Fedha za Radar Kurudishwa: Mgogoro kati ya BAE, TZ na UK

Membe nadhani ana ugonjwa wa akili!

BAE iliingia Hazina na kuiba pesa? Kwa nini asimuulize Andrew Chenge na Benjamin Mkapa ni kitu gani walichofanya badala ya kubwatuka tu?

Mahakama ilitoa hukumu kuwa hizo pesa ilipwe serikali ya Tanzania moja kwa moja?

W.t.f Membe?
 
Mkuu Nguruvi3,

Anachoonyesha Membe ni kwamba Serikali haijali National Interest.Anaonyesha weakness kwa Dunia kwamba Judiciary System,Bunge,Wizara ya Mambo ya nje na Idara ya Ulinzi na Usalama imepwaya

Kuna ile skendo ya Hon'ble Chenge kuweka Hela kwenye account nje ambazo zlikuwa suspected kuwa ni mgawo wa Rada,Serikali imefanya nini.Wale wahusika serikali imewafanyia nini? Serikali haikujua kwanba imeibiwa hadi hapo Waingereza hao hao walipotumia chombo chao kubaini wizi ule,sisis wakati huo tulikuwa kikwazo kuzuia wizi huo kuwa Exposed. Bernard Membe sina mashaka na Elimu yake na hata uzoefu wake kazini,ila namuomba aache kufanya compromise na Taaluma yake at the Expense of Tanzanians

Bibi Clare Short alisimama kidete kipindi kila kututetea huku waziri wa mambo ya nje kipindi kile Mh.JAKAYA MRISHO KIKWETE akiwa kimya.Sasa nani aliyekuwa akisimamia maslahi ya watanzania?Membe aache kujifanya kuwa anawajali watanzania.Pia kulikuwa na suala la kujadili kuhusu Mikataba ya kimataifa ambalo hajaliweka wazi nikirudi hapa nitalijadili

Ni kweli nakubali hatua hii ya BAE haionyeshi Picha nzuri kwa kuwa Dignity and Intergrity as a Nation itakuwa imeshuka,ila sisis wenyewe akiwamao Membe at his Capacity ndiyo tuliozidi au kuwapa nafasi ya kutudhalilisha.Serikali inastahili Heshima ipi katika Hili?Au kwa sababu tuna Bendera,Majeshi na Rais anayepigiwa Saluti?Ni kwa jinsi Gani sisis tunaweka Vipaumbele vyetu katika national interest na kuviheshimu ili wenzetu pia waviheshimu hasa katika International politics?
 
Membe nadhani ana ugonjwa wa akili!

BAE iliingia Hazina na kuiba pesa? Kwa nini asimuulize Andrew Chenge na Benjamin Mkapa ni kitu gani walichofanya badala ya kubwatuka tu?

Mahakama ilitoa hukumu kuwa hizo pesa ilipwe serikali ya Tanzania moja kwa moja?

W.t.f Membe?


Huyu membe naye ni kichekesho....ndio maana waziri mzima ameenda kujenga nyumba viwanja vya jangwani ikavunjwa ....huyu eti ndio anataka kuwa rais wa nchi hii....mtu anayejenga nyumba bila kibali tena kwenye viwanja vya kuchezea michezo....
 
Mkuu Nguruvi3,

Anachoonyesha Membe ni kwamba Serikali haijali National Interest.Anaonyesha weakness kwa Dunia kwamba Judiciary System,Bunge,Wizara ya Mambo ya nje na Idara ya Ulinzi na Usalama imepwaya

Kuna ile skendo ya Hon'ble Chenge kuweka Hela kwenye account nje ambazo zlikuwa suspected kuwa ni mgawo wa Rada,Serikali imefanya nini.Wale wahusika serikali imewafanyia nini? Serikali haikujua kwanba imeibiwa hadi hapo Waingereza hao hao walipotumia chombo chao kubaini wizi ule,sisis wakati huo tulikuwa kikwazo kuzuia wizi huo kuwa Exposed. Bernard Membe sina mashaka na Elimu yake na hata uzoefu wake kazini,ila namuomba aache kufanya compromise na Taaluma yake at the Expense of Tanzanians

