_ly
JF-Expert Member
- Mar 30, 2016
- 504
- 1,591
umeongea sahihi kabisa na ndo uhalisia ulivyo pia kitu kimoja cha kuongezea ni kuwa wakati tik tak inatawala hapakuwepo na mbinu ya kuizui kwa kipindi icho lkn saiz tik tak inaweza kuzuiliwa so tunaitaji kuji update...
Sent using Jamii Forums mobile app
Tikitaka sio suluhisho la matatizo ya barca kwa sasa. Tatizo la barca ni frontline butu na midfield isiyotengeneza nafasi za kutosha.
Kuna maana gani kua na position ya 81% kipindi chote cha kwanza bila kupata goli? Unaenjoy vipi hizi pasi kama upatikanaji wa magoli sio wa uhakika?
Once upon a time, we had xavi and iniesta. Hakika tulienjoy tikitaka sababu waliweza kuhold mpira, kupenya defence ngumu za wapinzani na kutengeneza nafasi za magoli kwa pasi za mwisho zilizokua world class.
Haikua ajabu kushinda goli sita mpaka nane wakati mwingine. Hapa tikitaka ilikua tamu haswa. Sababu tulikua na uhakika wa kupata goli muda wowote.
Mambo yamebadilika wakuu. Viungo tulionao hawafiki hata nusu ya uwezo wa xavi na iniesta. Nafasi zinatengenezwa chache, na uwezo wa ku unlock defence za wapinzani uko chini sana. Tunabaki kutegemea miujiza ya messi tu.
Kama mnakumbuka wakati MSN wanaitawala dunia, kulikua na mabadiliko ya namna tulivyocheza. Tulipiga pasi za harakaharaka na kushambulia kwa spidi from every angle. Tukaiteka dunia.
Nadhani kwa aina ya wachezaji tulionao, ndio mfumo unaotufaa zaidi. Kumuweka griezman apige tikitaka ni kama kumfundisha bata ustaarabu. Ni ngumu sana.
Kwa midfield ya akina rakitic, unaweza kupiga pasi buku jero ambazo hazina madhara kabisa kwa timu pinzani.
Ni either tupate watu sahihi watakao itendea haki tikitaka, au tukubali akina griezman wakimbie na mpira. Tofauti na hapo, tutapiga pasi kama dobi na bado ushindi tutaupata kwa mbinde.
Watu wanapaki, wanakupiga kimoja then wanakuacha upige pasi zako zisizo na madhara. We are better than that.
Nisiwachoshe wakuu, kilichonipoteza humu ni ile trauma ya anfield. Football isn't the same nowadays, imekua ngumu sana kusahau ile kitu.
Adios!
Sent using Jamii Forums mobile app