Fathima Godabar; Mwanamke anayeongoza kwa uzuri duniani

Fathima Godabar; Mwanamke anayeongoza kwa uzuri duniani

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,077
Reaction score
34,850
Fathima+Kulsum+Saudi+Arabia+queen+3.jpg



Fathima+Kulsum+Saudi+Arabia+queen+1.jpg



KWA UFUPI

Licha ya kujifunika mwili wake wote kwa mavazi yenye stara, hiyo haijawa sababu ya kuficha uzuri

wa asili mwanadada huyu, ambaye kwa sasa anaonekana kuwa mzuri zaidi akilinganishwa na

wanawake wote duniani.



Licha ya usemi unaosema uzuri upo machoni kwa mtu, lakini ukweli utabaki palepale kwamba kitu au mtu hadi kuonekana mzuri, lazima kiwe kimekubalika na watu wengi.

Wengi tumekuwa na fikra kuwa pengine Angelina Jolie na Aishwarya Rai, ndiyo wanawake wazuri duniani. Hiyo imesababishwa na umaarufu walionao walimbwende hao.

Lakini, umaarufu siyo kigezo cha kuwa mzuri kwani wapo watu wazuri mno na hawatambuliki, kwa sababu tu hawana umaarufu kama ilivyo kwa Angelina Joliea au Aishwarya Rai.

Miongoni mwa watu hao ni Fathima Zohar Godabari, raia wa Saudia Arabia, anayesadikiwa kuwa mwanamke mrembo kuliko wote walio duniani kwa sasa.

Licha ya kujifunika mwili wake wote kwa mavazi yenye stara, hiyo haijawa sababu ya kuficha uzuri wa asili mwanadada huyu, ambaye kwa sasa anaonekana kuwa mzuri zaidi akilinganishwa na wanawake wote duniani.

Mwonekano wa sura yake, urefu na wembamba wa wastani unatosha kudhihirisha mvuto wa hali ya juu alionao Fathima. Rangi ya ngozi, uzuri wa nywele na midomo yake inatosha kueleza na kukubali kuwa ndiye mrembo zaidi duniani kwa sasa.

Mrembo huyu anatoka katika familia ya kifalme ya nchini Saudi Arabia akitajwa pia kuwa mstari wa mbele kushiriki katika masuala yenye manufaa kwa wanawake.

Godabari pia ni mwanaharakati anayejihusisha na utetezi wa haki za wanawake na mshauri anayewakusanya wanawake katika makundi madogo madogo kwa lengo la kujisimamia na kupingana na aina yoyote ya ukatili dhidi yao.

Licha ya urembo na moyo wa kujitolea alionao, Godabari anatajwa pia kuwa ni miongoni mwa wanawake wachache kutoka nchi za kiarabu waliofanikiwa kupata kiwango cha juu cha elimu.

Kwa hivi sasa yuko nchini Uingereza ambapo anachukua shahada ya uzamili katika masomo ya uongozi wa biashara.Fathima Zohar Godabari alizaliwa Oktoba 22,1986 nchini India. Kwa sasa amefunga ndoa na Sheikh Awadi Al Muhammad wa ukoo wa kifalme nchini Saudia Arabia.


Imeandaliwa na Elizabeth Edward.chanzo. Fathima Godabar; Mwanamke anayeongoza kwa uzuri duniani - Makala - mwananchi.co.tz



 
Beauty is not having a preety face...it's about having preety mind,heart and most importantly, a beautiful soul....lakin watu wengi huzani uzuri wa mwanamke ni lazima aweke wazi mwili wake...wakati mwanamke bado ni mzuri katika vazi la heshma..
farkhina mbona unanimix, mara useme sio sura ni soul and pretty heart. Hapa tumeoneshwa sura pekee na ndio imetumika kujaji kuwa huyu ni mzuri. Usipindishe ukweli wa MziziMkavu labda kama mmeamua kupiga promo hijabu.

Na kama sio sura mbona hizo sifa zingine hazijawekwa?
 
Last edited by a moderator:
Kwani uzuri wa mwanamke ni kitu gani? kam sio uso? unataka mpaka uone kwa ndani?ili iweje Mkuu?

Uzuri sio sura, kuna shape, tabia, sauti, kutembea, mambo ya kikubwa & jinsi mtu anavyoishi na watu.

Ofcoz kuna watu ambao ni kweli wazuri kwa vingi na wanaonekana hivyo na wengi. Lakini huyu nilichoona hapo ni sura ukute hata haoleweki huyo
 
Hakuna mwanamke mzuri ka mke wangu, KWISHAAA!!

hizo nyingine stori tu msifie sura na hadi dada zetu wanatumia carolite kisa wanaamini uso ndio icon/signature ya uzuri.

Zile hijabu za kininja nazipenda sana Washawasha
 
Last edited by a moderator:
sasa mbona sura tu jamani.....wamfunue tuone bana.....sasa tutapima vipi?
ana kauso kazuri lakini uzuri si uso tu..tuona usafiri, shep, nk

mix with yours
 
Kila mtu duniani ni mzuri, inategemea wewe uzuri wa mtu unaangalia nini, wengine sura ya kawaida lakini ana tabia nzuri, roho nzuri, ana huruma ana upendo na shepu yake si haba zaidi anahofu ya Mungu, maisha yake ni ya kumtegemea Mungu, mtu kama huyo kwangu ni mzuri. Mwingine ni akicheka dimpose zake zinamfanya aonekane mzuri kuliko japo ni wa kawaida, mwingine ana mguu mzuri na mrefu wa wastani pia ni mzuri.
Kwangu sura si kigezo pekee cha kumuona mtu ni mzuri, huenda huyo unayemuona mzuri wa sura akivaa nguo ya kawaida ya heshima tu, huwezi kuamini maana ataonekana tofauti kuliko ulivyofikiria.
 
kiukweli kwa kigezo hicho cha sura dada huyo ni mzuri sana, ila dhana ya kusema kuliko wote duniani hapa natatanika kwani aliyetoa hilo jumuisho ameshatembea duniani kote? naamini wapo wazuri pengine kumpita ambao hawajapata fursa ya kuonekana na wengi.
 
Back
Top Bottom