Uzalendo wa Kitanzania
JF-Expert Member
- Mar 8, 2020
- 2,207
- 4,702
Ndugu Watanzania kwa mazingira ya sasa Bima ya Afya ni hitaji la msingi kwa kila Mtanzania.
Hata hivyo changamoto iliyopo ni hali ngumu ya Kiuchumi kwa Watanzania walio wengi.
Naishauri Serikali iwasilishe muswada Bungeni wa Bima ya Afya kwa wote kupitia Tozo zitakazokusanywa kupitia malipo ya bili za maji nchi nzima.
Tozo zimethibitika kuwa na manufaa makubwa kwenye Ujenzi wa madarasa, vituo vya afya na barabara.
Napendekeza kiwango maalumu kikatwe mara moja kwa kila malipo yatakayofanyika kulipia huduma za maji na kisha kiasi kitakachokusanywa kiwasilishwe kwa mamlaka husika.
Kupitia mfumo huu Mteja atalipia huduma hii bila kuona au kuhisi mzigo wowote na wakati huo akiwezesha kupatikana huduma muhimu ya Bima ya Afya.
Ndugu zangu Watanzania hakuna linaloshindikana.
Bima ya afya kwa Watanzania wote inawezekana.
Kazi Iendelee.