- Source #1
- View Source #1
Fatma Karume kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa X-Twitter ameandika kuwa " Vyama vya Upinzani vinapaswa kujenga uhusiano thabiti na wadau wakubwa wa ndani ya nchi ili kupata nguvu na rasilimali za kuendesha harakati zao. Kuishambulia CCM pekee si mkakati wa ushidi angalieni mfano wa Trump aliyepata msaada mkubwa kutoka kwa matajiri kama Elon Musk. Siasa ni mkakati si malalamiko
- Tunachokijua
- Fatma Karume ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea, mwanaharakati ambaye aliwahi kuwa rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) katika kipindi cha mwaka 2018 hadi 2019. Alipata wadhifa huo baada ya kushinda katika uchaguzi wa uraisi wa chama hicho uliofanyika Aprili 2018.
Agosti 12, 2025 chama cha mapinduzi CCM kilifanya harambee iliyokuwa na lengo la kukusanya kiasi cha shilingi Bilioni 100 kwa ajili ya mchakato wa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025.
Mara baada ya zoezi hilo watu mbalimbali wlaikuja na maoni tofauti ikiwemo vyama vya upinzani waliokuwa wanahoji jambo hilo na uwepo wa matajiri wakubwa waliojitolea kuchangia viwango mbalimbali vya fedha.
Madai
Kumekuwa na grafiki yenye nembo ya chombo cha habari cha Mwanahalisi ikieleza kuwa Fatma Karume kupitia ukurasa wake wa X amechapisha taarifa kuwaambia wapinzani waache kulalamika na badala yake watafute wadau wakubwa wa kuwapa misada.
Uhalisia wa Taarifa hiyo
JamiiCheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli.
Kupititia utafutaji wa maneno muhimu, JamiiCheck imejiridhsiah kuwa taarifa hiyo haijachapishwa na Mwanahalisi katika kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii. Aidha
Aidha ufuatiliaji kwa njia ya mtandao imebainika kuwa Fatma Karume hajaandika maneno hayo kupitia ukurasa wake wa X na hivyo ‘screenshot’ inayoonekana kuambatanishwa kwenye grafiki hiyo ni ya kughushi.