Bibi Clare Short alisimama kidete kipindi kila kututetea huku waziri wa mambo ya nje kipindi kile Mh.JAKAYA MRISHO KIKWETE akiwa kimya.Sasa nani aliyekuwa akisimamia maslahi ya watanzania?Membe aache kujifanya kuwa anawajali watanzania.Pia kulikuwa na suala la kujadili kuhusu Mikataba ya kimataifa ambalo hajaliweka wazi nikirudi hapa nitalijadili

Ni kweli nakubali hatua hii ya BAE haionyeshi Picha nzuri kwa kuwa Dignity and Intergrity as a Nation itakuwa imeshuka,ila sisis wenyewe akiwamao Membe at his Capacity ndiyo tuliozidi au kuwapa nafasi ya kutudhalilisha.Serikali inastahili Heshima ipi katika Hili?Au kwa sababu tuna Bendera,Majeshi na Rais anayepigiwa Saluti?Ni kwa jinsi Gani sisis tunaweka Vipaumbele vyetu katika national interest na kuviheshimu ili wenzetu pia waviheshimu hasa katika International politics?

Hapo kwenye RED: Membe anaweza kuwa na elimu nzuri lakini hakawa ajaelimika. Kwanza waliochota hizo fedha Hazina sio BAE bali ni maafisa wa Tanzania. Pili, waliotengeneza na kusaini mkataba wa mauzo ya RADAR ni maafisa wa Tanzania pamoja na Rais wao. Tatu, mama Clare Short alipopiga baragumu la kuukataa mradi wa RADAR hata akadiriki kwenda Chamwino - Dodoma kumweleza Rais wetu ubovu wa dili hilo la RADAR ni serikali yetu iliyomtolea nje. Nne, SFO ilipochukuwa jukumu la kuchunguza wizi ndani ya sakata la RADAR, maafisa wa Tanzania katika vitengo vya DCI, TAKUKURU, DPP na AG walitulia tuli kama vile hakuna jambo lolote baya linaloendelea. Isitoshe TAKUKURU ikamsafisha mmoja wa watuhumiwa katika sakata la RADAR.

Sasa hizi kelele za Membe kwamba fedha hizo zilipwe serikali ya Tanzania ni zanini wakati haina watuhumiwa wa wizi wa RADAR? Hata ripoti ya CAG haionjeshe wizi wowote wa fedha katika sakata hili.

Nashauri BAE iendelee na mpango wake wa kutoa fedha hizo kwa NGOs. Hachana na serikali ya Mafisadi.
 
BAE kweli wana makosa lakini sasa hta sisi tuna makosa tena makubwa sana......ongea ya membe huwa inaniacha hoi sana
 
BAE SYSTEM WASHENZI SANA, Naunga mkono hoja ya membe ya kuingiza ktk akaunti ya serikali fedha kutoka BAE.
 
Membe nadhani ana ugonjwa wa akili!

BAE iliingia Hazina na kuiba pesa? Kwa nini asimuulize Andrew Chenge na Benjamin Mkapa ni kitu gani walichofanya badala ya kubwatuka tu?

Mahakama ilitoa hukumu kuwa hizo pesa ilipwe serikali ya Tanzania moja kwa moja?

W.t.f Membe?

Mimi nadhani Mh Membe sio mtanzania,na kama ni mtanzania basi kakulia tuu
hapa bongo,na kama ni mtanzania basi sio mzalendo.
Ni ukweli usiopingika kuwa serekali ya Tanzania haipendi
wananchi wake.
Siku zote wananchi wamekuwa wakilalamika maisha kupanda
garama lakini yenyewe imekuwa kimya sababu tosha ya Dr Slaa kupanda
chati siku hadi siku na sasa ni rais wa mioyo ya watanzania walio wengi
kama Mh Membe haamini aende kwenye mikutano ya Dr Slaa amuulize mtu yeoyote
pick ramdomly atakwambia huyu ndiye alistahili kuongoza hii serekali.
Ninaunga mkono asimilia 1000% BAE kulipa fedha kupitia asasi zisizo-serekali (NGO)
bila wao kuingiza maluki wao
HILI NI ONYO KWA SEREKALI CORRUCPT
PIA ONYO KWA MH MEMBE.
WATANZANIA TUNAJUA KINACHOENDELEA.
VUENI MAGAMBA HAMTAKI,SASA MTAKOMA.
CHADEMA HOYEEEEEEEEEEEEE.
 
