FBI kuhusika katika kuchuja viongozi watakaompokea Obama

FBI kuhusika katika kuchuja viongozi watakaompokea Obama

Achakua mtumwa mTZ mwenzangu, hata mimi ninge kua nina cheo cha waziri mkuu ninge goma kwenda kumpokea huyo SHETANI. Kwanza wanaendelea kumuona mwafrica si chochote, kutaka kukabidhiwa mamlaka ya uwanja wa ndege yani wenyewe wawe ndio wasimamizi wa kuu wa shughuli zote ziendeleazo hapo uwanjani ni kuthibitisha kwamba sisi hatuna ulinzi ulio kamilika. Kama hatuwezi kujilinda maanayake jeshi letu ni dhaifu, sasa haya sio matusi? Nachukia sana mtu asie tambua thamani yake.
Ni kweli jeshi letu ni dhaifu kama tunashindwa kulinda mkutano wa chadema ulinzi wa Obama tutauwezea wapi? Utachukia sana lakini huo ndo ukweli
 
wana usalama wa marekani wana fwatilia mambo mengi sana hapa bongo....wanajua mbich na mbivu, .....wale vituko wetu pia wanajulikana, mwigulu, nape, kinana, wassira na ngamia wasahau kuwapo.
 
Kikwete alikuwa UK juzi juzi hata gazeti la Evening Standard linalogawiwa bure hawakuandika chochote kuhusu Kikwete. Mkuu nakukubalia Africa tuna miaka 2000 kufikia walipo wenzetu sasa hivi. Na bado kuna watu wanajidanganya ukiwa na pesa Dar kama huko New York thubutu!

toba huu ni uzalilishaji.....imenisikitisha alivyo pokelewa Singapol...ni aibu wakuu
 
Hivi kwa nini Zanzibar haipo kwenye ratiba ya Obama wakati ni sehemu ya Jamhuri?

Je huu sii ubaguzi??

Zanzibar inaandaliwa mazingira ya Uhuru kamili. So mtafuten Obama wakati mtakapoona inafaa sio lazima mletewa na watanganyika. Bwahahahaha
 
Ndugu wana jf nimejiuliza sijapata majibu naomba ufafanuzi kwa suala hili la ujo wa obama. Kwa kawaida huwa najua mgeni anapomtembelea mwenyeji anakuta ameshaandaliwa kila kitu hapo ugenini lakini kwa mgeni wetu huyu obama naona mambo ni tofauti!
 
sawa kabisa Obama usikubali kumshika mkono mwigulu chemba, nape, lukuvi, na wasira hawa ndo wanaratibu mauaji hapa nchini

Bila kumsahau Lwakatare anaehusishwa na ugaidi na yule mbunge wa Arusha anaechochea machafuko! Mr. Obama usimsalimie Slaa huyu ndie mzizi wa Fitina aliyetangaza nchi kutotawalika!!!
 
Achakua mtumwa mTZ mwenzangu, hata mimi ninge kua nina cheo cha waziri mkuu ninge goma kwenda kumpokea huyo SHETANI. Kwanza wanaendelea kumuona mwafrica si chochote, kutaka kukabidhiwa mamlaka ya uwanja wa ndege yani wenyewe wawe ndio wasimamizi wa kuu wa shughuli zote ziendeleazo hapo uwanjani ni kuthibitisha kwamba sisi hatuna ulinzi ulio kamilika. Kama hatuwezi kujilinda maanayake jeshi letu ni dhaifu, sasa haya sio matusi? Nachukia sana mtu asie tambua thamani yake.

Ulinzi wetu si dhaifu kwa viwango vyetu vya kibongo, lakini ulinzi wetu ni dhaifu mno kwa viwango vyao, yaani wanaona tuko nyuma miaka 60 kwenye ulinzi! Kuna mzungu mmoja anaandika makala kwenye gazeti moja la kila wiki anasema hata ndege zetu za ulinzi ni zile za miaka ya sitini au early 70's. Na kwa jinsi hii tunathibitisha hatuwezi kuwapa ulinzi wanaoutaka.
 
obama anakuja kuongea na wenye mbwa,hajaja kuongea na mbwa. Period

Halafu wakati mwingine muwe mnafikiri SURA ZA WATU WENGINE ZINATIIIISHAAA!!! Hivyo sidhani kama FBI watakubali Obama alale anaota majinamizi!!!!!!
 
Kwa hiyo wanaweza kupitisha chochote au yeyote kuingia au kutoka nchini. Hii balaaaaaa
 
Nimeipenda xana kwani watu kama "babu wanzita -wasira" , "lukuvi" "guu la chemba"-mwigulu, wata enguliwa mapeeeemaaa xana kwani watakuwa kwenye "data base " ya wazee wakazi kutokana na matukio yao wanayoyafanya na pia walipokuwa wanachunguza "matukio tata " ambayo yalikosa majibu kwa wa tz. kama hawaamini basi waende waone mbele ya mkulu wa dunia waone watavyoumbuka.
 
tunajirahisi sana kama malaya sijuhi sisi weusi tukoje kama vimbwa koko vile,ukiwaona wanajifanya mara mikakati ya bara mara africa tujitegemee kumbe ujinga kabisa.. mpaka ndege uwanja mzima waongoze wenyewe? this is crazy.
 
WaTZ tufanyeni kazi kwabidii tulijenge Taifa letu kwamanufaa yetu na vizazi vyetu vijavyo,maswala ya ujio wa Obama tusiayape umuhimu wowote. Ujio wake umejaa dharau na kebihi kwa mwafrica nisawa nakusema kaja kututia ujinga tu.
 
Mkurugenzi wetu wa TISS na Ramadhan Ighondu wake nao kwisha habari yao!
 
Pamoja na kwamba hilo ni Tusi kwetu kama Taifa, na pia Tusi kwa vyombo vyetu vya "Ulinzi & Usalama" ila kwa kweli tunastahili Tusi hilo! Hebu jiulize ni matukio mangapi yaliyotokea karibuni hapa Nchini na Vyombo vyetu vya Usalama wakayabatiza ni ya "Kigaidi" na mpaka sasa hamna yeyote aliyeweza kuthibitishwa kuhusika nayo? Jiulize Mahakamani kuna kesi ngapi sasa zilizobatizwa ni za "Kigaidi"??? Katika hali ya namna hiyo unatarajia wao wasichukue tahadhari ya kumlinda Raisi wao? Tafakari!!!
 
FBI wanajua ndani ya viongozi wa nchi hii kuna magaidi.Hebu tuangalie watakaochaguliwa ndipo tutajua nani kaachwa.
 
Mkurugenzi wetu wa TISS na Ramadhan Ighondu wake nao kwisha habari yao!

Hata Cha mgonjwa-Chagonja,Saidia uwe Mwema-Said Mwema nao hawatakuwepo?Maana record zao za utendaji katika jeshi la polisi si za kuvutia hata kidogo,Na ofisi ya Balozi wa Marekani ina taarifa zote za ki-Intelijensia maana yule Balozi ni Afisa wa Jeshi mstaafu wa Marekani na yupo Afrika kwa kazi maalum kwaajili ya Nchi yake.
 
Back
Top Bottom