Fatma Karume: Dk Shein Siyo Rais wa Zanzibar

Mwanahalisi!?

Wenye ile Elimu yetu ya hapa na pale!!
Hayaa tumewasikia, kakojoeni mlale!
Mkumbuke kushusha chandarua
 
Huyu mama anahitaji uangalizi maalum wa wanasaikologia walio bobea kumshauri huyu mama anakoelekea kutamgharim!
 
Hata tufanyeje uchaguzi hauwezi kurudiwa tena mkuu!

Ni kweli, ila lazima tuwe aware na consequence ya nn kinaweza kutokana na tunayoyafanya now!! Ni dhahili kuna watu (watu wengi) hawajaridhika na yaliyotokea znz, hii arrogance ambayo chama tawala na wafuasi wake wanaionesha inaweza ikawa ndio kuni ya kuchochea hasira ambazo wafuasi wa CUF bado wanazo.
 
Anapata wapi nguvu zakusema? Lazima kuna kitu nyuma ya pazia. Familia yao inakula na kunywa kwa pesa ya serikali sasa mtu kama huyu kuna haja kumchunguza anapat wapi hizo nguvu? Na nikwamasilah yanan anasema hayo?
...................
 
Alafu mbaya kuliko yote anasema maneno hayo akiwa Znz, wakati mtu kasha apishwa kisheria. Kwakwel huu ni uhaini ambao unapaswa kukemewa. Mböa hakusema hayo wakat wa kaka yake?
Uliposoma hiyo habari hukuona sehemu inasema kasema maneno hayo kwa uchungu akiwa ofisini kwake Dar es salaam ??
Kaka yake yupi unaye msemea ???
 
MJUKUU wa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, Abeid Amani Karume, amepinga hatua ya kumtangaza Dk. Alli Mohammed Shein, kuwa rais Visiwani, anaandika Pendo Omary.

Fatma Amani Abeid Karume, mtoto wa kwanza wa rais mstaafu, Amani Abeid Karume amesema, “Dk. Shein, siyo kiongozi halali wa Zanzibar. Amewekwa madarakani na jeshi na kinyume na Katiba na taratibu za nchi.”

Amesema, “Rais aliyewekwa madarakani na vyombo vya dola, siyo rais wa wananchi. Rais anayewekwa madarakani kwa nguvu za kijeshi na vitisho, hawezi kuwa rais wa wananchi. Anakuwa rais wa majeshi.”

Akiongea kwa sauti ya uchungu na MwanaHALISI Online, Jumatano wiki hii, ofisini kwake, jijini Dar es Salaam, Fatma amesema, “Chama Cha Mapinduzi, kisijidanganye. Zanzibar siyo shwari. Kinachotengenezwa sasa, siyo utawala. Ni muendelezo wa chuki, visasi na uhasama.”

Amesema, “CCM ya Tanganyika, ndiyo inayoiharibu Zanzibar. Wanalazimisha viongozi wasiokubalika na wananchi Visiwani kutawala kwa manufaa yao binafsi.”

Soma mahojiano kamili na mwanasheria huyo mashuhuri nchini, katika gazeti la MwanaHALISI Jumatatu wiki ijayo.

Mwanahabari Huru
 
Awali nilidhani unatoa taarifa ya mahojiano kati ya mnufaika na Mwanahalisi!

Kumbe wewe ndo mwanahali mwenyewe, umepost na umekomaa kuchangia mwenyewe! Au ndo mumewe Fatuma?
Kisu mfupani rejea mombasa tu hapa huwezi elewa
 
Anapata wapi nguvu zakusema? Lazima kuna kitu nyuma ya pazia. Familia yao inakula na kunywa kwa pesa ya serikali sasa mtu kama huyu kuna haja kumchunguza anapat wapi hizo nguvu? Na nikwamasilah yanan anasema hayo?

