ustadhijuma
JF-Expert Member
- Jul 20, 2015
- 3,133
- 2,117
Katika chapisho lenye maneno makali kwenye mtandao wa X (zamani Twitter), mwanasheria na mwanaharakati mashuhuri Fatma Karume amemshambulia vikali Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima, kwa nia ya kutaka “misikiti igeuzwe kuwa Sunday Schools.”
Kauli hiyo imeibua mjadala mzito kuhusu uhuru wa ibada, na chuki za kidini nchini zinazoenezwa na kiongozi huyo wa kanisa.
Fatma amelaumu unafiki wa baadhi ya watu wanaomuita yeye mdini kwa kuhoji matamshi ya Gwajima, ilhali Gwajima ambaye amewahi kupendekeza kufungwa kwa misikiti na kuigeuza kuwa Sunday Schools hapati lawama, bali anapewa sifa za "shujaa" kwa kukemea tukio moja tu la utekaji.
“Yeye anayetaka kufunga misikiti si mdini, bali ni hero wenu kwa kuwa alidiriki kukemea utekaji mara moja tu. Mie niliyekemea consistently, mie ndiye mdini? Shukran ya punda mateke!” ameandika Fatma kwa hisia kali.