Ben;1983512]Anachoonyesha Membe ni kwamba Serikali haijali National Interest.Anaonyesha weakness kwa Dunia kwamba Judiciary System,Bunge,Wizara ya Mambo ya nje na Idara ya Ulinzi na Usalama imepwaya.Kuna ile skendo ya Hon'ble Chenge kuweka Hela kwenye account nje ambazo zlikuwa suspected kuwa ni mgawo wa Rada,Serikali imefanya nini.Wale wahusika serikali imewafanyia nini? Serikali haikujua kwanba imeibiwa hadi hapo Waingereza hao hao walipotumia chombo chao kubaini wizi ule,sisis wakati huo tulikuwa kikwazo kuzuia wizi huo kuwa Exposed. Bernard Membe sina mashaka na Elimu yake na hata uzoefu wake kazini,ila namuomba aache kufanya compromise na Taaluma yake at the Expense of Tanzanians.Bibi Clare Short alisimama kidete kipindi kila kututetea huku waziri wa mambo ya nje kipindi kile Mh.JAKAYA MRISHO KIKWETEakiwa kimya.Sasa nani aliyekuwa akisimamia maslahi ya watanzania?Membe aache kujifanya kuwa anawajali watanzania.Pia kulikuwa na suala la kujadili kuhusu Mikataba ya kimataifa ambalo hajaliweka wazi nikirudi hapa nitalijadili
wasp;1983611]Kwanza waliochota hizo fedha Hazina sio BAE bali ni maafisa wa Tanzania. Pili, waliotengeneza na kusaini mkataba wa mauzo ya RADAR ni maafisa wa Tanzania pamoja na Rais wao. Tatu, mama Clare Short alipopiga baragumu la kuukataa mradi wa RADAR hata akadiriki kwenda Chamwino - Dodoma kumweleza Rais wetu ubovu wa dili hilo la RADAR ni serikali yetu iliyomtolea nje. Nne, SFO ilipochukuwa jukumu la kuchunguza wizi ndani ya sakata la RADAR, maafisa wa Tanzania katika vitengo vya DCI, TAKUKURU, DPP na AG walitulia tuli kama vile hakuna jambo lolote baya linaloendelea. Isitoshe TAKUKURU ikamsafisha mmoja wa watuhumiwa katika sakata la RADAR.
Sasa hizi kelele za Membe kwamba fedha hizo zilipwe serikali ya Tanzania ni zanini wakati haina watuhumiwa wa wizi wa RADAR? Hata ripoti ya CAG haionjeshe wizi wowote wa fedha katika sakata hili
Kibanga Ampiga MKoloni;1983537]Kabla hizo azijarudi tafadhali tunaomba zile walizo lamba wakina chenge, idrisa na wahindio wao zirudishwe

Sakata la BAE Membe analijua vema tangu mwanzo hadi mwisho, alikuwa serikalini. Kwanini anakuwa mkali kwa wageni wezi na haongei neno hata moja kwa wenyeji 'waliovunja' hazina!!
Wasp Kasema ripoti ya CAG haionyeshi wizi wowote, sasa Membe atueleze tumeibiwa wapi na nanikwanza.
Kwanini hawa viongozi wanatudhalilisha namna hii kutufanya sisi ni mazezeta tu na tutameza kila uchafu tunaotupiwa! Kwanini hawaelewi TZ ya 2011 si ya 1947? Kama hawatawataja wezi wa ndani, ni afadhali BAE wazigawe wanavyojua, hatukuibiwa ati!
 
BAE wanajua wanachokifanya hapa....wanajua huu mzigo wa lawama sio wao 100% ndio maana wanaendeleza hii game. Wanajua kabisa kuna maofisa wa serikali ya tz walioshirikiana nao kwenye hii dili lakini hawajachukuliwa hatua! Yaani hapa ni mwendo wa "Mwaga Mboga nimwage Ugali"

Kuna mwenye hii hukumu ya kesi atuwekee hapa jamvini?
 