Tukumbuke huyu ni mtu mzima, na anayejitegemea. Kama kuna mtu anakula kwa mgongo wa serikali basi ni baba yake na mama yake, ila si yeye!! Huyu ni wakiri, tena wa kujitegemea. Kudhani kuwa bado analishwa na baba yake ni kumtusi.

Kuna watu watasema alisoma kwa kutumia pesa za serikali😱. Ndio, ila haya sasa ndio matunda ya elimu ambayo aliipata, kuusimamia ukweli pasipo kuogopa wala kuegemea upande wowote. Hakika mzee wake hakupoteza pesa zake (kama alimlipia private)

Hata hivyo tukumbuke hata Zitto Kabwe, Mnyika, Lema, Mdee na baadhi ya wanasiasa na watu wengi ambao wako kinyume na serikali nao pia walisoma kwa kutumia pesa za serikali, ni wajibu wa serikali kusomesha watu wake. Kusomeshwa na serikali hakumaanishi kuwa mwanasesere wa serikali na kusema ndio kwa serikali katika kila jambo.
 
MJUKUU wa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, Abeid Amani Karume, amepinga hatua ya kumtangaza Dk. Alli Mohammed Shein, kuwa rais Visiwani, anaandika Pendo Omary.

Fatma Amani Abeid Karume, mtoto wa kwanza wa rais mstaafu, Amani Abeid Karume amesema, “Dk. Shein, siyo kiongozi halali wa Zanzibar. Amewekwa madarakani na jeshi na kinyume na Katiba na taratibu za nchi.”

Amesema, “Rais aliyewekwa madarakani na vyombo vya dola, siyo rais wa wananchi. Rais anayewekwa madarakani kwa nguvu za kijeshi na vitisho, hawezi kuwa rais wa wananchi. Anakuwa rais wa majeshi.”

Akiongea kwa sauti ya uchungu na MwanaHALISI Online, Jumatano wiki hii, ofisini kwake, jijini Dar es Salaam, Fatma amesema, “Chama Cha Mapinduzi, kisijidanganye. Zanzibar siyo shwari. Kinachotengenezwa sasa, siyo utawala. Ni muendelezo wa chuki, visasi na uhasama.”

Amesema, “CCM ya Tanganyika, ndiyo inayoiharibu Zanzibar. Wanalazimisha viongozi wasiokubalika na wananchi Visiwani kutawala kwa manufaa yao binafsi.”

Soma mahojiano kamili na mwanasheria huyo mashuhuri nchini, katika gazeti la MwanaHALISI Jumatatu wiki ijayo.

Mwanahabari Huru

shikamoo mwanangu Fatma.
 
Tukumbuke huyu ni mtu mzima, na anayejitegemea. Kama kuna mtu anakula kwa mgongo wa serikali basi ni baba yake na mama yake, ila si yeye!! Huyu ni wakiri, tena wa kujitegemea. Kudhani kuwa bado analishwa na baba yake ni kumtusi.

Kuna watu watasema alisoma kwa kutumia pesa za serikali😱. Ndio, ila haya sasa ndio matunda ya elimu ambayo aliipata, kuusimamia ukweli pasipo kuogopa wala kuegemea upande wowote. Hakika mzee wake hakupoteza pesa zake (kama alimlipia private)

Hata hivyo tukumbuke hata Zitto Kabwe, Mnyika, Lema, Mdee na baadhi ya wanasiasa na watu wengi ambao wako kinyume na serikali nao pia walisoma kwa kutumia pesa za serikali, ni wajibu wa serikali kusomesha watu wake. Kusomeshwa na serikali hakumaanishi kuwa mwanasesere wa serikali na kusema ndio kwa serikali katika kila jambo.
Asante sana hawa ccm mawazo yao ni dumavu
 
Wewe fatma mbona wakati babako anasaidiwa na CCM huku bara kuiba kura ili amshinde Maalim Seif hukupanuwa hilo domo lako?
 
Back
Top Bottom