Fedha za Radar Kurudishwa: Mgogoro kati ya BAE, TZ na UK

Inavyoonyesha BAE system wamesema pesa watazipelekwa kwa NGO (charity organisation); nimemsikia Membe akifura kwa hili analalamika kuwa inaonekana hatuaminiwi. Yeye ataka pesa zirudishwe serikalini moja kwa moja; lakni wao wamegoma watazipa charities mbalimbali za hapa TZ:dance:
 
Lakini na ho Waingereza wamezidi. inakuwaje mwizi anaamua kurudisha alichooiba kwa mtu anayemtaka yeye? halafu wanatundisha utawala bora?! Hata kama tuliwapa sisi pesa kwa nini walizipokea kama kweli wanaona sisi hatuna utawala bora? Just as bad.....
 
Afadhali hizi hela wapewe NGO zinazofanya kazi nchini. Kuwapa serikali ni sawa na kumkamata mwizi aliyekuibia kisha baada ya kuchukua hela zako ukampa tena hela zile zile alizokuibia.Kama zikirudishwa serikalini tutajuaje kama kweli hazitaibwa tena? Serikali ya ccm haiaminiki!
 
Membe na serikali ya ccm wanashangaza sana kwani walishasema hakukuwa na wizi wowote kwenye ununuzi wa rada. Sasa hizi hela wanahamu nazo za nini? Kwa nini tangu mwanzo hawakuwawajibisha wale wizi waliotufikisha hapa?
 
BBC wametangaza kuwa ile kampuni ya Uingereza iliyoiuzia Tanzania RADA katika mazingira ya kutatanisha na ikaamuriwa na mahakama ya Uingereza iilipe Tanzania faini ya Dola za Kimarekani milioni 50 imeamua KUTOLIPA faini hiyo SERIKALINI ila kwa taasisi za kijamii. Na imeunda bodi itakayoamua taasisi zitakazopewa fedha hizo.

Serikali ya JK imekuja juu ikidai pesa hizo ipewe - kwa mujibu wa Waziri Membe ambae amehojiwa na BBC juu ya maamuzi hayo ya BAE.
 
Serikali ya Tanzania imepinga vikali uamuzi wa kampuni ya silaha ya Uingereza –BAE Systems wa kulipa fidia ya Paundi milioni 29.5 za Uingereza kwa Tanzania kupitia asasi isiyo ya kiserikali badala ya kulipa fedha hizo moja kwa moja serikalini kufuatia kukamilika kwa kesi ya rushwa ya ununuzi wa Rada.

Mwanzoni mwa miaka ya 2000, Kampuni ya BAE System iliiuzia Tanzanai Rada kwa gharama ya Paundi milioni 41 za Ungereza wakati gharama halisi ilikuwa Paundi milioni 12.

Akitangaza msimamo wa serikali leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe amesema, uamuzi huu unaenda kinyume na msimamo wa serikali yetu uliotaka fidia hiyo irejeshwe serikalini.“Fedha hizo ziliibwa kutoka serikalini na hazina budi kurejeshwa serikalini,” amesema.

Tamko la Serikali limekuja miezi sita baada ya uamuzi uliotolewa na Jaji Bean wa mahakama ya Southwark ya Uingereza Desemba 21,2010 kutoa uamuzi kuwa BAE kulipa Paundi milioni 29.5 kwa wananchi wa Tanzania.

Jaji Bean alitoa uamuzi huo baada ya kutorishika na na maelezo ya makubaliano ya Ofisi ya Makosa makubwa ya jinai ya Uingereza SFO na BAE.
Kwa mujibu wa Waziri Membe, kampuni ya BAE system badala ya kulipa fedha hizo moja kwa moja kwa wananchi wa Tanzania, imeamua kuunda jopo litakalojumuisha watu kutoka ndani mwake kuishauri jinsi itakavyotumia fedha hizo kupitia kwa asasi isiyo ya kiserikali ya uingereza na sio kwa serikali ya Tanzania.

