi la dhati
 
Hayo ndo madhara ya kuingilia uhuru wa mtu na kumchagulia mtu wa kuishi nae,wazazi walikosea kwa hilo. Hiyo ya pili elimu zaidi inahitajika kwa wanaoendekeza desturi hizo
 
Nimesoma kisa
kizima,nimekukubali kwa utungaji wa stor fupi fupi za uongo na umbea,kwa
mtu anaefikiri stori yako haina mashko,wala sio ya kweli,ni kama stor
za shigongo.hamia uwazi au ijumaa,unafaa sana kwa stori za uongo na
stori za kubuni.

kwenye msafara wa mamba kenge nao hawakosi. hivyo ww ndio kenge hapa. umesamehewa bure.
 
Nimesoma kisa kizima,nimekukubali kwa utungaji wa stor fupi fupi za uongo na umbea,kwa mtu anaefikiri stori yako haina mashko,wala sio ya kweli,ni kama stor za shigongo.hamia uwazi au ijumaa,unafaa sana kwa stori za uongo na stori za kubuni.

hulazimishwi kuamini. shida ya baadhi ya watu huona kila mkasa ni story ya kutunga. hata hizo story za shigongo zinatokana na matukio halisi ndani jamii. mfano, kuna kitabu kinaitwa Rais Anampenda Mke wangu cha Shigongo. hivi hakuna marais wanaowapenda wake za watu? use your brain!
 
Back
Top Bottom