Mimi si mwanasheria na kwa muda wote nimekuwa nikisikia sakata la rada na chenge lakini nilikuwa sifahamu nani mshitaki; mshitakiwa nilikuwa namjua kuwa ni BAE systems. Jana nikasikiza BBC kwa makini sana.

BBC wanasema, pesa iliyolipwa BAE systems ni ya Tanzania, serikali ya kina Membe haikuchukua hatua yoyote licha ya kufahamu kuwa imeibiwa mabilioni ya pesa. Uingereze (please understand ni Uingereza siyo Tanzania) wakaishitaki kampuni ya BAE kwa kuwaibia Watanzania. Naambiwa Bi. Claire Shot ndiyo aliyeanzisha vuguvugu hilo la kimahakama. Kesi ikaendeshwa na hatimaye serikali ya Malkia ikashinda.

Kilichofuata hapo ni nani apewe hizo pesa. Mahakama ikaamuru pesa hizo zilipwe kwa watanzania kupitia mashirika ya hisani. Siyo kwa kina Membe.

Jana Membe alisikika na kuonekana akilia huku maudenda yakimtoka. Anadai pesa hizo ni za Tanzania (siyo za Watanzania kama mahakama inavyotafsiri). Membe anazitaka pesa kwenye serekali yake. Lazima zilipwe kwa serikali; kama zitalipwa kwa mashirika ya hisani, Membe aliapa hayatapata mlango wa kuingilia Tanzania. Hapo Membe akanichanganya kabisa. Sasa akizuia hayo mashirika na pesa zikashindwa kuja itakuwa hasara kwa nani? Kwa nini anadharau amri halali ya mahakama? Yeye kweli na serikali yake kama walikuwa na uchungu na hizo chapaa, kwa nini hawakufungua hiyo kesi wao? Kwa nini maofisa wa Tanzania walioshiriki kutekeleza wizi huo hawajachukuliwa hatua mpaka leo? Yaani kwa kuwa pesa imepatikana sasa Membe anataka kujifanya mtetezi wetu? Au udenda unamtoka kwamba sasa muda wa kununua ma V8 umewadia?

Membe huyuhuyu anaenda mbali zaidi kwa kulinganisha kesi hii na amri nyingine ya namna hiyo ambayo ilitolewa na pesa kulipwa kwa serikali ya marekani. Swali, kati ya Tanzania na Marekani, ni nchi gani, leo hii ikipigwa kura ya maoni itaonekana kuwa corrupt. Wazungu wanajua fika kuwa serikali ya Tanzania ni corrupt. Kiwango cha imani waliyonayo kwa serikali ya Marekani na kiwango walichonacho kwa serikali ya Tanzania ni tofauti kabisa.

Wazungu wanajua pesa hizi zikilipwa kwa serikali ya Tanzania, serikali ya kina Membe, hakika hazitawafikia walengwa.

Mimi nasema bora tusilipwe kabisa hizo pesa kuliko kulipwa serikali hii ya wala-rushwa kina Membe.
 
Hivi ni fedha zipi tunaidai Uingereza....zilitoka wapi?
Waziri Membe anaelewa anachokidai?
Ni vema kama hawezi kusema chanzo cha fedha hizo, basi na akae kimya milele.....:sick:
 
WAKATI kampuni ya BAE System ya Uingereza imekubali kurejesha nchini chenji ya pauni milioni 29.5, iliyozidishwa wakati wa ununuzi wa rada ya kijeshi ya Plessey Commander Fighter Control System. Lakini imeweka sharti kwamba lazima zipitie kwenye asasi moja ya nchini humo badala ya kuzifikisha mikononi mwa serikali ya Tanzania moja kwa moja kwa madai zitaangukia mikoni mwa mafisadi badala ya kuwanufaisha wananchi.