“Msemaji wa BAE amenukuliwa na Ubalozi wa tanzania nchini Uingereza akisema kampuni yake inaongozwa na sera ya kutoa misaada ya kihisani kwa asasi zisizo za kiserikali tu. Kwa msingi wa sera hiyo, kampuni hiyo haitaweza kulipa fidia hiyo moja kwa moja kwa serikali ya Tanzania,” amesema.

Waziri Membe amesema kuwa uamuzi hu wa BAE unalengo la makusudi kuonyesha sura ya kutokuamini mpango wa pamoja wa Serikali za Tanzania na Uingereza ulioelezea jinsi fedha hizo zitakavyotumika.

“Serikali ya Tanzania ilikusudia kutumia fedha hizo kununua jumla ya vitabu milioni 4.4 kwa ajili ya shule za msingi, vitabu vya miongozo ya mitaala 192,000 kwa ajili ya masomo 12 katiak shule 16,000, kununua madawati 200,000 kwenye shule zilizo na upungufu wa madawati na kujenga nyumba 1,196 za walimu katika wilaya zote nchini, kujenga vyoo 2,900’ amesema.

“BAE wanajaribu kujikosha mbele ya asasi mbalimbali zisizo za kiserikali za Uingereza baada ya kukosolewa sana kwa kashfa ya rushwa na kutoka sasa kuonekana kwamba inawajali zaidi Watanzania kukliko serikali yetu,” ameseam.
Waziri Membe ameeleza kuwa kampuni hiyo silaha ikikaidi kutoa fedha hizo moja kwa moja kwa serikali ya Tanzania, hakuna asasi isiyo ya Kiserikali ya Uingereza itakayopewa fedah hizo na kuruhusiwa kuja nchini.

Imeandikwa na Joseph Ishengoma
MAELEZO, DAR ES SALAAM

Wana Jf hili jambo kwanza niwashukuru sana waingereza lakini nina jambo ambalo ninataka kuli register hapa Jf kwa ajili kumbukumbu.

Nina Mashaka makubwa na Dhamira ya NYOKA WA MDIMU,huyu Jamaa watanzania Tuwe makini na Pesa zetu ana Matukio mawili aliyasimamia matokea Pesa hazikufika kwa walengwa,Tukio la kwanza ni Fedha ambazo CCM walipewa Na Kiongozi wa LIBYA Gadafi CCM walipata msaada wa Usd 3m jamaa akafikisha 1.5m pia Gadafi ameisamehe serekali bilioni 36,ambazo zimewekwa benki ya TIB kwa ajili ya Kusaida sekta ya KILIMO jamaa kaenda kumbana NONI na baadhi ya Viongozi akiwemo Mwanasheria Mkuu wa serekali akisema maagizo ya BOSS pesa apewe Mohamed Dewji eti alete Pembejeo za Kilimo mzee WEREMA akasema anataka maandishi Jamaa kaingia Mtini.

Tukio Jingine Membe alipokea dola 150,000 toka Balozi wa IRAN kusaidia CCM jamaa hajazifikisha Mpaka leo Balozi wa IRAN amefatilia kutaka kujua Msaada wake umefika ama hapana imeibua Mgogoro,Wana JF ushiriki wa membe ktk pesa zetu hizi unanipa mashaka makubwa sana Tuwe makini huyu jamaa anatafuta Pesa za URAIS.

Nafahamu atakuja MBOPO(Mwambene) hapa kuleta ubishi na kutetea ajira yake sitashangaa atakuja SANGARA(Mwameta) sitashangaa,ila niwaonye Mbopo ukileta kiherehere chako ktk maslahi ya Nchi yetu nitakulipua jinsi jamaa alivotumia nafasi yake kukupati Confermation hapo wizarani baada ya Naibu katibu Mkuu kuugua.
 
Mtihani kwa Mh. Membe:

BAE Systems fine: it won't be easy to pay Tanzania

Despite the Serious Fraud Office's investigation of BAE going on for years and a plea bargain being agreed back in February, there is no mechanism in place to pay the reparations to Tanzania.

BAE walked out of court this morning £750,000 poorer.

