Fedha za Radar Kurudishwa: Mgogoro kati ya BAE, TZ na UK

Utawarudishia wezi pesa??? kama wangekuwa makini pesa isingepotea. Tushukuru mungu kwa hawa waingereza Rada tunayo ya bure sasa
 
Mimi sijamuelewa Mh. Membe wala ''MAELEZO", maana kama hii ndiyo kutekeleza yale yaliyojiri ktk Semina Elekezi wiki iliyopita Dodoma naona serikali ya CCM inazidi kujichanganya! Nadhani serikali ya Uingereza inajua serikali ya Tanzania ingefuja 'hiyo chenji ya matumizi ya ununuzi wa RADAR' na hivyo kutafuta namna nyingine ya kutoa hiyo 'chenji'. Hili ni somo kwa serikali ya CCM kuwa makini na mikataba mibovu kwani hata 'haki' yetu sasa itapatikana kwa mbinde.

Pia serikali ya Uingereza inashauriwa kupunguza 'utoaji wa misaada' kwa nchi za kigeni, hivyo Mh. Membe anatakiwa awe mpole na kuomba busara toka kwa wabunge wa CHADEMA namna ya kukabili jambo hili ama sivyo tutakosa 'chenji' yetu na 'misaada' pia toka Uingereza.

Soma hapa shindikizo la ndani ya Uingereza kupunguza misaada kwa nchi zinazoendelea:
LiamFox415.jpg

Too much, too soon: Liam Fox said the deficit must be cut before aid can rise.

David Cameron faced a Tory revolt over international aid today after a letter written by Liam Fox was leaked.
The Defence Secretary warned the Prime Minister against creating a law that would commit Britain to spending millions of pounds on foreign aid.

And senior Tory backbenchers called on the Coalition to ditch plans to increase the aid budget while Britain is still in an economic crisis.
Senior Thatcherite MP John Redwood said the aid budget should not rise until Britain's debt mountain is reduced and aid programmes reviewed. "We need to get our deficit under control before we make the increases," he said.

In the leaked letter, Mr Fox challenged the Conservative manifesto commitment to set into law spending billions more, and argued that creating a statutory requirement will open the Government to future legal challenges.

Instead, he said the planned aid figure of 0.7 per cent of national income should be recognised simply as a target, along with a commitment to produce an annual report on whether it was being met.

The revolt threatens to undermine Tory attempts to "decontaminate" the party's brand and comes after MPs criticised the Government for committing £650 million for education in Pakistan while cutting school refurbishments in the UK.

Endelea kusoma ktk source: Tories back Liam Fox on defence spending law that could cost UK millions | News
 
safi sana membe endelea na msimamo huohuo, 2015 mkichakachua kura majeshi ya nato yatakuja kumfanya mshindi wa nec kama gbagbo, naona UK wanavua gamba maana hawa jamaa wamekuwa ni kikwazo kikubwa sana kwa demokrasia yetu
 
Naunga mkono uk-bae waipe oxfam pesa kusimamia maendeleo ya watz!hizo pesa zikienda serikalini ninavyojua zitaishia kwa wahindi na rushwa kidogo kwa waswahili!kwani ni nani alifichua uozo huo?amesahau mramba waziri wa ccm alisema tutake tusitake lazima radar inunuliwe tule hata majani.clear shot wa uk ndiye mwenye uchungu na watz!na kama membe anadai pesa ni zetu, jee ni watz wepi waliohusika kuziiba?
 
Viwavi jeshi hivyo! Vimeshambulia wakati wa masika, sasa vinagombania na vuli! Kweli kazi ipo.
 
Mimi niko pamoja sana na wadau wenzangu kuhusu swala lakulinda hela hizo na kujua zinatumikaje, ila wasiwasi wangu ni jinsi mataifa mbali mbali yanavyotufanya waafrica kuwa hatuna akili. Likitendewa serikali umetendewa wewe pia. Wazungu kama hamfaamu wanatufanya mandondocha wewe pamoja na serikali yenu. Sasa nini ninachopinga hapa nikutumia hela iliyoibwa ya watanzania kuwapa ngo ije itupangie nini chakufanya ilo ni tusi languoni na hatutakiwi kulikubali. Tukiruhusu hii hali kwakweli hatuna haja ya kuwa na serikali tanzania. Pesa iletwe serikalini then tuelezwe inatumikaje maana mchanganuo teyari uko wazi swala la kuibiwa na kuiba hao waingereza wenyewe wezi wa maliasili zetu. Kuwa na uhuru kamili nikitu kizuri sana , leo muingereza kasema hivyo mnamsupport kesho mmarekani, mfaransa mwisho nikama amna serikali. Acheni serekali ifanye jambo kwa wananchi wake kwani unadhani haiwezi wanaoweza ni hao waingereza? Tujiamini tutafanikiwa
 

Mimi nadhani Serikali ya Uingereza ingefanya jambo la busara sana iwapo hela za fidia kutoka ufisadi wa rada wangelipwsa wadai wa jumuia ya afrika ya mashariki iliyovunjika.

