Fatma Karume: Dk Shein Siyo Rais wa Zanzibar

Fatma Karume: Dk Shein Siyo Rais wa Zanzibar

MJUKUU wa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, Abeid Amani Karume, amepinga hatua ya kumtangaza Dk. Alli Mohammed Shein, kuwa rais Visiwani, anaandika Pendo Omary.

Fatma Amani Abeid Karume, mtoto wa kwanza wa rais mstaafu, Amani Abeid Karume amesema, “Dk. Shein, siyo kiongozi halali wa Zanzibar. Amewekwa madarakani na jeshi na kinyume na Katiba na taratibu za nchi.”

Amesema, “Rais aliyewekwa madarakani na vyombo vya dola, siyo rais wa wananchi. Rais anayewekwa madarakani kwa nguvu za kijeshi na vitisho, hawezi kuwa rais wa wananchi. Anakuwa rais wa majeshi.”

Akiongea kwa sauti ya uchungu na MwanaHALISI Online, Jumatano wiki hii, ofisini kwake, jijini Dar es Salaam, Fatma amesema, “Chama Cha Mapinduzi, kisijidanganye. Zanzibar siyo shwari. Kinachotengenezwa sasa, siyo utawala. Ni muendelezo wa chuki, visasi na uhasama.”

Amesema, “CCM ya Tanganyika, ndiyo inayoiharibu Zanzibar. Wanalazimisha viongozi wasiokubalika na wananchi Visiwani kutawala kwa manufaa yao binafsi.”

Soma mahojiano kamili na mwanasheria huyo mashuhuri nchini, katika gazeti la MwanaHALISI Jumatatu wiki ijayo.

Mwanahabari Huru
Fatma atulizane tuu, baba yake mbona alikuja kwenye kuapisha? amuulize bibi take
 
Alafu mbaya kuliko yote anasema maneno hayo akiwa Znz, wakati mtu kasha apishwa kisheria. Kwakwel huu ni uhaini ambao unapaswa kukemewa. Mböa hakusema hayo wakat wa kaka yake?
 
Kwani yeye ni nani mpaka apinge maamuzi ya Jecha salum Jecha!?

Kwanza siyo lazima amtambue Dr shein,kumbuka hata UKAWA hawamtambui Magufuli lakini wanamuomba asaidie suala la Zanzibar!
kwani ww ni nani mpaka uyakubali maamuzi ya jecha?
 
Angeyasema maneno wakati baba yake akiuwa watu pemba na kusababisha wakimbizi kukimbilia Kenya hadi Somalia tungemuelewa. Kwani hata baba yake ni muendelezo huohuo tu wa madaraka . Na huyo binti ni mnufaikaji na siasa hizo chafu za Zenj. Anajaribu kusoma upepo wa kuokoa mambo
 
Attachments

  • FB_IMG_1458926222112.jpg
    FB_IMG_1458926222112.jpg
    35.1 KB · Views: 48
Baba yake kapiga kura ....ndio dola anayoongelea hiyo
 
Alafu mbaya kuliko yote anasema maneno hayo akiwa Znz, wakati mtu kasha apishwa kisheria. Kwakwel huu ni uhaini ambao unapaswa kukemewa. Mböa hakusema hayo wakat wa kaka yake?
Kaka yake yupi huyo aliyewahi kuwa rais.?
 
Uchaguzi umeisha tufanye kazi tulijenge Taifa letu.
Kwanza hata asipo mtambua hapunguzi kitu!

"Youngblood" kama jina lako lilivyo, unaonekana hauna weredi katika kutazama haya mambo!! Chaguzi ambazo huwa zikiisha watu wanarudi katika kujenga nchi ni zile zinazofanyika katika hali ya amani au malidhiano yanayohafikiwa na pande zote! Historia ya dunia inatuonesha kuwa chaguzi zenye mfanano na huu wa zanzibar ulioisha juzi huwa zinaacha madonda makubwa ambayo huchukua muda kupona.

Watu wanaanza vipi kujenga nchi kama baadhi wanaamini kabisa wameporwa haki yao?!😱

Ila kwasasa sisi tunaopinga jinsi uchaguzi ulivyofanyika tunaonekana mabwege! But soon or later yatatokea mambo ambayo utaelewa kwanini ninasema Zanzibar haiwezi kuwa shwari katika mazingira ambayo baadhi wanaamini wamedhulumiwa ndani ya nchi yao wenyewe!
 
Hata tufanyeje uchaguzi hauwezi kurudiwa tena mkuu!
 
Ni maoni yake binafsi, nayaheshimu. Lakini si lolote si chochote kwa watanzania zaidi ni wale wenye mtazamo kama wake ambao ni wengi pia
 
Angeyasema maneno wakati baba yake akiuwa watu pemba na kusababisha wakimbizi kukimbilia Kenya hadi Somalia tungemuelewa. Kwani hata baba yake ni muendelezo huohuo tu wa madaraka . Na huyo binti ni mnufaikaji na siasa hizo chafu za Zenj. Anajaribu kusoma upepo wa kuokoa mambo
kuna sentensi mmoja kwenye hayo maelezo anasema "ccm ya Tanganyika ndio inaiharibu Zanzibar"hii sentensi inafikirisha sana
 
Anapata wapi nguvu zakusema? Lazima kuna kitu nyuma ya pazia. Familia yao inakula na kunywa kwa pesa ya serikali sasa mtu kama huyu kuna haja kumchunguza anapat wapi hizo nguvu? Na nikwamasilah yanan anasema hayo?

Lakini kula na kunywa kwa mgongo wa serikali isiwe sababu ya kukaa kimya hata kama mambo hayako sawa.

Hawa wanaopata vya bure wanatakiwa watuonee huruma na kodi zetu.
 
Back
Top Bottom