The headline sum in BAE's plea bargain with the Serious Fraud Office may be £30m, however the only money the company is legally obliged to pay is a £500,000 fine and costs of £250,000 as ordered by Mr Justice Bean.

Both are in relation to one charge of failing to keep accounting records relating to the sale of a $40m (£28m) air traffic control system to Tanzania.

The balance of the £30m agreed with the SFO is to be paid in reparations to "the people of Tanzania" by BAE.

After the sentencing, Richard Alderman, the director of the Serious Fraud Office (SFO), said: "I expect BAE to honour the agreement. I expect the company to pay it as quickly as possible."

But despite the investigation going for years and the plea bargain being agreed back in February, BAE has yet to put in place a mechanism to pay the money.

Three possibilities immediately arise.
  1. Firstly that the money is handed over to the government of Tanzania, a route thought to be preferred by the SFO;
  2. secondly that BAE grants the money directly to charities in Tanzania;
  3. thirdly that an independent party, possibly the World Bank, is used as an intermediary to distribute the money.
However each solution carries potential problems.

The Tanzanian government could refuse to accept payment from BAE. Taking cash from BAE in connection with the £40m air traffic control deal it brokered could be seen locally as a tacit admission of involvement in what the judge described as "shady activity".

Nick Hildyard of campaigning group Corner House said: "The tragedy is the government of Tanzania may not even accept the money, as to do so could be seen to be admitting its part in the affair."

Giving money to local charities could turn reparation into little more than a PR exercise for BAE Systems. No process has been put in place to facilitate the third avenue.

A spokesperson for BAE said the company was actively looking at how it would pay the £29.3m reparation to Tanzania. It said no formula or timetable had been set.
Source: Judge questions SFO evidence in BAE case - Telegraph

BAE fined in Tanzania defence contract case

21 December 2010
Today at Southwark Crown Court BAE Systems Plc was fined £500,000 after admitting it had failed to keep adequate accounting records in relation to a defence contract for the supply of an air traffic control system to the Government of Tanzania.

This outcome follows a settlement by BAE as part of a global agreement it reached earlier this year with the Serious Fraud Office and the US Department of Justice concerning contracts in a number of countries. The settlement with the SFO relates to the Tanzania contract whereby BAE agreed to pay an ex-gratia payment for the benefit of the people of Tanzania of £30 million less any fine imposed by the Crown Court.
Additionally, BAE was ordered to pay £225,000 costs to the SFO.

SFO Director Richard Alderman said, "I am delighted that the Judge stressed the seriousness of BAE's actions and that he recognised that the true victims were the people of Tanzania".

The prosecution case opened at Southwark Crown Court on 20 December 2010 before Mr Justice Bean.
Documents relating to the proceedings are now published on the SFO website. These are (a) the prosecution Note for Opening, (b) the Settlement Agreement and Basis of Plea and (c) the Charge

The Judgment can be seen on Judges, Tribunals and Magistrates | Judgments | R -v- BAE Systems PLC - sentencing remarks
 
Hapa tunaipenda nchi au tunajadili kwa ushabiki tu naamini tukiipenda nchi twaweza kubaliana na wazo la fedha hizi zije serikalini na CAG asimamie matumizi yake lakini ikipewa NGO ya Uingereza almost 45 to 60% zitatumika Kama administrative cost . Tuache kumjadili msemaji tuone mantiki ili pamoja tutoe wazo muafaka Tuache ushabiki Wa mtu na vyama pls
 
Mvua Gamba umeleta habari nzito hapa Hebu lete vielezo tumpe Dr awalipue hawa Kama huna nawe utakuwa mzandiki Maana kumtungia mtu ni dhambi kubwa haya Nasubiri ....
 
See my comments below
QUOTE=MVUA GAMBA;1982963]Wana Jf hili jambo kwanza niwashukuru sana waingereza lakini nina jambo ambalo ninataka kuli register hapa Jf kwa ajili kumbukumbu.