Ikumbukwe kwamba hela hizo ziliwekwa kwa Crown Agents ya Uingereza baada ya mgawo wa mali na madeni ya jumuia hiyo na baadaye kulipwa kwa serikali za nchi tatu za jumuia hiyo ikiwamo Tanzania.

Lakini serkali ya Tz haikufanya hivyo ilizitumia kwa matumizi mengine ikiwamo vita ya Uganda – inavyosemekana.

Baada ya miaka kadha bila aibu wakaja kulipa upupu tu, ikilinganishwa na wale wenzao wa Kenya na Uganda ambao walilipwa in full na kwa formula iliyopendekezwa na wataalamu.

Hivyo kwa kuwa kuna pesa ambazo serikali ya Uingereza inazishikilia kutokana na ufisadi uliohusisdha baadhi ya maofisa wa serikali ya hapa, basi ni busara sana, na haki kwa serikali hiyo ya Uingereza kuwalipa wastaafu hao wa EAC ya zamani.

Serikali ya Uingereza itakuwa imejikosha katika issue hiyo ya wastaafu kwani zile za awali waliwapa maharamia wa serikali ya TZ na wakazila.

Serikali ya Uingereza iombe orodha ya wastaafu hao na yenyewe ndiyo ifanye mahesabu ya mchakato na hatimaye kuwalipa wastaafu hao.
 
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa mh.benald membe amesema kuwa kampuni ya BAé system ya uingereza ni lazima ilipe pesa ambazo imeamliwa na mahakama 1 huko uingereza,Tanzania ndio inayopaswa kulipwa hizo bili0ni 29,amekwenda mbali na kudai kua zile pesa ni za watanzania na wao(BAé system)walizikwapua hivyo ni lazima wazilete,lakini BAé nao wamesema kuwa wao watatoa hzo pesa kwa mashrika wahisani ili ziwasaidie watz
my take:kama pesa zilikwapuliwa je watanzania hawakuhusika?Baé waliipataje kandaras?membe tueleze wakwapuaji,pili BAé hebu wawe wakweli charity ni leo?na kwanin leo?
 
Utawarudishia wezi pesa??? kama wangekuwa makini pesa isingepotea. Tushukuru mungu kwa hawa waingereza Rada tunayo ya bure sasa

Membe wacha unafiki! Mbona hamuwakabi wale walio shirikiana na BAE yaani akina Tanil Somaiya na wenzake? Maana hawa mapapa wanajulikana katika ushiriki wao katika ununuzi wa Mitambo hiyo rada, lakini leo Mzee Membe unakomaa kwamba BAE iilipe Serikali!

Ni heri kupitia huko kwenye mashirika ya kijamii maana wao wanatambua uaminifu wa viongozi wa serikali maana yalishirikiana nao kukwapua hizo $12million! Ufisadi mtupu!
 
Natamani kuchangia ila HASIRA ZIMENIJAA SANA. TANZANIA, TANZANIA, NAKULILIA TANZANIA.
 
Wadau nimemsikiliza waziri wetu wa maswala ya ughaibuni mh. Bernard Membe akihojiwa na BBC juu ya hatua ya BAE system kutaka pesa walizo amriwa na mahakama nchini Uingereza kuzilipa kwa mashirika ya kijamii.

Ukweli ni kwamba japo tuna haki ya kudai kupatiwa fedha hizo lakini serikali hii inanishangaza pale inapokuja juu kudai pesa ambazo awali walikataa kwamba hapakuwa na rushwa kwenye mchakato wa kununua rada, pili hata walipoambiwa wawafungulie kesi wahusika wote serikalini (Chenge na wenzake) katika mchakato wa rada waligoma,

Huu ujasiri wanautoa wapi Membe na Mkuu wa Kaya? Mimi nafikiri kwa kuonyesha kuwa walikerwa na hiyo rushwa basi wangeanzisha mchakato wa kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wale wote waliohusika na kisha kuwafilisi, hapo ndipo sasa serikali ingekuwa na jeuri ya kuwadai BAE kuwalipa.
 
