1.Trio
Ofcoz, Trio ni sababu kubwa ya 5 ya Man U kufungwa tarehe 28. Hawa watu watatu wataigharimu sana Man U kuweza kuwadhibiti dakika zote 90 za mchezo. Nionavyo ni kwamba kwa sababu Pep anajua Man U ina ukuta mgumu sana katikati, atakachofanya ataanza kwa kushambulia tokea pembeni huku akiwa hana namba 9. Lionel Messi atacheza deep kama kiungo akiwa anatumika kama virtual centre forward hii itamfanya asiweze kukabwa na Vidic au Ferdinand. Wakati Messi atacheza kama kiungo, David Villa atakuwa anashambulia zaidi kwa kutokea kulia huku Pedro Rodriguez na Andres Iniesta watakuwa wanashambulia tokea kushoto. Hii itawalazimisha Nemanja Vidic na Rio Ferdinand kutanuka pembeni ili kuwasaidia mafullback Patrice Evra na kulia sina akika ataanza Fabio au Raphael, ila binafsi ninaamini akianza John Oshea itakuwa advantage kwa Man U maana yupo physic kuliko mapacha na pia anauwezo mkubwa wa kukaba na kuoverlap. Kutanuka kwa hawa centre defenders kutatoa mwanya kwa Xavi Hernandez na Andres Iniesta kusupply mipira kwa Lionel Messi. Mbinu pekee ambayo itawasaidia Man U kuweza kuwadhibiti hawa Trio ni kuanza kwa kutumia double holding midfielders, Darren Fletcher na Michael Carrick. Sina hakika sana na fitness ya Fletcher kwa ajili ya huo mpambano, maana japokuwa amecheza mechi ya mwishoni mwa msimu lakini bado fitness yake ina mashaka kidogo especially kwa sababu ya ugumu wa mechi yenyewe.