Nina Mashaka makubwa na Dhamira ya NYOKA WA MDIMU,huyu Jamaa watanzania Tuwe makini na Pesa zetu ana Matukio mawili aliyasimamia matokea Pesa hazikufika kwa walengwa,Tukio la kwanza ni Fedha ambazo CCM walipewa Na Kiongozi wa LIBYA Gadafi CCM walipata msaada wa Usd 3m jamaa akafikisha 1.5m pia Gadafi ameisamehe serekali bilioni 36,ambazo zimewekwa benki ya TIB kwa ajili ya Kusaida sekta ya KILIMO jamaa kaenda kumbana NONI na baadhi ya Viongozi akiwemo Mwanasheria Mkuu wa serekali akisema maagizo ya BOSS pesa apewe Mohamed Dewji eti alete Pembejeo za Kilimo mzee WEREMA akasema anataka maandishi Jamaa kaingia Mtini.

Tukio Jingine Membe alipokea dola 150,000 toka Balozi wa IRAN kusaidia CCM jamaa hajazifikisha Mpaka leo Balozi wa IRAN amefatilia kutaka kujua Msaada wake umefika ama hapana imeibua Mgogoro,Wana JF ushiriki wa membe ktk pesa zetu hizi unanipa mashaka makubwa sana Tuwe makini huyu jamaa anatafuta Pesa za URAIS.

Nafahamu atakuja MBOPO(Mwambene) hapa kuleta ubishi na kutetea ajira yake sitashangaa atakuja SANGARA(Mwameta) sitashangaa,ila niwaonye Mbopo ukileta kiherehere chako ktk maslahi ya Nchi yetu nitakulipua jinsi jamaa alivotumia nafasi yake kukupati Confermation hapo wizarani baada ya Naibu katibu Mkuu kuugua.[/QUOTE]
 
Yes, Leo Membe mkuu wangu kaumbuka sana na ushauri wake kwamba hizo fedha ni za serikali ya Tanzania wakati madai haya yakitolewa serikali ilikana kutokuwepo na wizi wowote..

Sasa kama imebainika kulikuwa na wizi huko UK, iweje sisi tuingie kudai hizo fedha bila kuwa na ushahidi kama walioutaka mwanzo kwamba wizi ulitokea?..Je sii jambo la busara kwa serikali yetu kufikia maamuzi kwanza kuwepo wizi wa fedha za umma kisha ndio mnaweka madai kuonyesha jinsi mlivyoibiwa..

Hakika tunaonekana wajinga sana kuweka madai hali sisi wenyewe tunasema makubaliano yalikuwa halali na hakuna jambo lililofanyika kinyume cha sheria, sasa tunadai hizi fedha kwa mpango gani?
 
  • Thanks
Reactions: 911
Mimi ningekuwa serikali ya Uingereza ningewambia tutawapa fedha pale mtakapo wawajibisha wahusika wa huu wizi. Maana inaelekea kama vile BAE walijipa rushwa wenyewe! Wezi wetu tumewakumbatia huku ela tunazitaka. Hatuoni kwamba tungewashughulikia tungepata ela mara mbili. Tukikusanya za kina Chenge and company si tungekuwa matajiri. Why should this government be trusted!
 
Hii ni aibu sana kwa serikali kulilia pesa ya BAE, wajue kuwa pesa ile si change kwani makubaliano ya awali yalikuwa ni kuuziana radar ya GBP 12m kwa GBP 41m. BAE wamefanya jambo bora sana kuinyima hazina pesa hizo, kama mpango wa kujenga madarasa ulikuwa ni bora zaidi kwa nini serikali hii hii iliweka kipaumbele kwenye kununua radar?, je na zile pesa walizotaka kuwalipa dowans nazo je?, mradi wa vitambulisho pia?, inaonesha ni jinsi gani walivyochanganyikiwa na pesa hii ambayo kiukweli si change bali ni humanitarian aid iliyotakiwa kutolewa kwa watanzania ili kuua shauri la rushwa lilikokuwa linaiandama BAE. Tena BAE wanatakiwa kutoa pesa hizo kwa asasi za kiraia za UK ambazo zipo well regulated na kufanya mambo yao transparency ikiwemo ku-Publish statements of financial activities and Trustees annual reports, filing annual returns to the Charity Commission. Kitu ambacho kitakuwa kinaeleza kila penny ilivyotumika badala ya kuwakabidhi Serikali wakalipie madeni ya mishahara na posho zao za semina elekezi. Kama Membe atakataa Asasi hizi kuja kufanya kazi Tanzania basi tutashauri uanzishwe mfuko wa kusomeshea watanzania wasio na uwezo nje ya Tanzania ambao mwananchi ataomba kupitia British Council ambayo itamuunganisha na asasi iliyokabidhiwa pesa hizo na akiwa na vigezo anapewa scholarship kuliko kuwakabidhi watu wanaodai change wakati hakuna mtu hata mmoja aliyefikishwa mahakamani kwa kulisababishia taifa hasara ya GBP 29 m!