Naunga mkono katika hili. Serikali ya CCM isipewe hata senti kwani pesa hizo zitafisidiwa tu. Haioni hata haya kuwadhulumu wazee wale?
 
Serikali ya Tanzania imepinga vikali uamuzi wa kampuni ya silaha ya Uingereza –BAE Systems wa kulipa fidia ya Paundi milioni 29.5 za Uingereza kwa Tanzania kupitia asasi isiyo ya kiserikali badala ya kulipa fedha hizo moja kwa moja serikalini kufuatia kukamilika kwa kesi ya rushwa ya ununuzi wa Rada.

Mwanzoni mwa miaka ya 2000, Kampuni ya BAE System iliiuzia Tanzanai Rada kwa gharama ya Paundi milioni 41 za Ungereza wakati gharama halisi ilikuwa Paundi milioni 12.

Akitangaza msimamo wa serikali leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe amesema, uamuzi huu unaenda kinyume na msimamo wa serikali yetu uliotaka fidia hiyo irejeshwe serikalini."Fedha hizo ziliibwa kutoka serikalini na hazina budi kurejeshwa serikalini," amesema.

Tamko la Serikali limekuja miezi sita baada ya uamuzi uliotolewa na Jaji Bean wa mahakama ya Southwark ya Uingereza Desemba 21,2010 kutoa uamuzi kuwa BAE kulipa Paundi milioni 29.5 kwa wananchi wa Tanzania.

Jaji Bean alitoa uamuzi huo baada ya kutorishika na na maelezo ya makubaliano ya Ofisi ya Makosa makubwa ya jinai ya Uingereza SFO na BAE.
Kwa mujibu wa Waziri Membe, kampuni ya BAE system badala ya kulipa fedha hizo moja kwa moja kwa wananchi wa Tanzania, imeamua kuunda jopo litakalojumuisha watu kutoka ndani mwake kuishauri jinsi itakavyotumia fedha hizo kupitia kwa asasi isiyo ya kiserikali ya uingereza na sio kwa serikali ya Tanzania.

"Msemaji wa BAE amenukuliwa na Ubalozi wa tanzania nchini Uingereza akisema kampuni yake inaongozwa na sera ya kutoa misaada ya kihisani kwa asasi zisizo za kiserikali tu. Kwa msingi wa sera hiyo, kampuni hiyo haitaweza kulipa fidia hiyo moja kwa moja kwa serikali ya Tanzania," amesema.

Waziri Membe amesema kuwa uamuzi hu wa BAE unalengo la makusudi kuonyesha sura ya kutokuamini mpango wa pamoja wa Serikali za Tanzania na Uingereza ulioelezea jinsi fedha hizo zitakavyotumika.

"Serikali ya Tanzania ilikusudia kutumia fedha hizo kununua jumla ya vitabu milioni 4.4 kwa ajili ya shule za msingi, vitabu vya miongozo ya mitaala 192,000 kwa ajili ya masomo 12 katiak shule 16,000, kununua madawati 200,000 kwenye shule zilizo na upungufu wa madawati na kujenga nyumba 1,196 za walimu katika wilaya zote nchini, kujenga vyoo 2,900' amesema.

"BAE wanajaribu kujikosha mbele ya asasi mbalimbali zisizo za kiserikali za Uingereza baada ya kukosolewa sana kwa kashfa ya rushwa na kutoka sasa kuonekana kwamba inawajali zaidi Watanzania kukliko serikali yetu," ameseam.
Waziri Membe ameeleza kuwa kampuni hiyo silaha ikikaidi kutoa fedha hizo moja kwa moja kwa serikali ya Tanzania, hakuna asasi isiyo ya Kiserikali ya Uingereza itakayopewa fedah hizo na kuruhusiwa kuja nchini.

Imeandikwa na Joseph Ishengoma
MAELEZO, DAR ES SALAAM

Napata shida kuyaamini maneno haya labda angelisema hizo Billioni 50 walipanga kununua Toyota VX 180 , marupurupu yangeliongezwa mara 200%, nyumba 50 za mawaziri zingelijengwa dodoma ikisha baada ya miaka 5 wakajiuzia wenyewe. Safari za JK zingeliongezeka mara 10, wangelitumia pesa hizo kuongeza posho ya wabunge, na mwisho kabisa zilizobakia wangelipeleka hazina zikalipie riba ya mikopo wanachukua kulipia mishahara ya wafanyakazi. Hapo ningelikubaliana nao :biggrin1:

Serikali ya Uingereza imefanya uamuzi sahihi kabisa kwani wanafahamu vizuri kinachoendelea ndani ya serikali ya CCM. Na serikali ya CCM wawe waangalifu jamaa wanalumbana sasa hivi kupunguza msaada overseas. Jana waziri wa ulinzi Uingereza bwana Liam Fox aliwataka serikali kupunguza misaada overseas. Ni vema wakaangalia kwa upana kauli zao kwani mwishoe isije kuwa tumekosa yote.
 
