Hivi kwa mechi ya jana unamlaumu vipi kocha?
Team nzima iliunderperform. Kwa zile clear chances, one to one na golikipa zaidi ya tatu huwezi kumlaumu Valverde.
Jana hata King Messi hakua kwenye ubora. Amekosa nafasi kadhaa ambazo hua hakosi hata akifumba macho.
Hatuwezi kushinda mechi zote, hatuwezi kucheza vizuri mechi zote. Cha muhimu ni kupata matokeo pale tunapoyahitaji zaidi.
Subiri muone kesho kutwa atakachofanywa Lyon, hua tunabadilika kulingana na mtu tunaecheza nae.
By the way, Girona kawapakata majirani huko. Gepu linazidi kukua.
- KANA -