Sasa ndio napata majibu taratiibu kwanini nchi yetu ni masikini... Kumbe hawa viongozi wetu vilazaaa
 
Zile fedha ni mali yetu, hivyo ni lazima waturudishie cash, siye ndio tutakaopanga tuzitumie vipi fedha hizo sio wao, kwa kuwa ni fedha zetu sio msaada. Wasubiri wakitupa misaada yao ndio watupangie namna ya kutumia sio watupangie tutumie vipi fedha zetu. Kama tukizifanyia ufisadi, sawa tu maana ni fedha zetu.
 
Hii imekaaje?

Serikali ya Tanzania ndio iliozemebea mchakato wa mkataba wa rada na kufumbia macho hali ya wazi wazi ya kifisadi kuwepo miongoni mwa wahusika wake.

SFO ya UK ndio yenyewe ikaibua wasi wasi wa hali ya rushwa kuhusiana na ununuzi wa Rada na ikashauri, kupitia waziri wake Clare Short, kuwa Tanzania isinunue hiyo rada. Bado serikali ya Tanzania ikapuuza ushauri huo.

Baada ya kesi imeonekana kwa kiasi kikubwa kuwa rushwa ilikuwepo.

Ni Vipi Membe aone kuwa Serikali hiyo hiyo zembe ya Tanzania inastahili fidia kutoka UK. Hiyo Fidia ni hisani tu ambayo UK inafanya kwa huruma ya nchi masikini kama TZ.

Hili tamko la waziri Membe ni muendelezo wa ubabe na vitisho ambao Membe huko nyuma amekuwa na kawaida ya kuulekeza kwa serikali za nje.

Mifano ni:
(a) Ubabe na vitisho vya kutaka UN iombe msamaha kwa Serikakli ya Tz kuhusiana na utafiti uilofanywa na wataalamu wa UN kuwa kuna uwezekano watu wachache ndani JWTZ wanahusika kwenye kupitisha silaha nchi jirani.

(b) Pia alipotokea mkichaa mmoja wa ubalozi wa nje kumtemea mate askari polisi, Membe alienda mbali hadi kutishia mahusiano ya Serikali ya Tz na nchi husika akidai kuwa kitendo hicho kimedhalilisha Serikali na umma mzima wa wa-Tanzania.

Membe alishindwa kuona kuwa kile kitendo ni cha mtu binafsi kutema mate na kuwa hakiwakilishi mtizamo wa Serikali au raia wa nchi anakotaka mtu huyo.

Diplomasia iko wapi kwenye Wizara ya nje? Ni kama vile Wizara hiyo inahitaji somo kuhusu fani hiyo hiyo ya diplomasia ambayo ndio wanatakiwa kuisimamia.

... Jamani hii kweli imekaaje?
 
Source: Habari Leo

SERIKALI imepinga, kulaani na kutoa msimamo juu ya uamuzi wa Kampuni ya Ulinzi ya Uingereza (BAE Systems) wa kuipa asasi isiyo ya kiserikali ya nchi hiyo pauni za Uingereza milioni 29.5 (Sh bilioni 74) ili kufanya shughuli za hisani nchini badala ya kuilipa Tanzania moja kwa moja kama ilivyoamriwa na Mahakama nchini humo.