Wandugu,

Jioni ya leo nimemsikia Waziri Membe akihojiwa na Mtangazaji wa BBC kwenye kipindi cha Dira ya Dunia kuhusu suala la Rada lililohusisha Kampuni ya ABB ya kiingereza. Inavyoonekana, ABB wametekeleza agizo la mahakama la kuwataka kurejesha fedha ya wavuja jasho wa Tanzania iliyokwapuliwa kwa dili lililohusisha hata maafisa wa serikali. Hata hivyo, ABB itatoa hiyo fedha kupitia kwenye mashirika yasiyo ya kiserikali ya uingereza.

Kinachonishangaza ni namna Membe anavyopinga modality hiyo ya urejeshaji wa fedha. Anaonekana ana uchungu sana na fedha za watanzania. Je, kwa nini leo ndiyo anang'aka kiasi hicho! Wakati vyombo vya habari na vyama vya kisiasa vilipopiga kelele mwanzoni kabisa mwa dili hilo, mbona serikali iliwapuuza tena kwa maneno ya kejeli?!? Huo siyo unafiki kweli?? Ndugu zangu, tukumbuke kuwa yule Mama, waziri Clare Shot wa uingereza alijiuzuru hata uwaziri akipinga biashara/dili hiyo. Hivi ni waziri gani wa Tanzania aliyejiuzuru kuhusiana na suala hilo. Maoni ya Membe kwangu hayana maana yoyote.
 
Anadai kwamba hizo hela ziliibiwa serikalini. Ingekuwa bora zaidi kama wale walioziiba walikamatwa na kupelekwa mahakamani. Nakubaliana na ABB kutoa hizo fedha kwa mashirika yasiyo ya kiserikali kwa sababu ingepewa serikali zingepotelea mara nyingine tena kwenye mifuko ya wajanja.
 
Naunga mkono uk-bae waipe oxfam pesa kusimamia maendeleo ya watz!hizo pesa zikienda serikalini ninavyojua zitaishia kwa wahindi na rushwa kidogo kwa waswahili!kwani ni nani alifichua uozo huo?amesahau mramba waziri wa ccm alisema tutake tusitake lazima radar inunuliwe tule hata majani.clear shot wa uk ndiye mwenye uchungu na watz!na kama membe anadai pesa ni zetu, jee ni watz wepi waliohusika kuziiba?

Siku zote Mwizi BAE Systems umuofia Mwizi mwenzake Vigogo wa serikali ya TZ! Ndio maana wanataka wapewe vyama vya Kijamii ili mafisadi wa TZ wasije faidi mara mbili!
 
Bora tukose hizo fedha maana hawa jamaa wanajifanya sasa wanauchungu lakini ukweli ni kwamba hata hizo zikija zitaliwa tu.
Membe anasema atazuia taasisi za Uingereza zikipewa pesa hizo zisifanye shughuli zake hapa.. lo huo ni ujinga kwa viongozi wla kidhalimu na ufisadi kama hawa,i maana ni sawa na kuvuja kwa pakacha.
 
Kwa nini usijitahidi tu kueleweka ili watakaochangia waone tatizo ni nini. Yeye Membe anatoa msimamo wa serikali kwa sababu ukweli ni kwamba Serikali ndiyo iliyoibiwa fedha hizo na ndiyo inayostahili kurejeshewa fedha hizo. Uhalali au kukosa uhalali na fedha hizo hakutokani na jinsi serikali ilivyolishughulikia suala hili kwa sababu mpaka kabla ya uamuzi wa mahakama kuwatia hatiani BAE hauna ambaye angeweza kusema kwa uhakika kwamba kulikuwa na usanii. In any case waliofanya wizi huo walifanya in their personal capacities na hiyo haiwezi kuwa basis ya serikali kunyimwa fedha hizo. Hizi ni fedha ambazo serikali ilitapeliwa na anayetakiwa kurudishiwa ni yule aliyetapeliwa. Sasa cha ajabu hapo ni nini?
 
Back
Top Bottom