Membe, amesema kitendo cha kampuni hiyo ya Uingereza kukataa kurejesha fedha hizo mikononi mwa serikali, kina lengo la kutaka kuiaminisha dunia kwamba Tanzania haiaminiki na imekithiri kwa rushwa. Alisisitiza kuwa serikali haiko tayari kudhalilishwa kiasi hicho na kwamba haitaipokea asasi yoyote kutoka Uingereza itakayopewa kazi ya kuzileta fedha hizo endapo BAE itakaidi kuzirejesha mikononi mwa serikali. Akibainisha hatua zitakazochukuliwa kuhakikisha fedha hizo zinarejeshwa zilikotoka, Membe alisema suala hilo litafikishwa bungeni kupitia Kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalma ili itume ujumbe kwenda nchini Uingereza kuzungumzia suala hilo.


MATUMIZI

Fedha hizo ambazo ni zaidi ya sh bilioni 70 zitatumika kuboresha elimu ya msingi nchini ambapo vitabu milioni 4.4 vya kiada na vitabu 192,000 vya miongozi ya mitaala kwa ajili ya masomo 12 ya shule 16,000, vitanunuliwa. Aidha madawati 200,000 kwa shule zenye mahitaji zaidi, ujenzi wa nyumba 1196 za walimu kwa wilaya zote, ujenzi wa vyoo 2900; kukarabati madarasa, majengo chakavu na kuongeza vifaa vya kufundishia kwa shule husika.


Source: Tanzania Daima
 
Tunamshukuru aliyeleta hii. Safi sana. Kwa pamoja tunaungana nao kuwa waelekeze fedha hizo kwenye "charity fund" kwani sio juhudi yao iliyorejesha fedha hizo. Hawakuona sababu ya kuzitafuta kwa kuwa wanajua fika kuwa mhusika mkuu aliyekula hilo jasho la Wanzania angejulikana. Tunawapongeza Waingereza. Mungu aendelee kuongeza hazina yao.
 
BAE wanajua wanachokifanya hapa....wanajua huu mzigo wa lawama sio wao 100% ndio maana wanaendeleza hii game. Wanajua kabisa kuna maofisa wa serikali ya tz walioshirikiana nao kwenye hii dili lakini hawajachukuliwa hatua! Yaani hapa ni mwendo wa "Mwaga Mboga nimwage Ugali"

Kuna mwenye hii hukumu ya kesi atuwekee hapa jamvini?

Huo ndiyo ukweli
 
Nawaunga mkono BAE.ni heri wabaki nazo kuliko wawape hawa mafisadi.
Eti anadai serikali itaonekana ni ya rushwa?Kwani hizo pesa ziliingia vipi BAE kama si rushwa?
Huu ni muendelezo wa tamthilia ya "KUJIVUA GAMBA" wanataka waonekane ETI sasa hawapendi rushwa.
 
Ni aibu kwa serikali ya Tanzania kukomalia fedha kutoka BAE wakati imeshindwa kuwawajibisha watumishi wa serikali yake na wanasiasa wa Tanzania walioshirikiana na BAE kuwaibia watu wa Tanzania, katika mazingira hayo Membe anategemea nani ataiamini serikali ya CCM kusimamia fedha hizo ipasavyo?
Naunga mkono msimamo wa BAE na ninaomba serikali ya Uingereza isiyumbishwe na mbwembwe za akina Membe ili liwe fundisho. Wakikataa kuruhusu hizo asasi za kiraia pesa hiyo itunzwe hadi pale serikali inayowajibika itakapopatikana Tanzania na fedha hizo kurejeshwa.... Hongera BAE kwa msimamo mzuri, mmetuma ujumbe sahihi!
 
Kampuni ya ulinzi ya Ulaya, BAE Systems imesema italipa fidia ya sh. billion 67.29 zilizobaki katika manunuzi ya Rada. Jambo la kusikitisha ni kwamba kampuni hiyo imesema serikali ya Tanzania ikipewa pesa hizo zitatumika ndivyo sivyo, badala yake pesa hizo zitalipwa katika NGO's za Uingereza zinazota misaada Tanzania.

Kitendo hicho ni cha kuidhalilisha nchi na kinaonesha kwamba hatuwezi kupanga namna ya kutumia vema raslimali za nchi kulingana na mahitaji yetu.
 
Back
Top Bottom