Akitoa msimamo huo Dar es Salaam asubuhi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, alisema kwa kuwa kinachofanywa na BAE ni udhalilishaji na matusi yanayolenga kushawishi walimwengu na jamii ya Uingereza kuwa Serikali ya Tanzania si aminifu kwa raia wake na kuwa inaongoza kwa misingi ya rushwa, huku ikijua kuwa sio kweli, asasi itakayotumwa kuja kutumia fedha hizo kwa mgongo wa kutoa hisani haitaruhusiwa kuingia.

Waziri Membe alisema ni afadhali Tanzania ikajua imepoteza, kuliko kukubali kufanyiwa
udhalilishaji wa wazi kama huo na kampuni ambayo kisheria inapaswa kuilipa Serikali kiasi hicho cha fedha, bila masharti.

Alisema, hilo ndilo lililoipasa BAE kwa sababu ilifanya wizi wa makusudi kwa kuiongezea Serikali kiasi kikubwa cha fedha katika gharama ya mauzo ya rada, jambo lililothibitisha kuwepo kwa tofauti kubwa ya bei; kati ya bei halisi na gharama ambazo Tanzania ilitozwa.

"Ubalozi wetu London ulituarifu juu ya uamuzi huo wa BAE jana (juzi) jioni na kutupa taarifa zaidi leo (jana) asubuhi.

Ni uamuzi wa kufedhehesha, kusikitisha na usiokubalika. BAE wanataka kuvuta simanzi za walimwengu kuwa wako sahihi, lakini ukweli unabaki kuwa walituibia na wanapaswa kurejesha walichokikwapua mahali walipokitoa.

"Wanatapatapa na kutaka kujisafisha kwa kuichafua Serikali yetu, hilo halikubaliki na kwa kuwaonesha msimamo wetu kuwa hatuhitaji na wala hatujawahi kuhitaji msaada wao (BAE), hatutairuhusu hiyo asasi yao iingie nchini kufanya hizo hisani zao … walikuwa wapi kutusaidia miaka yote waoneshe kuwathamini na kuwajali Watanzania sasa hivi, kwa kupitia fedha za Watanzania wenyewe! Huu ni mchezo mbaya, tumeugundua na hatutauruhusu," Membe alisema.

Kadhalika, alisema uamuzi wa BAE umepuuza mpango wa pamoja wa Serikali za Tanzania na Uingereza ulioeleza namna fedha hizo zitakavyotumika kuendeleza sekta ya elimu nchini, kwa kununua vitabu vya kiada milioni 4.4 kwa ajili ya shule za msingi, vitabu vya miongozo ya mitaala 192,000 kwa ajili ya masomo 12 kwa shule 1,600 za msingi, kununua madawati
200,000 kwa shule zenye upungufu wa vifaa hivyo, kujenga nyumba 1,196 za walimu katika wilaya zote nchini, vyoo 2,900 na kukarabati madarasa na majengo mengine chakavu.

"BAE imepuuza ahadi ya serikali hizi mbili ya kusimamia matumizi ya fedha hizo za fidia na inataka kujisafisha kutokana na kuchafuka kwake kwa kutoa rushwa.

Inataka kuwaonesha Watanzania, kuwa inawapenda zaidi ya Serikali yao. Huu ni ubabaishaji na maneno mengi, ingewathamini Watanzania isingewatenda ilivyowatenda".

Kwa maelezo ya Membe, Tanzania ina uhusiano mzuri na Uingereza, hivyo BAE haipaswi kuuharibu kwa njia yoyote. Uamuzi ulioitaka kampuni hiyo ya ulinzi kuilipa Tanzania kiasi hicho cha fedha ulitolewa Desemba 21, mwaka jana na Jaji Bean wa Mahakama ya Southwark, Uingereza, baada ya kukamilika kwa kesi ya rushwa dhidi ya BAE.

Kesi hiyo ilifunguliwa na Ofisi ya Makosa Makubwa ya Jinai ya Uingereza (SFO) baada ya kukamilisha upelelezi wake, ambapo waendesha mashitaka wa ofisi hiyo na BAE walikubaliana kuimaliza nje ya mahakama kwa kampuni hiyo kukiri kosa la kutoweka sawa kumbukumbu za fedha na hesabu katika mchakato wa mauzo ya rada.

Vile vile, kumalizwa kwa kesi hiyo nje ya mahakama, kulitazamia BAE itekeleze kipengele muhimu cha makubaliano ya kuilipa Tanzania sehemu ya fidia hiyo, lakini cha kushangaza, kwa maelezo ya Waziri Membe, kampuni hiyo imekuja na mtindo usiokubalika wa kulipa kiasi
hicho, baada ya kunyamaza kwa miezi sita tangu kesi hiyo itolewe uamuzi.

Hata hivyo, katika kuthibitisha msimamo wao wa kukwepa kuilipa Serikali, Msemaji wa BAE alinukuliwa akisema wanafanya mambo yao kwa kutekeleza sera yao inayowataka watoe fedha kwa asasi zisizo za serikali tu na si vinginevyo.

Alisema, ili kutekeleza hilo, jopo la watu sita kutoka kampuni hiyo litaundwa ili kuishauri BAE jinsi ya kutekeleza suala hilo, ikiwa ni pamoja na kuainisha asasi zitakazopewa fedha hizo, kati ya nyingi zilizoomba, kwa ajili ya kuendesha shughuli za hisani nchini.

My take: Hivi BAE wanatudhalilisha au tunajidhalilisha?
Suala la rada lilipoongelewa na viongozi wa upinzani (Lipumba) serikali ya Tanzania chini ya Mh Mkapa akisaidiwa na mwanasheria Chenge na mawaziri wake walikana na kupuuza bila ya uchunguzi tena wakisisitiza hakuna hujuma.

Aliyekomalia ni mama mwingereza (Linda ?) hadi yeye kupoteza kazi yake kwa kile alichokisema kuonea huruma masikini walivyoporwa.

Watuhumiwa wa kesi wametoroka,wengine wakiwa chini ya ulinzi wa vyombo vya dola. Wapo duniani na kila tukiuliza tunaambiwa uchunguzi unaendelea. Waliopo nchini wameendelea kupeta tena na nyadhifa zao.

Kama hatukuweza kuzuia pesa kuibwa au kubaini tumeibiwa, kama hakuna aliyefikishwa mbele ya sheria, kama tulikana hakuna wizi, kama tumeshindwa kuwakamata wahalifu waliopo na waliotoroka, kwanini iwe udhalilishaji BAE wakisema serikali yetu ni corrupt na je huo si ukweli?
Hizo pesa tutazitumiaje vema kama hatukujua zilivyoibwa, na je si kweli hizi pesa zinawezatumika katika semina elekezi na sio kama alivyosema waziri Membe.

Tunajidhalilisha sisi wenyewe kwa kuanzia, na hapa BAE wana hoja. Tuangalie tulipojikwaa na sio tulipoanguakia.
 
tena hizo pesa wangehesabu maalbino wote, vilema na watoto yatima wazigawe kwao

hongera serikali ya uingereza kwa kushitukia udhaifu wa serikali tawala ya tanzania
 
Hizo pesa tutazitumiaje vema kama hatukujua zilivyoibwa, na je si kweli BAE hizi pesa zitatumika katika semina elekezi na sio kama alivyosema ewaziri Membe.

Tunajidhalilisha sisi wenyewe kwa kuanzia, na hapa BAE wana hoja. Tuanglelie tulipojikwaa na si tulipoanguakia.
Hapo kwenye nyekundu,ni kweli hii serikali inapenda raia wake?Hivi membe anajua anachotamka?kweli kwenye pesa wakati mwingine kunakufanya ujivue GAMBA kuonekana ni muungwana!Juzi mmepiga wananchi watano risasi huko Mara bado tu mnawapenda raia?
 
Hivi huyu membe mzima kweli, anataka kusema kuwa BAE walituonea na si kwamba mkapa na chenge ndiyo waliotuingiza mkenge. Yaani walioba pesa na kuchora deal wako huru, hizo hela zikilitwa watakula deal tena.

Nawaunga mkono BAE, madawati tununue wenyewe!
 
Back
Top Bottom